in , ,

Messi amkwida mchezaji

 

*Mourinho ahofia kikosi

 

Mchezaji anayeheshimika duniani, Lionel Messi wa Barcelona amezua tafrani baada ya kumpiga kichwa mchezaji wa Roma kwenye mechi ya kirafiki.

 

Messi aliingia matatani kwa kumpiga mchezaji wa zamani wa Newcastle, Mapou Yanga-Mbiwa kabla ya kusonga mbele na kufunga kwenye mechi ambayo Barca walitoka na ushindi wa 3-0.

 

Messi alionekana mwenye hasira ambapo kwanza alimkaba beki huyo Mfaransa kabla ya kumsukuma, na ilikuwa bahati kwamba hakupewa kadi nyekundu.

 

Wawili hao walitenganishwa na mchezaji wa Roma, Leandro Castan na mwamuzi Javier Estrada Fernandez, kabla ya kuwapa kadi ya njano.

 

Yanga-Mbiwa alionekana kumchezea rafu Messi ambaye hakupendezwa na kuamua kuchukua hatua mkononi

 

MOURINHO AHOFIA KIKOSI CHAKE

Jose
Jose

Chelsea wamemaliza mechi za kujiandaa na msimu mpya pasipo kushinda hata moja, na kocha Jose Mourinho ameeleza hofu juu ya kikosi chake.

 

Chelsea wamecheza mechi tani, kupoteza tatu na kwenda sare mbili ambapo Mourinho anasema wasiwasi wake ni juu ya hali ya mshambuliaji wake wa kati, Diego Costa.

 

Mchezaji huyo wa Hispania ameumia tena misuli ya paja na hakuna uhakika iwapo atakuwa dimbani kwa ajili ya mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya England wikiendi hii.

 

Mourinho amesema anashangaa kwa nini mchezaji huyo hana utimamu wa mwili licha ya kwamba alipata muda wa kupumzika. Wakati mwingine amekuwa akimchezesha hata kama ana hitilafu kidogo kwani ni tegemeo lake kubwa.

 

Katika mechi ya mwisho ya kujiandaa, Chelsea wamefungwa 1-0 na Fiorentina kupitia bao la Gonzalo Rodriguez kwenye mechi ambayo beki wa Chelsea Kurt Zouma ambaye Mourinho anamkuza alicheza rafu mbaya na nusura apewe kadi nyekundu.

 

Mourinho amesema mechi ya kweli ni Jumamosi ijayo wakati watakwaana na Swansea kwenye mechi ya kwanza ya kutetea ubingwa wao.

 

“Soka ya kweli ni Jumamosi kwa sababu leo hatungeweza kukabili mechi hii tofauti na tulivyofanya. Wale wanaocheza wikiendi wamepata dakika 30 tu na ambao hawatacheza niliwapa dakika 60. Natumaini hapatakuwapo majeruhi. Nilimwona Eden Hazard akichechemea lakini sidhani kwamba kuna tatizo,” akasema Mourinho.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Usajili EPL wafikia £500m

West Ham nje Europa