in

Mechi kumi zilizompa ubingwa Liverpool

10: May 2, 2019

Newcastle 2- 3 Liverpool

Liverpool kabla ya hii mechi walikuwa wametoka kupokea kichapo cha goli 3-0 kutoka kwa Barcelona kwenye mechi ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

Walienda St. James Park wakiwa na kumbukumbu ya kichapo hicho , kumbukumbu ambazo ziliwafanya kwenye hii mechi kupata ushindi mida ya jioni sana .

Mpaka dakika ya 89, mechi ilikuwa 2-2, magoli ya Liverpool yakiwa yamewekwa na Virgil Van Djik na Mohammed Salah huku magoli ya Newcastle United yakiwa yamewekwa na Solomon Rondon.

Divock Origi aliingia zikiwa zimebaki dakika chache mpira kumalizika na alifanikiwa kufunga goli dakika ya 89 na kuipa ushindi Liverpool wa magoli 3-2, ushindi ambao uliwaepushia kuacha alama,  wiki moja baadaye walikuja kuwafunga Barcelona magoli 4-0 huku Divock Origi akiwa shujaa.

9: August 17

Southampton 1-2 Liverpool

Mechi hii Liverpool alikuwa anakabiriwa na majeraha ya golikipa wao namba moja , Allison Backer huku golikipa wao namba mbili Adrian naye alikuwa na majeraha lakini alicheza mechi hii.

Mechi hii Roberto Firmino na Saido Mane waliipa ushindi Liverpool licha ya Dany Ings kufunga goli la Southampton. Siku hii Manchester City walitoka sare na Tottenham Hotspurs ya magoli 2-2 , na kuwafanya wapoteze alama huku wapinzani wao Liverpool wakifanikiwa kutopoteza alama.

8: September 22

Chelsea 1-2 Liverpool

Mechi ya kwanza ya ushindi ya mashindano ya Jurgen Klopp kama kocha wa Liverpool ilikuwa dhidi ya Chelsea. Lakini kwenye mechi ya msimu huu akakutana na ushindani mkubwa.

Mechi ilidumu kwa goli 1-1 kwa muda mrefu , lakini Trent Alexander Arnord alipiga krosi dakika za mwisho , krosi ambayo ilimfikia Firmino na kufunga goli la ushindi na kuiokoa Liverpool kutopoteza alama.

7: October 5, 2019

Liverpool 2-1 Leicester City

Mechi ambayo mpaka dakika za nyongeza ambazo ziliongezwa mbili , Liverpool na Leicester City walikuwa 1-1 lakini mpira ukiwa unaelekea mwishoni Saido Mane aliangushwa kwenye eneo la hatari kisha James Milner akafunga hili kwa njia ya penati.

6: November 2 , 2019

Aston Villa 1-2 Liverpool

Siku hizi timu zote mbili ambazo zilikuwa kwenye mbio as ubingwa yani Manchester City na Liverpool zilikuwa zinacheza muda mmoja.

Liverpool alikuwa ugenini akicheza na Aston Villa , wakati Manchester City alikuwa akicheza na Southampton . Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Manchester City na Liverpool wote kuwa nyuma ya goli 1.

Kipindi cha pili kilipoanza Manchester City walifanikiwa kusawazisha na kuongeza goli jingine na kuwafanya waongoze kwa goli 2-1. Kama Manchester City wangeshinda na Liverpool kufungwa basi Manchester City angekuwa nyuma ya alama tatu dhidi ya Liverpool.

Lakini Liverpool kwenye dakika za mwisho mwisho walifanikiwa kusawazisha kupitia mchezaji kutoka Senegal , Saido Mane. Mechi ikiwa inaelekea mwishoni Saido Mane alifunga goli la ushindi na kuifanya Liverpool kutopoteza alama nyingine tena.

5: November 10 , 2019

Liverpool 3-1 Manchester City

Mechi ambayo iliwakutanisha wao kwa wao , timu ambazo zilikuwa zinapewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa. Mwisho wa siku magoli ya Fabinho , Mohammed Salah pamoja na nahodha wa Liverpool , Jordan Henderson yaliwapa uhakika wa kutopoteza alama mbele ya wapinzani wao wakubwa.

4: December 26 , 2019

Baada ya Christmas,  Liverpool walitakiwa kuwapa mashabiki wao zawadi nzuri ya Christmas licha ya kwamba kipindi hicho walikuwa wametoka kushinda kombe la klabu bingwa dunia kule Qatar.

Liverpool walikaribishwa na Leicester City vijana wa Brendan Rogders . Wakati zinakutana hizi timu , Liverpool alikuwa kwenye nafasi ya kwanza huku Leicester City akiwa kwenye nafasi ya pili . Watu wengi waliitazama ni mechi kubwa lakini Liverpool waliifanya kuwa mechi ndogo kwa kuifunga Leicester City magoli 4-0 magoli ya Firmino aliyefunga mawili , James Milner na Trent-Alexander Anorld.

Siku hiyo Manchester City alifungwa na Wolverhampton Wonders magoli 3-2 licha ya kuongoza kwa goli 2-0. Hivo washindani wa Liverpool (Leicester City na Manchester City)  siku hiyo wakawa wamepoteza michezo yao na Liverpool kushinda.

3: January 19 , 2020

Liverpool 2-0 Manchester United

Ni siku ambayo Liverpool aliongeza tofauti ya alama kati yake na timu iliyokuwa inashika nafasi ya pili ambayo ni Manchester City kwa tofauti ya alama 16. Kabla ya mechi hii mashabiki wa Liverpool walikuwa wanawaambia mashabiki wa Manchester United kuwa angalieni tunavyoenda kushinda kombe.

Siku hiyo wakawaonesha namna ya kushinda kombe, achana na pasi ya Allison Backer kwa Mohamed Salah , Pasi ambayo ilisababisha goli la pili na ushindi , wakati goli la kwanza likiwa limewekwa na Virgil Van Djik .Siku hiyo Manchester City alipoteza pia dhidi ya Crystal Palace kwa goli 2-1.

2: January 23 , 2020

Wolverhampton Wonders 1-2 Liverpool

Moja ya mechi ambayo Liverpool walikuwa roho juu mwanzo hadi mwisho wa mchezo ilikuwa hii mechi. Liverpool mpaka dakika 6 za nyongeza walikuwa 1-1 na Wolverhampton Wonders lakini ndani ya dakika za nyongeza Roberto Firmino alifunga goli lililowapa ushindi na kuwafanya wasipoteze alama kwenye mchezo huu.

1: February 15, 2020

Dakika 16 zilikuwa zimebaki ili mpira uishe , matokeo yalikuwa Norwich 0- 0 Liverpool, lakini Saido Mane aliinuka kama shujaa kwa kufunga goli pekee na la ushindi kwenye mechi hiyo na kuifanya Liverpool iongoze ligi kwa tofauti ya alama 25 tena ndani ya mwezi February tu.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Bernard Morrison

Morrison anahitaji MANAGER Haraka sana..

Harmonize

Harmonize kupeleka Bongofleva bungeni?