in , , ,

Matano yanayomkabili Kylian Mbappe

Nyota wa Real Madrid, Kylian Mbappe amejikuta katika wakati mgumu baada ya kushuhudia timu yake mpya ikizabwa mabao mawili kwa nunge katika mfululizo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya katika mchezo waliokabiliana na Liverpool ya England. Kwa ushindi huo Liverpool inaendeela kusalia kileleni mwa mashindano hayo, huku ikiwa na msimu mzuri sana. katika mchezo huo Kylian Mbappe alijikuta akishindw akupchika bao baada ya penati yake kudakwa na golikipa wa miamba hiyo ya EPL. TANZANIASPORTS inaangzia masuala matano yanayomkabili nyota huyo.

Presha kubwa, mpira kichwani bila miguu

“Natakuwa na uwezo kama wewe, lakini sitaki kuwa wewe,” hiyo ni kauli wa staa wa Ufaransa na beki mahiri wa Liverpool, Ibrahima Konate alipozungumzia juu ya nahodha wake Kylian Mbappe. Wakati Konate akisema hilo, naye Jude Bellingham staa  wa Real Madrid alisema “presha inayomkabili Mbappe ni kubwa mno kuibeba,”. 

Wachezaji wote wawili wanazungumzia jambo moja ambalo linaonekana katika uchezaji wa Kylian Mbappe. Nyota huyo amefunga mabao 7 ya La Liga lakini amekuwa na kipindi kigumu kuonesha umahiri wake ulioifanya timu hiyo imnunue. Katika mchezo dhidi ya Liverpool baada ya nahodha msaidizi Lucas Vazqiez kufanyiwa madhambi eneo la hatari, mwamuzi aliashiria adhabu ya penati. Kylian Mbappe kwa kutambua ndiye staa wa timu na akiunga mkono na wachezaji  wenzake alibeba jukumu la kupiga penati hiyo lakini hafunga. Nyota huyo amekuwa akipata nafasi mara nyingi lakini ameshindwa kucheka na nyavu. Pia anakabiliana na tatizo na utulivu na umaliziaji mzuri wa kuipa mabao Real Madrid. Wengi wanasema sababu ya presha hivyo kufanya acheze mpira kichwani huku miguu ikiwa inamsaliti.

Kivuli cha Vini Jr

Hakuna ubishi kivuli cha Vinicius Junior kianendelea kutawala katika klabu hiyo licha ya nyota mpya kuingia. Msimu uliopita mastaa watatu walikuwa gumzo barani Ulaya, Rodrygo, Vini na Bellingham. Nyota hao walicheza bila namba tisa kamili hivyo wakawa wanapangwa kucheza bila kuwa na uzoefu nayo, ambapo kiufundi huitwa ‘false nine’. Belligham, Vin na Rodrygo waligawana mabao kwa wingi msimu uliopita na haikushangaza Vini na Bellingham wakiwa miongoni mwa vinara wa kuwania tuzo ya mchezaji bora. Vini amefunga mabao katika fainali mbili za Ligi ya Mabingwa na kumpa mataji mawili ya mashindano hayo. Kabla ya ujio wa Mbappe staa wa Real Madrid ni Vini amekuwa na mchango mkubwa kila anapocheza na kuipa  mafanikio timu hiyo.

Rekodi za wenzake

Mbappe anacheza na wachezaji ambao wametwaa mataji mengi. Kuanzia Jude Bellingham ambaye katika msimu wake wa kwanza amechukua Ligi ya Mabingwa, kisha wageukie Rodrygo na Vini nao wametwaa taji hilo mara mbili. Nje ya nyota hao wachezaji wa Real Madrid wamechukua Ligi ya Mabingwa hadi mara tatu na wengine nne hadi tano na kumfanya Mbappe awe mchezaji asiyte na taji la Ulaya. 

Rekodi za wenzake katika kikosi ni zinamletea presha nyingine ambapo mashabiki wanatarajia kuona kama atakuwa ndiye kinara wa timu. Hata hivyo mambo yamekuwa ndivyo sivyo.

Vivuli vya mastaa wa Real Madrid

Kuna Ronaldo De Lima halafu kuna Cristiano Ronaldo. Kwa Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji kipenzi cha Kylian Mbappe. Katika rekodi za kifalme ndani ya Real Madrid Cristiano Ronaldo anazo nyingi na kwmaba ni mlima mrefu kwa Mbappe kuweza kuzifikia. Mashabiki wanaamini wamepata “Ronaldo wa tatu” yaani kutoka Ronaldo De Lima kisha Cristiano Ronaldo na sasa Mbappe. Nyota huyu anakabiliwa na kivuli hicho kwani kiumekuwa na mvuto kwa mastaa wengi klabuni hapo. 

Naye Cristiano Ronaldo anamsifia Mbappe na anaamini ndiye mwenye uwezo wa kuzifikia rekodi zake. Lakini hali ya staa huyo wa Ufaransa imekuwa ngumu, umahiri wake katika chenga umekuwa butu, ufungaji ni butu hali kadhalika hata kiwango chake kimekuwa kibaya. Tukiachana na hao, utaona majina mengine kama Karim Benzema, Gareth Bale, David Bekcham, Zinedine Zidane ni miongoni mwa majina yenye rekodi ndani ya klabu hiyo hivyo Mbappe amekuja kwenye klabu ambayo ina mlima mrefu wa utawala katika soka na kumfanya awe na wakati mgumu kukabiliana na vivuli vya mastaa waliopita na ambao sasa wanamtupia jicho kama mmoja wa watakaoleta furaha zaidi kwa kizazi kipya.

Nafasi ya kuchezeshwa

Imezoeleka kuwa Mbappe alikuwa akicheza winga wa kushoto na ndiyo ilimpa sifa kubwa. Lakini ndani ya Real Madrid nafasi hiyo imechukuliwa na Vini kiasi kwamba Mbappe anashindwa kufuta umwamba uliopo sasa. Katikia mchezo  wa Real Madrid dhidi ya Liverpool Kylian Mbappe alipewa nafasi ya kucheza eneo analolipenda lakini hakung’ara wala kuwa tishio kwa maadui. 

Nyota huyo amekuwa akicheza katika hali ya kawaida kiasi kwamba mashabiki na wadau wa mpira wanajiuliza ni kitu gani kinachoendelea katika kichwa cha Mbappe. Lakini jambo la pili ni kuchezeshwa namba 9 ambayo hakuizoea. Mbappe anatakiwa kuongoza safu ya ushambuliaji huku winga wa kulia akiwa Rodrygo na kushoto anacheza Vini Jr, hata hivyo imekuwa vigumu kwa staa huyo kuonesha cheche zake.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Yanga Walifeli Kwenye Usajili au Benchi la Ufundi?

Tanzania Sports

Madeni yanayomkabili kocha Fadlu Davids