in , ,

Madeni yanayomkabili kocha Fadlu Davids

USHINDI wa 1-0, pointi tatu muhimu na kushikilia nafasi ya pili katika msimamo wa kundi, umemwaweka katika amzingira mazuri mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania kwenye mfululizo wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos ya Angola. Ushindi wa Simba ulikuja kutokana nja kazi kubwa iliyofanywa na benchi la ufundi na wachezaji kwa ujumla wake, lakini TANZANIASPORTS imebaini madeni ambayo kocha wa klabu hiyo Fadlu Davids pamoja na wachezaji wake wanapaswa kuyalinda kwa mashabiki na wadau wa soka.

Kapombe na Hussein wanalindwaje?

Hilo ni swlai linalotakiwa kutawala kwa benchi la ufundi. Shomari Kapombe na Mohammed Hussein wanatumika kama mawinga wa pili katika kuongeza mashambulizi dhidi ya wapinzani. Katika uchezaji wao mabeki wote wawili kwa asili wanapenda kushambulia, lakini ili wakamilishe kazi yao nao wanahitaji kulindwa. Kama ‘wing backs’ wanatakiwa kuwawezesha viungo washambuliaji na mawinga wao kudhibiti wapinzani na kuchochea mashambulizi zaidi. Lakini inapotokea timu inacheza kwa kupanua uwanja yaani pasi zinakwenda kulia na kushoto na wanashambulia kupitia pembeni kwa sababu wanajua mabeki hao wawili wanapendelea kushambulia na hivyo kuacha mwanya nyuma yao. Fadlu Davids na benchi wanatakiwa kuangalia namna bora ya kuwafanya viungo wakabaji wawili kuwalinda mabeki hao kulia-pembeni nan a kushoto-pembeni.

Ufundi ndani ya kundi

Bravos FC wamefungwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa lakini kocha wa Simba anatakiwa kuitazama timu hiyo kwa jicho la tatu. Bravos inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi lao ambao FC Costantine wanaongoza wakiwa na poiinti 3 sawa na Simba. Kiufundi Bravos walihatarisha ushindi wa Simba mara nyingi, kwa sababu mabadiliko yaliyofanywa na benchi la ufundi yalikuwa kuwarudisha nyuma mabeki wa pembeni wa Simba, Shomari Kapombe na Mohammed Hussein. 

Bravos walifanikiwa kwa kiasi fulani na wametuonesha kuwa upo udhaifu ambao unaweza kutumika kuwaumiza Simba. Kwa sababu winga wa Bravos wa upande wa kulia alikuwa kwenye shughuli pevu dhidi ya Mohammed Hussein, hali kahdalika upande wa kushoto wa Bravos kulikuwa na kazi nzito dhidi ya Shomari Kapombe. Kwahiyo kimbinu Bravos wanachezaji vizuri kwenye mfumo wa 3-4-2-1. Nyuma yao wana mabeki watatu, halafu eneo la kiungo kuna wachezaji wanne, ambapo wawili ni mabeki wa pembeni kisha wengine ni mawinga, halafu namna 8 na 10 wanakuwa karibu sana na eneo 18 za adui na kumpa nafasi mshambuliaji wao. Kifundi wanategemea zaidi kupata mabao kutokea kulia na kushoto kwa mawinga wao na viungo wa eneo la katikati huku mshambuliaji wao akiw ahana madhara ya kutisha. Ni jukumu la Fadlu Davids kuizingatia timu hiyo kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo.

Wapi acheze na namna gani huyu Edwin Balua

Kipaji cha Edwin Balua ni kikubwa na anao uwezo wa kutoa mchango katika timu. Uchezaji wake hauonekani kuwa ni maagizo ya mwalimu ama hayatendei haki kwa asilimia moja. Edwin Balua ni mchezaji kijana ambaye ana muda mrefu wa kucheza soka, lakini Fadlu Davids analo deni la kumwimarisha kinda huyo wa Simba. 

Katika mfumo wa 4-3-3 au 3-4-3 anaweza kuwa sehemu ya kiungo, vilevile katika mfumo wa 4-2-3-1 anaweza kuwa sehemu ya mawinga wa Simba wenye mchango mkubwa. Pia nyota huyu anaweza kucheza kama mshambuliaji pacha yaani namba kumi. Lakini uchezaji wake nyuma ya mshambuliaji unaathiriwa na uamuzi anaofanya kuelekea lango au kutengeneza mashambulizi, kwnai ni mwepesi kupoteza mpira au mwelekeo wa shambulizi hivyo huifanya timu ikose huduma yake katika eneo. Deni alilonalo Fadlu Davids nji kumchagulia eneo mwafaka la kumchezesha kinda huyo ambaye anakabiliwa na ushindani kutoka kwa Ladaki Chasambi na Jushoa Mutale. Edwin Balua ni silaha ambayo Simba walifanya uamuzi mzuri kumnunua lakini benchi la ufundi linapaswa kuimarisha ubora na maarifa yake. Ana asilimia nyingi za kufanikiwa.

Kuvunja rekodi

Mashabiki wa Simba wanafahamu suala la kuvuka kwneye hatua ya makundi sio habari mpya kwao. Mashabiki wa Simba pia wanafahamu kufika robo fainali sio habari mpya kwao, kwahiyo jukumu la kocha Fadlu Davids ni kuhakikisha miamba hiyo yha Afrika inafika nusu fainali au kwenda kuchukua kombe kabisa. Katika deni hili kocha wa Simba atakuwa anatazamwa kwa maana kuvunja rekodi kwani kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho, watani wao Yanga walitinga fainali na kulikosa kombe kwa tofauti ya bao moja. Mashabiki wa Simba wanataka kuona timu yao inafika angalau nusu fainali au fainali kisha kuchukua kombe hilo. Ukiangalia uzito na ukubwa wa Simba kwenye mashindano ya Kimataifa utakubaliana nasi kuwa Simba wanatakiwa kuwa na lengo moja; kutwaa kombe la Shirikisho. Hilo ni deni la Fadlu Davids.

Deni la mabao zaidi

Uamuzi wa kumwanzisha Steven Dese Mukwala ulishangaza wengi lakini kocha wa Simba amedhihirisha kuwa habahatishi katika uamuzi na mkakati wake ulikuwa na malengo mahususi. Kwa kawaida Leonel Ateba ndiye alikuwa akiongoz asafu ya ushambuliaji, lakini kwenye mchezo dhidi ya Bravos alimpa majukumu Mukwala. Hata hivyo Fadlu Davids anatyakiwa kuinoa safu ya ushambuliaji kupachika mabao ya kutosha. Kadiri timu inavyopachika mabao ya kustosha ndivyo inavyjiondoa kwenye shinikizo. Lakini timu inaposhindwa kufunga mabao inajiweka katika hatari ya kuadhibiwa. Safu ya ushambuliaji ya Simba imekosa mabao mengi kiasi kwamba ingeliweza kuondoka na ushindi mnono. Samba wanahitaji mabao ya kutosha katika mfumo wowote iwe wa kuwaanzisha washambuliaji wote wawili Leonel Ateba au Steven Mukwala.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

17 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Matano yanayomkabili Kylian Mbappe

Taifa Stars

Rekodi ya COSAFA kwenye AFCON 2025