in , , ,

Mapacha wa Simba wanapoachana

IMECHUKUA muda mrefu tangu alipoondoka Alphonce Modest katika soka la Tanzania hadi kupatikana kwa Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. Hili linaweza kuonekana ni jambo kawaida, lakini hakuna namna ambayo unaweza kubeza mchango wa kapteni wa Simba, Mohamed Hussein. Ligi Kuu Tanzania imeshuhudia nyota wengi kutoka nje ya nchi na ndani wakicheza kwa muda mrefu. 

Nafasi mbalimbali kama ushambuliaji, winga, kiungo na beki wa kati wamejitokeza wachezaji kadhaa na kupotea, lakini Mohamed Hussein amedumu katika ushindani Simba kwa kipindi cha miaka 10. Hali kadhalika pacha wake Shomari Kapombe ni miongoni mwa mabeki wakali wa Simba kama ilivyokuwa kwa Said Sued ‘Scud’. Imewachukua miaka mingi Simba kumpata Shomari Kapombe tangu walipoondokewa Said Sued katika nafasi ya beki wa kulia. 

Said Sued alikuwa miongoni mwa mabeki wakali, uwezo w akukukota mpira, chenga, kukaba muda wote wa dakika 90, kushambulia kupitia winga wa kulia, ilikuwa habari nyingine. Nyota ya Alphonce Modest ilihamia kwa Mohammed Hussein kwa kipaji, uimara, nidhamu na kutumikia Simba kwa upendo. 

Modest aliibukia Mtibwa Sugar, kisha kucheza soka bora kabisa na kuzivutia Simba na Yanga. Lakini ni kama vile kipaji chake kilikuja kuwanyima nafasi wengine kwani tangu alipoondoka kwenye soka namba tatu haikupata mchezaji wa maana. Ujio wa Mohammed Hussein uliipa Simba kujiamini na kutamba kuwa timu yenye beki bora. 

Hali kadhalika Shomari Kapombe nyota aliyetokea mkoani Morogoro ni miongoni mwa mabeki hodari wa kulia kwa kipindi cha miaka 10. Uhodari wa Kapombe si wa kubishaniwa. Uzoefu alionao sasa ni matunda ya kazi nzuri ya Simba kuendelea kumwamini na kumtunza kijana wao. 

Mohammed Hussein na Shomari Kapombe, wakiwa Simba wamelia kwa uchungu, wamefurahia ubingwa, wamecheza mashindano ya kimataifa. Wametwaa makombe mbalimbali, wameitwa kucheza timu ya taifa mara nyingi, wammecheza mashindano ya CHAN, AFCON na kadhalika. Mapacha hawa wanajua raha na karaka ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mashindano ya Kombe la Shirikisho. 

Katika wasifu wao, wamecheza fainali ya Kombe la Shirikisho. Ni miongoni mwa mabeki ambao itawachukua muda mrefu tena Simba kuwapata kama hao. Ni kama ilivyokuwa kwa Modest na Said Sued. Kila nafasi kwenye soka huwa na wachezaji ambao wanakuja na kitu cha kipekee. 

Wachezaji hao wanaleta maarifa, mwendelezo wa kiwango, kucheza kisasa kwa maana ya nidhamu na kujituma na zaidi kupigania nemba ya Simba au Taifa Stars. Kwa msingi huo mapacha hawa wa Simba kuachana kwao sasa kunaleta mjadala wa nafasi ya kulia na kushoto. 

Kwa Simba nafasi ya kulia wanaweza kusajili mchezaji yeyote, lakini hawezi kuwa kama Mohammed Hussein wala Shomari Kapombe. Hadi sasa Shomari Kapombe, anaelekea kubaki klabuni. Lakini Mohammed Hussein ameshaaga kwenye klabu hiyo na uongozi wa Simba umeshampa ‘Thank You’. 

Kibarua kilichopo sasa ni Simba kuleta mabeki bora katika nafasi hizo mbili. Nafasi ya beki wa kushoto ni dhahiri Mohammed Hussein analiacha pengo kubwa, kama itakavyokuwa kwa Shomari Kapombe. Kuondokewa na mabeki kama hawa iwe kwa pamoja ua nyakati tofauti, ni jambo la kuhuzunisha. Ni wachezaji wenye wasifu mkubwa sana barani Afrika. 

Mohammed Hussein anapendwa sana na mashabiki wa Kaizer Chiefs ya Afrika kusini. Ukitembelea katika majukwaa mbalimbali ya kimichezo ya Afrika kusini, mashabiki wa Kaizer Chiefs wanaongoza kumwongelea vizuri nahodha huyo wa zamani wa Simba. Ni nyota ambaye anawavutia Kaizer Chiefs ambayo inafundishwa na Nasredine Nabi, kocha wa zamani wa Yanga. Sifa wanazomwagia Mohammed Hussein ni kuwa mchezaji mwenye nidhamu na wasifu mkubwa, wanamwona kama nyota ambaye amechezea mashindano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho ngazi ya klabu. Wanaamini ni staa anayefaa kuchezea timu yao kwakuwa ana uzoefu mkubwa kuzidi baadhi ya nyota waliopo klabuni kwao. 

Mohammed Husseina amechota uzoefu pia kwenye mashindano ya CHAN na AFCON ambayo yanawapa wazimu mashabiki wa Kaizer Chiefs. Haijalishi Mohammed Hussein anakwenda wapi, lakini Simba kuondokewa na pacha wa Shomari Kapombe ni pengo ambalo uongozi unatakiwa kufanya kazi ya ziada kuhakikisha wanaleta beki mahiri zaidi. 

Ni nafasi ambayo kila kiongozi atakiri kuwa Mohammed Hussein amewaachia mtihani mgumu kwani kila beki atakayesajiliwa atakuwa analinganishwa na nahodha wao huyo. Hii ina maana Mohammed Hussein ameweka hadhi fulani ya kucheza katika nafasi ya beki wa kushoto, kwahiyo mashabiki wanategemea nyota mpya atakuwa kama yeye. 

Kila Simba watakapokuwa wanacheza watalinganisha beki wao na Mohamed Hussein. 

Hali kadhalika, siku Shomari Kapombe akiondoka hali itakuwa hiyo hiyo, kwamba mchezaji mpya atakayesajiliwa atatakiwa kuwa na kiwango au kuonyesha kiwango kama cha Shomari Kapombe. Watatamani kuona beki mpya akishambulia, akipiga krosi, akaitengeneza mabao na kuipa uhai Simba katika upande wa kulia. katika amzingira hayo, viongozi wa Simba nao lazima wahuzunike, kuwa miaka zaidi ya 10 kuwa na beki mwenye kiwnago kizuri na kipaji cha uhakika kama Moahmmed Hussein kisha akaondoka klabuni. 

Mohammed Hussein alianza kuichezea Simba kama kijana mdogo, lakini amewaaga Simba akiwa mwanaume wa shoka, ambaye ametumikia nyakati za furaha na huzuni. Na zaidi alikuwa kiongozi wa wachezaji mchanganyiko na wenye tamaduni tofauti kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika. 

Kuwa nahodha katika mchanganyiko wa utamaduni wa wachezaji toka nchi tofauti Afrika na kuona timu ikiwa katika hali nzuri kwa uhusiano miongoni mwa wachezaji, ni jambo la kujivunia. Ni wakati sasa Simba kufikiria maisha bila Shomari Kapombe kama inavyotokea kwa Moahmmed Hussein. Ni huzuni mapacha hawa katika nafasi ya mabeki wa pembeni kuwaona wakiachana na kila mmoja kuendelea na klabu nyingine.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

CHAN jukwaa la vipaji vipya Ligi Kuu

Kocha Romain Folz

Kocha Romain Folz katika njia ya Ramovic