in , , ,

CHAN jukwaa la vipaji vipya Ligi Kuu

Benjamini Mkapa Sradium, Dar-Es-Salaa, Tanzania

AGOSTI 2 mwaka huu Tanzania, Kenya na Uganda zinakwenda kuwa wenyeji wa Mashindo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani. Mashindano hayo yanafanyika kwenye miji ya Dar Es Salaam, Nairobi na Kampala. Timu wenyeji zinajiandaa kwa mashindano hayo huku washabiki wa soka wakiwa tayari kushuhudia mitanange hiyo na kupata burudani. Mashindano ya CHAN ni sehemu muhimu ya kuimarisha soka la Afrika ambalo limnapokuja timu za Taifa zinaundwa zaidi na wachezaji wanaosakata soka barani Ulaya na kwingineko. TANZANIASPORTS inaangazia mambo kadhaa muhimu ambayo yanatarajiwa kuimarisha Ligi Kuu Tanzania.

Wasaka vipaji

CHAN ni sehemu muhimu ambayo makocha na viongozi wanaweza kutumia kama njia ya kuvumbua vipaji vipya vya kusajiliwa kwenye timu zao. Mashindano haya yanawapunguzia gharama vilabu vya Afrika mashariki ksuafiri kwenda mataifa mengine kuwafuata wachezaji wanaowataka. Kupitia mashindano haya makocha watakuwa na nafasi ya kugundua vipaji na ubora wa wachezaji ambao wanafaa kusajiliwa kwenye timu zao. Ikiwa timu mbalimbali za Ligi Kuu zimefanikiwa kuachana na baadhi ya wachezaji ni dhahiri suala la usajili wa wachezaji wapya linakuwa muhimu zaidi. Mawakala nao watakuwa bega kwa bega kuangalia namna bora ya kupata wateja wapya ambao wataingizwa kwenye kampuni zao za usimamizi. Mawakala hao kama walivyo wasaka vipaji wengine watakuwa na jukumu la kuwaangalia kwa ukaribu zaidi wachezaji wenye viwango na ubora ambao wanafaa kuuzwa kwenye vilabu vikubwa. 

Ligi Kuu

Kama ilivyo kawaida, mashindnao haya yatakuwa na wachezaji kadhaa wanaosakata kabumbu katika klabu za Ligi Kuu Tanzania. Ni wachezaji ambao wanatambulisha ubora na viwango vya soka vilivyopo kwenye Ligi Kuu. Kwa vile Ligi Kuu ni miongoni mwa sehemu ambazo wachezaji wametumia kama jukwaa lao la kujitangaza, bila shaka yoyote wengi watatupia macho kufanya tathmini za mwisho juu ya umuhimu wa wachezaji waliokuwa wanafuatilia na ambao wameitwa kwenye timu za Taifa. Vilabu vya Ligi Kuu Tanzania vitakuwa na nafasi ya kuwaangalia wachezaji wapya wa kusajili kwa makini kuliko kutegemea kuwaita kufanya majaribio. Kwenye mashindano haya, vilabu vingi vya Ligi kuu ambavyo vina uwezo wa kusajili wachezaji wa kigeni vina fursa ya kuongeza wapya.

Kocha wa Simba

Kocha Fadlu Davids ni miongoni mwa walimu ambao wana kibarua kikubwa cha kushauri uongozi aina ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa. Tayari Simba wameachana na wachezaji kadhaa akiwemo nahodha wao Mohammed Hussein. Kwa maana hiyo Fadlu Davids na jopo lake la ufundi watakuwa na jukumu la kuangalia mashindano ya CHAN kama sehemu ya kuchota vipaji vipya kwa ajili ya kusajiliwa Simba. 

Kocha huyo anahusishwa na kumsajili mshambuliaji raia wa Cameroon, John Bosco Nchindo kutoka klabu ya Coton Sports, lakini huyo ni kati ya wale wanaowindwa na klabu ya Simba. Hivyo basi Simba watakuwa kwenye msako wa kiungo mkabaji kuziba nafasi ya Fabrice Ngoma aliyemaliza mkataba wake, Moahmmed Hussein kwenye beki wa kushoto pamoja na kiungo mshambuliaji kuchukua nafai ya Deborah Fernandez Mavambo. Kwa maana hiyo Simba pia wanatarajiwa kuwafukuzia wachezaji wa Taifa Stars ambao wanatoka vilabu vingine vya Ligi Kuu.

Vigogo vya soka

Katika suala la usajili, si la timu za Afrika amshariki peke yake bali nyingine kutoka Ligi Kubwa kama vile PSL ya Afrika kusini, Misri, Tunisia, Algeria, Morocco, Angola na kwingineko. Vilabu vya Al Ahly, Zamalek, Kaizer Chifes, Mamelodi Sundowns, Orlando Pirates, Pyramids, Raja Casablanca, Wydad Casablanca na nyinginezo zitakuwa kwenye mawindo ya wachezaji wapya wenye vipaji ili kuingia kwenye timu zao. CHAN ni sehemu ambayo hutumiwa na vigogo hawa kuimarisha timu zao hivyo ni mashindano ambayo kila mdau wa soka awe mtaalamu au shabiki anatarajia mambo makubwa katika mashindano haya.

Kutokana na kushuka kwa viwango vya uzalishaji wa wachezjai kwa vilabu vya soka Afrika, mashindano ya CHAN ni jukwaa ambalo linafaa kutengeneza mwelekeo wa vipaji vingine vinavyozalishwa kwenye vilabu mbalimbali.

Miundombinu

Kwenye mashindnao haya pia yataonyesha namna Ligi Kuu ilivyo na miundombinu ya viwanja na mazingira ili kuwavutia wataalamu zaidi. Katika suala hili bila kujali upande, wamiliki wa viwanja wanatakiwa kutengeneza hali nzuri ambayo itasaidia viongozi kuona fursa ya kuja kuweka kambi ya maandalizi ya msimu kutokana na hali ya hewa. Kwahiyo CHAN ni jukwaa ambalo linakwenda kuimarisha miundombinu ya nchi zao kama nyenzo ya kuwavutia wachezaji wa kigeni pamoja na walimu wengine.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Serie A itakuwa Ligi ya wazee

Tanzania Sports

Mapacha wa Simba wanapoachana