in , , ,

Serie A itakuwa Ligi ya wazee

KWENYE mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, klabu ya Inter Milan ilifungwa mabao ya kutosha na PSG. Yalikuwa mabao 4 ambayo yaliangusha umwamba wa Inter Milan ambayo ilitinga fainali hiyo kwa kuitupa nje Barcelona kw ajumla ya mabao 7. Mechi mbili za nusu fainali msimu uliopita zilikuwa ngumu na ambazo zilitengeneza mabao mengi zaidi. 

Kutokana na wimbi la mabao la mchezo wa kwanza, ilibashiriwa huenda Inter Milan wangeshinda kirahisi katika mchezo wa marudiano. Lakini haikuwa hivyo hadi pale Inter Milan ilipolazimika ksuawazisha dakika za jioni kisha kuongeza bao la ushindi na mchezo kumalizika kwa kuvuka hatua ya fainali.

Kwenye mchezo wa marudiano ulionyesha namna Inter Milan alivyohangaika kudhibiti damu change za Barcelona ambapo vijana wake wanakimbia kwa kasi na kuwapelekea moto mwingi kiwanjani katika mechi zote mbili. 

Ulipowadia mchezo wa fainali hali ilikuwa hiyo, Inter Milan walibugizwa mabao mengi kuliko matarajio huku wengi wakidhani kuwa kulikuwa na siku mbaya kazini kwa klabu hiyo. Hata pale kocha wao Simone Inzaghi alipokuwa anawahamasisha bado wachezaji wake hawakujizuia kuonyesha kushindwa kabisa katika mchezo huo na kuwapa ubingwa PSG. 

Sababu mojawapo ya Inter Milan kunyanaysika katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa tofauti ya umri wa wachezaji wa PSG na Inter. Hali kadhalika wachezaji wa Barcelona waliwanyanyasa sana kiwanjani Inter Milan kutokana na tofauti za umri. Wachezaji wenye umri mkubwa hutumika kama njia ya kutoa uzoefu na kucheza mechi ngumu bila kuelemewa na presha zozote. Lakini kwa wachezaji chipukizi mara nyingi huwa wanazidiwa eneo dogo lam uzoefu wa mechi kubwa na zenye ushindani. Inter Milan waliwamudu Barcelona na chipukizi wao, lakini walikwama mbele ya vijana wa PSG.

Sababu iliyotajwa ni tofauti ya umri, kwmaba wachezaji wengi wa Inter Milan walikuwa na umri wa juu ya miaka 30  huku wale wa Barcelona na PSG wakiwa na wastani wa umri wa miaka 20-28. Kwa maana hiyo PSG na Barcelona walikuwa na wachezajazi chipukizi ama vijana ambao walikuwa na nguvu za kukimbizana na wazee wa Inter Milan.

Unaweza kudhani tatizo la umri mkubwa wa wachezaji ni la Inter Milan pekee. Hata hivyo watazame ndugu zao AC Milan, ambao wametangaza kumsajili Luka Modric mwenye umri wa miaka 40 kama mchezaji wao mpya wa nafasi ya kiungo. Luka Modric ametokea klabu ya Real Madrid ambako amemaliza muda mkataba wake na kwenda Italia akiwa mchezaaji huru. Hata hivyo Lukia Modric anakuwa miongoni mwa wachezaji wenye umri mkubwa wnaojiunga na Ligi Kuu Italia na kuifanya Ligi hiyo iwe maarufu ya wazee.

Msimu uliopita Inter wamelikosa kombe la Ulaya sababu ya wingi wa wachezaji wazee. AC Milan badala ya kuliona hilo wao wameongeza mzee kwenye kikosi chao na uzisha hoja inakuwaje timu inasajili mchezaji wa umri huo huku ikitaka kushindana kwenye mashindano ya Ulaya msimu ujao? Pengine swali linaweza kuwa hivi AC Milan hawajajifunza kwa inter Milan msimu uliopita? Hawakuona namna wachezaji wenye umri mkubwa walipofikia hatua ya kushindana kuendana na kasi ya vijana hao?

Ni dhahiri vilabu hivi viwili vinawakilisha taswira ya Ligi Kuu Italia. Timu nyingine kama Napoli ilimmsajili Kevin De Bruyne ambaye alimaliza muda wake katika klabu ya Man City, huku A C Milan hao walimchukua Kyle Walker katika dirisha lililopita la usajili. Hivyo basi unakutana na rundo la wachezaji ambao wamefuka miaka 30 na kushindwa kuendana na kasi ya wapinzani wenye umri mdogo. 

Katika nukta hiyo, Serie A inakuwa na idadi kubw aya wachezaji ambao wamemaliza muda wao kwenye Ligi zenye ushindani mkali na hivyo kana kwamba wanakimbilia  Italia kumaliza muda wao wa uchezaji wa soka.

Luka Modric mwenye miaka 40 hawezi kushindana na wachezaji vijana kama akina Martinelli, Myles, Joao Pedro, Madueke linapofika suala la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ni vigumu kuwaona wachezaji wazee wa Italia wakitoboa mbele ya wachezaji chipukizi na wenye uchu wa kutwaa makombe waliopo kwenye timu mbalimbali barani humo.

Si rahisi wachezaji wazee kutoa ubora wote unaohitajika kwa mashindano au mechi zenye presha kubwa lakini wanaweza kumudu kutuliza presha pekee. Katika hali ya kukabiliana na presha hiyo ndipo wanakutana na uhodari mpya wa wachezaji chipukizi na kuwa mwiba kwao. 

Ligi inapokaribisha wachezaji wenye umri mkubwa yaani waliovuka miaka 30 maana yake wanakwenda kuziba nafasi ya wachezaji vijana ambao wangeweza kutoa mchango mkubw aklabuni kuliko wazee ambao hucheza msimu mmoja kwa kiwango cha asilimia 45 huku zilizobaki ni muda wa kukaa benchi na kuingia kama mchezaji wa akiba. Ni sababu hii timu za Italia zinatandikwa katika mashindano kwa kuwa wachezaji wao hawawezi kuhimili shughuli ya wachezaji vijana.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Marti Cifuentes analeta nini Leicester City?

Tanzania Sports

CHAN jukwaa la vipaji vipya Ligi Kuu