in , , , ,

Mancini bosi mpya Milan

*De Gea, Fabregas waumia

Kocha wa zamani wa Manchester City na Galatasaray, Roberto Mancini amerejea Italia tayari kuanza kuwasuka Inter Milan kwa kipindi cha pili.

Mancini (49) aliyekuwa hana kazi tangu aachane na Galatasaray Juni mwaka huu, anachukua nafasi ya Walter Mazzarri aliyefukuzwa kazi majuzi. Mancini alitwaa ubingwa wa Italia mara tatu mfululizo kati ya 2004-2008 alipochukua nafasi ya kocha wa Chelsea, Jose Mourinho.

Rais wa Milan, Erick Thohir akimzungumzia Mancini ambaye alipohamia England aliwafundisha Man City na kuwapa ubingwa 2012, alisema kwamba rekodi yake ndani ya Milan na kwingineko inajieleza yenyewe wala hakuna shaka juu ya uwezo na ufanisi wake.

“Uzoefu wake wa kimataifa na kiu ya mafanikio utatuvusha Milan katika hatua nyingine kubwa ya mafanikio,” akasema rais huyo.

Mancini ametwaa jumla ya mataji makubwa 10 katika klabu tano tofauti alizofundisha, ambapo licha ya ubingwa wan chi amepata kuwaongoza Milan kutwaa Kombe la Ligi.

 Licha ya mafanikio yake, Mancini alifutwa kazi na vigogo hawa wa Italia kutokana na maoni aliyotoa baada ya kufungwa na Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, kasha akatangaza mara moja kwamba angeachana na klabu hiyo.
 
DE GEA, FABREGAS WAUMIA HISPANIA
image

Golikipa wa Hispania, David de Gea anayechezea Manchester United ameteguka kidole cha mkono kwenye mazoezi ya timu hiyo, ikiwa ni muda mfupi baada ya Cesc Fabregas kuumia misuli ya paja.

De Gea ameumia kidole cha mwisho cha kulia na atakosa mechi ya kufuzu michuano ya Euro 2016 baina ya Hispania na Belarus leo jijini Hueva. Atafanyiwa uchunguzi na madaktari kabla ya uamuzi kutolew, lakini atabaki kikosini.

United wanachuana na Arsenal kwenye mechi ya Ligi Kuu England wikiendi ijayo na kipa huyo ni tegemeo muhimu, kwani amekuwa akiwaokoa kutokana na matatizo ya ngome waliyo nayo vijana wa Louis van Gaal. De Gea alipata kuumia katika eneo hilo tena siku zilizopita.

Fabregas naye hatacheza kwenye mechi hiyo ambapo licha ya vipimo kuonesha hajaumia sana, mwenyewe anasema hajihisi vyema. Baada ya uchunguzi itaamuliwa iwapo abaki kikosini au arejeshwe klabuni kwake London.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Guinea wenyeji AFCON 2015

Caf, Guinea na siasa za AFCON