in , , ,

Man City, Newcastle, Norwich washinda

Crystal Palace wawakandamiza Sunderland

 

Mzunguko wa tatu wa Ligi Kuu ya England umeendelea kutoa matokeo ya aina yake, ambapo Manuel Pellegrini walau ametoka akipumua vyema.

Manchester City hatimaye walifanikiwa kuwafunga Hull City, lakini aina ya soka waliyoonesha vijana hao wa Pellegrini haikuvutia wala kutia moyo kuhusu hatima yao.

Ilibidi Manchester wasubiri hadi baada ya saa nzima kupata mabao waliyoyahitaji sana kuweka hali yao kuwa ya kawaida, ambapo mabao yalipitia kwa Alvaro Negredo na Yaya Toure.
Hull walicheza vyema, hasa katika kipindi cha kwanza na walipata nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia hivyo wamebaki na pointi tatu baada ya kucheza mechi tatu pia, wakiwa katika nafasi ya 17 wakati Manchester City wakiwa nafasi ya pili kwa pointi sita kutokana na mechi tatu.

Katika mechi nyingine, Everton wameambulia pointi moja kwa tabu walipocheza na Cardiff waliopanda daraja msimu huu. Everton wanaofundishwa na Roberto Martinez bado wanatafuta ushindi wa kwanza tangu kuanza kwa ligi hii.

Kwa matokeo hayo, Everton wanapokwenda kwenye mapumziko ya mechi za kimataifa wanabaki katika nafasi ya 15 wakiwa na pointi tatu baada ya mechi tatu huku Cardiff wakishika nafasi ya 10.

Newcastle walipata mwanga mpya, kutokana na bao la Hatem Ben Arfa katika dakika za mwisho dhidi ya Fulham, wakiwa wamemaliza balaa la kutoka bila bao katika mechi nne za nyumbani tangu msimu uliopita.

Mchezaji anayetarajia kujiunga na Arsenal, Yohan Cabaye na Loic Remy waliingia na kuongeza kasi ya Newcastle na Papiss Cisse alikosa bao kwa mpira wake wa kichwa kugonga mtambaa wa panya.

Nusura Adel Taarabt wa Fulham awarejeshee bao Fulham, lakini jitihada zake zilizuiwa na kipa wa Newcastle, Tim Krul. Kwa ujumla Fulham walishindwa kufanya mashambulizi hadi Ben Arfa alipowafungia Newcastle dakika nne kabla ya mechi kumalizika.

Kutokana na ushindi huo, Newcastle wanashika nafasi ya 11 wakati Fulham wapo ya 16.
Katika mchezo mwingine, Norwich walipata tulizo baada ya kuwafunga Southampton bao 1-0 katika mechi waliyokuwa nyumbani Carrow Road.

Alikuwa mchezaji kinda, Nathan Redmond (19) aliyewasafishia njia Norwich kwa kufunga bao lake la kwanza la Ligi Kuu baada kuchomoka kutoka wingi ya kulia na kupiga shuti la chini lililomshinda kipa Artur Boruc kutoka umbali wa yadi 20.

Kocha wa Norwich, Chris Hughton, ambaye ndiye kocha pekee mweusi katika EPL, alionekana kuwa na furaha kubwa kwa ushindi huo aliosema ni muhimu, kwani licha ya kufanya usajili mzuri na wa ghali msimu huu, alianza vibaya.

Maana ya matokeo hayo ni kwamba Norwich wanakamata nafasi ya nane huku Southampton wanaofundishwa na Mauricio Pochettino wakiwa nafasi ya tisa.

Mechi nyingine iliyoshuhudia matokeo ya kustaajabisha ni ya Crystal Palace wanaofundishwa na Ian Holloway waliocheza nyumbani kwao kuwafunga Sunderland wa Paolo Di Canio mabao 3-1.

Sunderland wamekaa nafasi ya pili kutoka mkiani wakati Palace wakiwa nafasi ya 14. Jumapili hii inasubiriwa mechi ya watani wa jadi wa Uingereza – Manchester United dhidi ya Liverpool na mahasimu wa London kaskazini, Arsenal na Tottenham Hotspur.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Bayern wawapiga Chelsea Super Cup

USAILI WAGOMBEA TFF, BODI YA LIGI