in ,

Mali wakomalia ushindi wa tatu

*Wawazidi nguvu Ghana kwa 3-1

 

Mali imenyakua nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya pili mfululizo.

Wakicheza kwa kasi na kujiamini, kwenye mvua katika uwanja mzuri wa Port Elizabeth, Mali waliwachakaza Ghana waliokuwa wakipewa nafasi kushinda, kwa jumla ya mabao 3-1.

Mahamadou Samassa aliwatanguliza Tai wa Mali mbele dakika ya 21 kwa kichwa safi, bao lililodumu hadi kumalizika nusu ya kwanza ya mchezo.

Walikuwa ni Mali walioanza tena vyema kipindi cha pili, ambapo dakika tatu tu zilimtosha nahodha Seydou Keita kufunga bao la pili, akijaza mpira wavuni kutoka karibu na goli.

Kiungo wa Ghana, Kwadwo Asamoah alirejesha matumaini ya Black Stars kwa kumtungua kiufundi golikipa Soumbeyla Diakite katika dakika ya 82 na kurejesha wasiwasi wa mechi kuingia dakika za ziada au hata penati.

Hata hivyo, mchezaji aliyeingia dakika ya 78, Sigamary Diarra aliwainua vitini washabiki wa Mali kwa kupachika bao katika dakika za majeruhi.

Ghana walipoteza nafasi nzuri ya kufunga, pale Mubarak Wakaso aliyekuwa mmoja wa wafungaji wazuri, kupaisha penati juu ya lango.

Timu mbili hizi zilikuwa zikikutana kwa mwaka wa pili mfululizo na mara ya nne katika mashindano mawili yaliyopita, kwani zilikutana pia kwenye hatua za makundi.

Ghana walionekana kuwa na uhai mpira ulipoanza, kwa beki Richard Kissi Boateng kuwavuta Wamali kwenye eneo lao, lakini alishindwa kumfikishia mpira mpachika mabao, Asamoah Gyan.

Alikuwa tena Gyan aliyezawadiwa mpira wa kufunga na beki wa Mali, Adama Coulibaly katika eneo la hatari, lakini alipaisha mpira juu na kubaki akijilaumu.

Jumapili hii ni fainali, ambapo Burkina Faso wataoneshana kazi na Nigeria katika uwanja wa FNB Soccer City jijini Johannesburg.

Katika mechi hiyo ya mwisho, ambapo mfalme wa soka Afrika atapatikana, mchezaji mahiri wa Burkina Faso, Jonathan Pitroipa aliyeoneshwa kadi nyekundu kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Ghana, anacheza.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limemfutia kadi hiyo aliyooneshwa na mwamuzi Slim Jdidi kwa madai alijirusha kwenye eneo la penati. Tayari mwamuzi huyo amekiri alikosea na ameondoshwa kuchezesha.

 

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Gharika Manchester City

AFRICAN REFEREES LET DOWN AFRICAN SOCCER