in

Makocha watajwa kumrithi Zidane

ZZ

MSIMU wa ligi kuu Hispania maarufu kama La Liga unaelekea ukingoni huku binga akiwa hajulikani hadi sasa kutokana na timu nne za Atletico Madrid,Barcelona na Sevilla zote kuwa na nafasi ya kuibuka vinara. Pamoja na mbio hizo kuwa gumzo kwa wadau wa soka, lakini yapo mambo mengine yanayoendelea na kugeuzwa kuwa mjadala mkubwa.

Mjadala mkubwa kwa sasa ni nafasi ya kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane ambaye tetesi za awalizilidai kuwa huenda akaachana na klabu hiyo. Zidane amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake, lakini sasa haonekani kuwa atabaki klabuni hapo huku mwenyewe akikoleza moto zaidi kuwa unapowadia wakati wa kuondoka ni muhimu kufanya hivyo.

Uamuzi wa kumkabidhi timu utakuwa mikononi mwa rais Florentino Perez na bodi yake chini ya ukurugenzi wa Angel Sanchez. 

Wakati hayo yakiendelea, habari zingine zinadai kuwa Zidane anawindwa na timu tatu zikiwa na sababu mbalimbali za kuhitaji makocha wapya. Kwanza, PSG inatajwa kuwinda huduma ya Zidane baada ya jaribio lao la pili kufeli kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na kutolewa hatua ya nusu fainali na Manchester City.

Pili, klabu ya Juventus imedaiwa kutaka huduma ya Zinedine Zidane ili kuponya msimu mbaya waliokutana nao wakiwa chini ya Andre Pirlo. Zidane hajawahi kukanusha juu ya kuvutiwa kuwa kocha wa Juventus, na amewahi kusema kuwa ni klabu anayoamini atafundisha siku moja. 

Tatu, klabu ya Manchester City nayo imehusishwa na kumwajiri Zidane kwa kile kinachoitwa huenda Pep Guardiola akarejea katika klabu ya nyumbani kwao Barccelona. 

Sababu mbili za kumwondoa Pep Guardiola ni endapo atashindwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea na hatua ya kuchaguliwa rais mpya wa Barcelona Joan Laporta ambaye wamewahi kufanya kazi pamoja miaka ya nyuma kwa mafanikio makubwa. Inaelezwa Pep huenda akaungana na Laporta hivyo kuchukua nafasi ya Ronald Koeman.

Hata hivyo nafasi ya ukocha wa Real Madrid imekuwa gumzo kwa sasa, huku majina mbalimbali yakitajwa kuwa vinara, yakiongozwa na watatu ambao duru za habari zinasema wapo kwenye kufanyiwa tathmini ikiwa wapewe nafasi au la. 

RAUL GONZALEZ

Tanzania Sports
RAUL GONZALEZ

Anapigiwa mbiu zaidi na vyombo vya vya habari vya Hispania. Kwanza kwa sababu ni raia wa Hispania, ni mtoto wao. Pili ni mchezaji wa zamani wa Real Madrid ambaye amecheza kwa mafanikio akiwa na Zidane. Katika muundo wa ukocha kwenye klabu ya Real Madrid, Raul amekuwa kocha wa Real Madrid Castilla tangu mwaka 2019, nan i mmoja wa wapishi wa vipaji na mafanikio ya timu kama ilivyokuwa kwa Zidane.

Raul Gonzalez akiwa kocha wa Castilla anawindwa na klabu mbili za Bundesliga za Eitratch Frankfurt na Schalke O4 za Ujerumani. Alianza kazi ya ukocha kwa kufundisha klabu ya A Sadd, lakini mwaka 2019 aliajiriwa kuwa kocha wa kikosi cha pili cha Real Madrid Castilla. 

Ametwaa taji la uefa kwa vijana msimu uliopita. Raul anatajwa kwa kigezo kuwa hata Zidane alianza ukocha akiwa na kikosi cha Castilla. Hata hivyo wana tofautiana kwani Zidane alikuwa kocha msaidizi kipindi cha Carlo Ancelotti ambako mwaka 2014 walitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa Raul ndio kwanza anaanza safari na hajawahi kuwaongoza mastaa wakubwa wa timu. 

Hana uzoefu mkubwa lakini anatajwa kuwa na sifa za kuajiriwa, ingawa uamuzi uko mikononi mwa  rais Florentino Perez na Angel Sanchez pamoja na bodi ya klabu hiyo

MAXIMILLIANO ALLEGRI 

Tanzania Sports
MAXIMILLIANO ALLEGRI 

Amekaa nje ya ukocha kwa miaka kadhaa sasa tangu alipong;atuka Juventus. Allegri alikuwa kocha mwenye mafanikio akiwa Juventus. Kwa misimu kadhaa amehusishwa na kazi za ukocha katika klabu za PSG,Chelsea,Man Cit,Barcelona na hata Real Madrid hapo awali. Allgeri amepata mafanikio ya ukocha katika Ligi Kuu Italia na aliachana na Juventus akiwa ameipata mataji kadhaa. Ana uzoefu wa kuwaongoza mastaa  wakubwa katika klabu na wachezaji wa kimataifa. 

Timu alizowahi kufundisha ni Aglianese(2003-2004),SPAL(2004-2005),Grosselo(2005-2006),Sassuolo(2007-2009),Cagliari(2008-2010),AC Milan(2010-2014) na Juventus (2014-2019). Wakati wakiwa mchezaji alicheza nafasi ya kiungo.

Uamuzi wa kumkabidhi timu utakuwa mikononi mwa rais Florentino Perez na bodi yake chini ya ukurugenzi wa Angel Sanchez. 

JOACHIM LOW

Tanzania Sports
JOACHIM LOW

Ni kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani tangu mwaka 2004-2006. Kocha huyo awali alikuwa msaidizi wa Jurgen Klinsmann wakati fainali za Kombe la dunia mwaka 2006 ambako Ujerumani walikuwa wenyeji na walitolewa katika hatua ya nusu fainali.

Baada ya fainali za Kombe la dunia  mwaka 2006 Joachim Low alipokea majukumu ya kukinoa kikosi cha Ujerumani. Mwaka 2014 alitwaa ubingwa Kombe la Dunia baada ya kuizaba Argentina katika mchezo wa fainali bao lake likifungwa na Mario Goetze. Pia ametwaa taji la Kombe la Mabara mwaka 2017 nchini Urusi.

Mnamo Machi 9 mwaka 2021 alitangaza kuwa hataendelea kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani. Kwa sasa ana umri wa miaka 61, ni mzee.

Timu alizowahi kufundisha ni FC Frauentfeld(1994-1995),VFB Stuttgat(1996-1998),Fenerbahce(1998-1999),Karlsruher SC(1999-200),Adanaspor(2000-2001), FCTirol Innsbruck(2001-2002),Austria Wien(2003-2004

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Hekaheka

Simba walizidiwa lakini watafanya maajabu..

SIMBA SC

‘Simba ni bingwa Ligi Kuu Bara’