in

Mabeki wanaoweza kumrithi Sergio Ramos Real Madrid

JULES KOUNDE

Mwezi Desemba unaelekea ukingoni na kupisha Januari ya mwaka mpya wa 2021. Ifikapo mwezi Januari Sergio Ramos atakuwa amebakiza miezi sita katika mkataba wake wa kucheza Real Madrid. Miezi hiyo inampa mamlaka ya kuzungumza na timu zingine ambazo zitakuwa tayari kumsajili. Hadi sasa hakuna taarifa yoyote kutoka kwa pande zote mbili;uongozi wa Real Madrid na Sergio Ramos licha ya matumaini kuwa huenda akapewa mkataba mpya, ambao utakuwa tofauti na sera ya klabu.

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane mara kadhaa amebainisha kuwa na matumaini nahodha huyo ataongeza mkataba na kustaafu soka akiwa Real Madrid. Maoni yake hadi sasa hayajathibitishwa kwa vitendo kutangaza mkataba mpya wa Ramos au kuondoka klabuni.

Tanzania Sports
Sergio Ramos

Ikiwa hataongeza mkataba maana yake mwishoni mwa msimu huu Ramos hatakuwa mchezaji wa Real Madrid hivyo ataruhusiwa kuondoka bure au FlorentinoPrez aamue kumuuza dirisha dogo la usajili ili kupata fedha.

Ramos ni nguzo ya mafanikio ya Real Madrid kwa kipindi cha miaka 15 aliyokaa klabuni hapo, ambapo sasa ana umri wa miaka 34. Utaratibu wa Real Madrid kwa wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 30 ni kuwaongezea mkataba wa mwaka mmoja, jambo ambalo ni kibarua kigumu kwa Perez, ikiwemo kuongeza mkataba wa Luka Modric mwenye umri wa miaka 35.  

Endapo nahodha huyo ataondoka Real Madrid, mabeki wafuatao wanaweza kurithi mikoba yake.

PAUL TORRES

Ni beki wa Villareal amekuwa nguzo ya klabu hiyo ya La Liga na kuitwa timu ya Taifa ya Hispania ambako amecheza mechi mbili za Nation League sambamba Sergio Ramos katika nafasi ya beki wa kati, hivyo anafikiriwa kuwa mmoja wa wanaoweza kurithi mikoba yake. Torres ana miaka 23 amethibitisha kuwa beki hodari kati ya wengi wa La Liga. Nyota huyu anatumia mguu wa kushoto hatakuwa tatizo kuchukua nafasi ya Ramos.

“Ramos ni nahodha anayerahisisha maisha ya kambini na uwanjani kwa timu ya taifa. Ni mchezaji wa aina yake ambaye ananifanya nijione nacheza kama yeye,” amewahi kusema Paul Torres mwanzoni mwa mwezi Novemba.

Paul Torres alisaini mkataba mpya Villareal mwaka 2019 utakaomweka klabuni hapo hadi mwaka 2024. Ada ya kuvunja mkataba wake ni Euro milioni 50, pia inaweza kufika hadi Euro Milioni 65 siku za mwisho za kumalizika dirisha usajili.

DAVID ALABA

Ni beki mwingine wa kati anayetumia mguu wa kushoto. Alaba anaweza kujiunga na Real Madrid kabla ya Ramos hajaondoka klabuni hapo. Mkataba wa nyota huyo wa Austria katika klabu yake ya Bayern Munich unatarajiwa kumalizika mwishoni m  amsimu huu, huku Real Madrid wakiwa miongoni mwa timu zinazomtolea jicho kumsajili.

Kwa asili David Alaba mwenye umri wa miaka 28 ni beki wa kushoto ambaye amebadilishwa nafasi hadi kucheza beki wa kati chini ya kocha Hansi Flick, akiwa amefanikiwa kutwaa taji la pili la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita 2019/2020. Alaba ni beki mwenye nguvu na kasi, anashambulia na kurudi nyuma haraka hivyo anaweza kuwa nguzo katika kikosi cha Zinedine Zidane iwe anajiunga mwezi januari au mwishoni mwa msimu huu.anafaa pia kumrithi Ramos.

JULES KOUNDE

JULES KOUNDE
JULES KOUNDE

Real Madrid walimsajili Sergio Ramos mwaka 2005 kutoka Sevilla, inawezekana tena wakarejea katika klabu hiyo kumsajili Jules Kounde kuwa beki wao wa kati. Kounde alihusishwa kujiunga na Manchesster City mwanzoni mwa msimu lakini mpango huo haukutimia. Sera ya Sevilla ni kusajili wachezaji kwa bei nafuu na kuwauza kwa bei ghali.

Wakati Man City walipobisha hodi Sevilla ili kumsajili Kounde, Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Monchi alisema ada ya kuvunja mkataba wa beki huyo ni Euro milioni 90. Kwahiyo bei ya nyota huyo mwenye miaka 22 kumtoa Sevilla kwenda Real Madrid huenda ikawa ya juu zaidi na kuwapa mtihani Los Blancos ikizingatiwa Kounde ana makataba hadi mwaka 2024.

EDER MILITAO

Tanzania Sports
EDER MILITAO

Real Madrid walitumia kiasi cha Euro milioni 50 kumsajili beki huyu kutoka Porto ya Ureno mwaka 2019 walijua atakuwa tegemeo miaka ijayo. Militao ana miaka 22, lakini bado hajafanikiwa kuonesha kama anaweza kuvaa viatu vya Sergio Ramos au Raphael Varane ambao ni chaguo la kwanza la kocha Zinedine Zidane.

Militao anapocheza na Varane anaonekana kuvurunda zaidi, jambo ambalo linawatia hofu Los Blancos na kushusha matumaini yao ya kumwona akibeba majukumu ya nahodha wao Ramos kama mpango wao wa kumsajili ulivyokuwa. Msimu huu Zidane amebadili mbinu kwa kumtumia Nacho Hernandez katika mechi ambazo Sergio Ramos amekuwa anatumikia adhabu au kuwa majeruhi. Nacho anaelekea kucheza vizuri anapokuwa na Varane kuliko Militao na Varane.

Kwa msingi huo mategemeo ya Militao kumrithi Ramos yatategemeana na uamuzi wa Real Madrid wenyewe kuona iwapo wataendelea kumwimarisha ili awe bora zaidi au watanunua beki mwingine. Militao ana miaka 22 ambayo ni kigezo kikubwa cha kuendelea kujifunza na kuimarishwa. Kwahiyo wanaweza kumpa nafasi ili ajiimarishe kabla ya kutamba kikosini hapo.

Nafasi ya kuimarika pia itategemea mwitiko wa Militao mwenyewe, ikiaminika vipaji vya Kibrazil huwa havina mashaka. Lakini Militao anafaa kufikiriwa kuwa miongoni mwa warithi wa Ramos, kwani tayari amekaa msimu mmoja kujifunza na kuelewa mazingira na uzoefu ameshapata.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Arsenal

Mikel Arteta, awaamini chipukizi wa Arsenal…

The FA

BREXIT: Soka na maisha mapya