in , , , ,

Liverpool kicheko, Arsenal maumivu

*Real Madrid karamu ya mabao

Liverpool wamepata ushindi wa tabu kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) baada ya kuikosa kwa miaka mitano, huku Arsenal wakianza kwa kufungwa 2-0 ugenini nchini Ujerumani.

Nahodha wa  Liverpool, Steven Gerrard aliwafungia bao la ushindi dakika za majeruhi, kwani walikuwa wametoshana na mabingwa wa Bulgaria, Ludogorets Razgrad kwa bao 1-1.

Wakicheza nyumbani Anfield, Liverpool walitarajiwa kuwa na mchezo rahisi, lakini walibanwa vilivyo hadi dakika ya 82 mshambuliaji wao mpya, Mario Balotelli alipofanikiwa kuwazidi maarifa walinzi wawili na kutia bao kimiani.

Hata hivyo, dakika ya 90 mchezaji aliyetokea benchi, Dani Abalo alimzunguka kipa wa Liverpool, Simon Mignolet na kutikisa nyavu. Kosa la kipa mahiri wa wageni, Milan Borjan kumchezea rafuJavier Manquillo liliwapa Liverpool penati iliyowapatia pointi tatu muhimu.
 
ARSENAL WALALA UJERUMANI
dortmunds

Kama ilivyotarajiwa, Arsenal walioondoka London kwenda Ujerumani na hofu kutokana na majeruhi kwenye safu yao ya ulinzi, waliambulia kipigo cha bao 2-0 mikononi mwa Borussia Dortmund waliotupia bao moja kila kipindi.

Ciro Immobile alifunga baada ya kumzidi nguvu beki wa kati, Laurent Koscielny na kumtungua kipa Wojciech Szczesny kwa mpira wa chini chini katika dakika ya 45 wakati Pierre-Emerick Aubameyang alifunga la pili dakika ya 48.

Aubameyang pia aligonga mwamba kwa mpira mwingine, huku mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck akipoteza nafasi moja baada ya kuwa katika nafasi nzuri kabisa ya kufunga.

Arsenal wanawakosa beki wa kulia, Mathieu Debuchy atakayekuwa nje kwa kati ya wiki nane na 12, beki wa kushoto, Nacho Monreal anayetarajia kurejea karibuni, Calum Chambers mwenye homa na pia baada ya kumuuza beki wa kati, Thomas Vermaelen hawajafidia nafasi hiyo.

Arsenal walimchezesha beki Hector Bellerin (19) ambaye mechi pekee ya kiushindani alicheza dakika 26 katika mashindano madogo ya Kombe la Ligi. Hata hivyo, Arsenal walitawala mechi hiyo kwa asilimia 56 lakini wakapiga mashuti manne tu golini huku wenzao wakipiga 22.
 
MATOKEO MENGINE YA UCL

Katika mechi nyingine Jumanne hii, Real Madrid waliwakausha FC Basel 5-1, Juventus wakawafunga Malmo FF 2-0, Olympiakos wakawapiga Atletico Madrid 3-2, Benfica wakazidiwa nguvu 0-2 na Zenit St Petersburg, Monaco wakang’ara 1-0 kwa Bayer Leverkusen na Galatasaray na Anderlecht wakatoshana nguvu 1-1.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal hofu kwa Dortmund

Lucas Moura amevurugwa Brazil, PSG