in , , , ,

Arsenal hofu kwa Dortmund

*Vigogo uwanjani mechi za UCL

Hatua za makundi za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) inaanza huku Arsenal wakiwa nyumbani kwa Borussia Dortmund na shaka ya safu yake ya beki.

Masahibu yanayowaandama Arsenal zaidi ni kuumia kwa beki wake wa kulia, Mathieu Debuchy na wa kushoto, Nacho Monrteal, huku mwenzake wa kushoto Kieran Gibbs akiwa fiti lakini ana kawaida ya kuumia mara kwa mara.

Kana kwamba hiyo haitoshi, beki mpya na chipukizi, Calum Chambers hana uhakika wa kucheza kutokana na kuwa ameumia lakini matabibu walikuwa wakiangalia iwapo ataweza kuingia dimbani.

Kocha Arsene Wenger alisema Chambers ana asilimia 50 kwa 50 ya kucheza au kutocheza na iwapo atashindwa, basi Mhispania, Hector Bellerin (19) sawa na Chambers atabeba jukumu hilo, licha ya kwamba amecheza mechi moja tu katika kikosi cha wakubwa Arsenal.

Wenger alimwelezea Bellerin kuwa ni mpambanaji, mwenye haiba na asiyetishwa kwa namna yoyote na shinikizo la mechi kubwa, akisema ni kiwango kizuri sana, hasa kwa vijana kama yeye, akisema ana kasi na anajua kuusoma vyema mchezo.

Hata hivyo, Arsenal wanatakiwa kuchukua hatua juu ya beki yao, ikiwa ni pamoja na kuongeza mchezaji kwenye beki ya kati, kwani tangu walipomuuza nahodha wao, Thomas Vermaelen kwa Barcelona kiangazi hiki, hawajaingiza mchezaji mpya, na wanaweza kujilaumu baadaye mambo yakiwa mabaya.

Wanachoweza kufanya sasa ni kusajili wachezaji huru, ambao wapo kadhaa sokoni, na walidaiwa walitaka kumsajili Mario Yepes lakini pia Joseph Yobo yupo, sawa na wengine kadhaa. Wenger amepata kukana kuwa na tatizo kwenye safu yake ya ulinzi.

Katika mechi nyingine za UCL Jumanne hii, Liverpool wanawakaribisha Ludo Razgd, Real Madrid ni wenyeji wa FC Base, wakati Atletico Madrid wamesafiri kukabiliana na Olympiakos.

Juventus wanacheza na Malmo FF, Benfika wanawakaribisha Zenit St Petersburg, Monaco wenyeji wa Bayern Leverkusen na Galatasaray watapepetana nyumbani kwao na Anderlecht.

Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema atauchukulia mchezo wa leo kwa umuhimu kana kwamba wanacheza na Real Madrid.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Jerome Champagne kumvaa Blatter

Liverpool kicheko, Arsenal maumivu