in , , ,

Ligi Kuu inahitaji washambuliaji kama Mayele

WAKATI timu zikiwa zinafanya juhudi za usajili wa wachezaji wapya, lipo jambo moja ambalo linatafakarisha sana. si ajabu kutafakari jambo kwa sababu bado safu za washambuliaji wa timu za Ligi Kuu zimeshindwa kufikia rekodi nyingi za Fiston Mayele aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Yanga. Ligi kuu Tanzania imekuwa na washambuliaji wengi ambao wametoka nchi mbalimbali, lakini hawajafanikiwa kujiandikia rekodi za kipekee. 

Klabu za Simba, Yanga na Azam zilishiriki mashindano ya Kimataifa lakini washambuliaji wao hawakufua dafu mbele ya mabeki wa timu pinzani. Kwa mfano eneo la mashindano ya Kimataifa ya CAF, washambuliaji wa vilabu vyetu walifanya juhudi kubwa kutaka kuibuka na ushindi, na hata timu ziliposhinda bado wafumania nyavu hawa hawakuleta matokeo makubwa. 

Yanga wanaye Prince Dube, na Simba wanaye Lionel Ateba na Stephen Mukwala, lakini bado nyota hawa hawakufua dafu kimataifa. Kwa upande wa washambuliaji wazawa hali ya mambo ilikuwa ileile, Clement Mzize ndiye aliyeonekana kuwa kinara wa kusaka mabao ndani nan je. Mzize akiwa na klabu ya Yanga hakufua dafu kimataifa kwa maana ya kufunga mabao mengi lakini angalau alionesha juhudi. 

Kiufupi timu zetu zinaposhiriki mashindano ya CAF tunatarajia kuona nyota hao wakipiga hatua zaidi katika upachikaji wa mabao. Yanga walikuwa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa ambako walitupwa nje katika hatua ya makundi hivyo kushindwa kuchachafya zaidi. 

Yote hayo yalitokana na makosa ya uongozi wa Yanga wenyewe na kocha wao Sead Ramovic ambaye hakuwa na ujuzi wa kutosha kuongoza klabu kigogo kama Yanga. Hali kadhalika Simba walikuwa chini yakocha Fadlu Davids lakini washambuliaji wake wawili wa kimataifa Stephen Mukwala na Lionel Ateba hawakuweza kufikia rekodi ya Fiston Mayele.

Mojawapo ya kibarua ambacho washambuliaji toka nje wanacho ni kuwa na uwezo wa kufunga mabao mengi kwa msimu. Ukiangalia washambuliaji wa nje waliopo sasa hakuna yeyote aliyefikisha idadi ya mabao 20 katika mashindano yote sembuse Ligi Kuu. Katika Ligi Kuu hakuna mshambuliaji mwenye mabao 15 ikiwa na maana hakuna aliyevunja rekodi ya Boniface Ambani wala Mohammed Hussein. Hivyo basi washambuliaji waliopo sasa wana kibarua kigumu cha kuhakikisha wanapachika mabao ya kutosha na kuweka rekodi katika mashindano yote wanayoshiriki na klabu zao. 

Fiston Mayele alikuwa mshambuliaji namba moja wa Yanga. Mayele ndiye mfalme wa soka la Tanzania kwa upande wa washambuliaji. Mayele alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania, akawa mfungaji bora wa mashindano ya CAF na kuweka rekodi kuwa nyota kutoka Tanzania aliyetamba kwenye mashindano hayo. 

Si vibaya kukiri kuwa kama kuna mchezaji ambaye amekuja kuleta sifa nzuri nje ya Tanzania na ambaye amecheza Ligi Kuu basi Fiston Mayele ni namba moja. Baada ya kuondoka Yanga alisajiliwa na klabu ya Pyramids ya Misri. Kana kwamba haitoshi akiwa kwenye kikosi cha Pyramids alifanikiwa kuipa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika klabu hiyo ikiwa ni mara yao ya kwanza. 

Pia ilikuwa mara ya pili kwa Mayele kucheza fainali ya mashindano ya CAF, akitokea kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho ambako alifungwa na USMA Alger kwa tofauti ya bao moja. Katika Ligi Kuu Tanzania Fiston Mayele alikuwa akifunga mabao mara kwa mara, hali ambayo washindani wake walimkosoa na kudai ni mshambuliaji wa kawaida. Lakini Mayele alipiga hatua zaidi kuwa mmoja washambuliaji hatari katika mashindano ya CAF na akaibuka kuwa mfungaji bora.

Hii ina maana washambuliaji wanaosajiliwa Tanzania wana kila sababu ya kumwona Fiston Mayele kama alama yao ya soka. Kiwango alichokiweka Fiston Mayele ndicho kinachotumiwa na kuwapima washambuliaji wengi wa nje wanaosajiliwa na timu za Ligi Kuu. Kama mshambuliaji wan je ameshindwa kupachika mabao 20 kwa msimu, na kwa mashindano yote maana yake kzi yake ipo chini ya ufanisi. Ili mshambuliaji wan je anayecheza Ligi kuu Tanzania aonekane kuwa mahiri lazima avunje rekodi zote za Fiston Mayele. 

Hata hivyo washambuliaji wanaosajiliwa bado hawajaonesha sababu za kusajiliwa kwao kama ilivyokuwa kwa Fiston Mayele. Ni dhahiri kuwa klabu za Yanga, Simba na Azam pamoja na Singida Black Stars zinatamani kuwa na nyota kama Fiston Mayele. Lakini hali ya mambo imekuwa tofauti hadi sasa. 

Unapokuwa na washambuliaji wakali katika timu yako, wanatakiwa kuvuka mipaka ya ushindani na kutetemesha timu za nje, na hivyo kujiweka katika nafasi ya kuwauza kwa fedha nyingi. Clement Mzize ni nyota mzawa ambaye anapambana na washambuliaji wa kigeni. 

Hilo lina maana mshambuliaji kutoka nje ya nchi anatakiwa kupambana vilivyo ili aweze kuchukua nafasi yake ama aweze kuitafuta rekodi ya Mayele. Angalau mshambuliaji wa kigeni awe na uwezo wa kufunga mabao 25 katika mashindano yote kwa msimu mmoja. Kinyume cha hapo klabu zetu zitakuwa zinaula wa chuya kwa kusajili wachezaji wasio na vigezo wala uwezo kwa sababu tu wameletwa na wananchama fulani fulani kwenye klabu.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Kocha Romain Folz

Kocha Romain Folz katika njia ya Ramovic

Ben McCarthy ataweza kuipaisha Harambee Stars?

Ben McCarthy ataweza kuipaisha Harambee Stars?