in , ,

Ben McCarthy ataweza kuipaisha Harambee Stars?

KENYA ni mwenyeji kwenye mashindano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani. Mashindano hayo ni maarufu kwa jina la CHAN. Kenya inashirikiana na Tanzania na Uganda katika kukamilisha mashindano ya CHAN. Wageni wanatarajiwa kupepetana kwenye dimba Moi Kasarani kwenye mmashindano haya. Hata hivyo umaarufu wa Kenya kwenye soka ulikuwa umedidimia kwa kiasi fulani, lakini jina la kocha wake limeifanya kuwa nchi ya kutupiwa jicho kwneye fainali hizi. TANZANIASPORTS inakuletea uchambuzi yakinifu kuhusiana naushiriki wa Kenya kwenye mashindano ya CHAN.

Ufunguzi wa CHAN

Mashindano ya CHAN yanatarajiwa kufunguliwa katika dimba la Benjamin Mkapa ambapo mwenyeji Tanzania atapepetana nan a Burkina Faso ya Stephane Aziz Ki. Baada ya mchezo wa kwanza kufungua pazia la CHAN jijini Dar Es Salaam. Mchezo wa fainali wa kufunga mashindano ya CHAN utafanyika nchini Kenya, ambapo Harambee Stars inapewa changamoto ya kuwa moja ya timu ya kutinga mchezo w afainali. Mechi za makundi mengine zitafanyika katika nchi zote tatu, Tanzania, Kenya na Uganda. Na mashindano haya yatatumika pia kuzipima nchi hizo katika uwezo wao wa kuandaa mashindano makubwa ya AFCON.

Umaarufu wa kocha wao

Ben McCarthy ni nyota wa zamani wa vilabu vikubwa kama vile FC Porto, mahali ambapo alifanya makubwa kwa kutwaa Taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa chini ya kocha Jose Mourinho. Moja ya matukio ya kukumbukwa ya Ben McCarthy ni hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2004 ambapo Porto ilicheza dhidi ya Manchester United ya Alex Ferguson. 

Ben alikuwa shabiki wa Man United, lakini siku ya mchezo alilazimika kufanya kazi ya ziada kuhakikisha anaifunga timu hiyo ili kwenda fainali. Ndivyo ilivyotokea, Man United walitupwa nje ya mashindano. Ben MacCathy ni jina kubwa katika soka Afrika. Akiwa kwenye jezi za timu ya Taifa ya Afrika kusini alitetemesha kwenye mashindano ya AFCON ambako amekuwa mmoja wafungaji bora kwenye fainali zilizofanyika Burkina Faso. Si hilo tu, Ben ni miongoni mwa magwiji wa soka barani Afrika, pamoja na Ulaya ambako amepita vilabu mbalimbali. Kwahiyo ni kocha maarufu kwa Kenya.

Nafasi ya kwanza ukocha

Ben hakuwahi kufundisha timu ya Taifa katika historia yake ya ukocha. Alianza kazi ya ukocha huko kwao katika ngazi ya klabu, kabla ya kuajiriwa kuwa kocha wa washambuliaji wa klabu ya Manchester United. Katika nafasi ya ukocha Ben anatakiwa kuipa ushindi Kenya ili kusalia katika kibarua chake. Kenya inajiweka mguu sawa kwenye mashindano ya CHAN ili kuelekea fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027. Kwenye fainali za AFCON mwaka 2027 Kenya itakuwa mwenyeji kwa ushirikiano na Tanzania na Uganda. Kwa maana hiyo Kenya kama mwenyeji anatazamwa nini anachotarajiwa kukifanya katika mashindano haya. Wakati huu ikiwa kwenye kinyang’anyiro cha CHAN, Kenya inataka kuonesha kuwa inaweza kurudia ukali wake katika soka la Kimataifa kama walivyofanya miaka 1990. Hii ni nafasi muhimu ya kocha Ben kuipaisha Harambee Stars.

Kujitoa ‘Four Nations’.

Tanzania Sports
Ben McCarthy ataweza kuipaisha Harambee Stars?

Kabla ya kunguruma mashindano ya CHAN hapo Agosti 2 mwaka huu, kulikuwa na mengine ya ‘CECAFA Four Nations’ katika uwanja wa Black Rhino Academy huko Karatu. Kwenye mashindano hayo yaliandaliwa kama sehemu ya mazoezi kwa timu za Tanzania, Uganda, Senegal, na Kenya. Lakini Kenya ilitangaza kujitoa kwenye mashindano hayo na kuwaachia wengine. 

Benchi la ufundi la Harambee Stars lilitathmini mashindano hayo kwa mtazamo hasi huku wakiwa na hofu ya kupoteza wachezaji muhimu kuelekea mashindano ya CHAN. Mashindano ya ‘Four Nations’ yamefanyika wiki chache kabla ya kuanza rasmi mashindano ya CHAN, hali ambayo benchi la ufundi la Harambee Stars liliona haliwezi kuandaa timu vyema kuelekea CHAN. Hatua hiyo ya kujitoa imelelezewa kuwa njia ya kuandaa kisaikolojia wenyeji Kenya kushiriki vyema kwenye mashindano ya CHAN.

Taji la kwanza

Kenya haijawahi kunyakua taji lolote la AFCON au CHAN sawa na majirani zake Tanzania na Uganda. Katika mashindano haya Harambee Stars ina kibarua ya kujiandikia rekodi ya aina yake na kuwa Taifa la kwanza la Afrika mashariki kutwaa taji la CHAN. Lakini taji hilo litawezekana iwapo kocha Ben McCarthy atawaongoza vyema mastaa wake kuibuka vinara mbele ya Senegal, Tanzania, Burkina Faso na mataifa mengine. Je Ben McCarthy ataweza kuipaisha Harambee Stars? Hilo ni jambo la kusubiri na kuona kizazi kipya cha wachezaji wa kikenya wakiweka rekodi nzuri au mbaya. Ni jambo linalosubiriwa pia kwa mashabiki kuona namna kocha wao Ben anavyotumia maarifa aliyopata katika Ligi Kuu England maarufu kama PL kuwapa ubingwa na furaha kwa wakenya.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Ligi Kuu inahitaji washambuliaji kama Mayele

Taifa Stars

Je Hemed Morocco atavunja rekodi ya Maximo?