in

Kwanini Shikalo ni bora kuzidi Metacha ?

Shikalo

Juzi kulikuwa na mechi kati ya Namungo FC na Yanga, mechi ya michuano ya kombe la mapinduzi. Mechi hiyo ilimalizika kwa Yanga kushinda goli kwa bila , mfungaji pekee wa goli alikuwa Zawadi Mauya.

Kwenye mechi hiyo Yanga walimwanzisha golikipa Farouk Shikalo ambaye alichukua nafasi ya Metacha Mnata ambaye kwa msimu huu amekuwa golikipa chaguo la kwanza. Kwenye mechi hii Farouk Shikalo alionesha ubora ambao Metacha Mnata hana. Kwanini Farouk Shikalo ni bora kuzidi Metacha Mnata?

SWEEPER GOALKEEPER

Farouk Shikalo ni “sweeper goalkeeper”. Nini maana ya “sweeper goalkeeper?”. Sweeper goalkeeper ni aina ya walinda mlango ambao hupenda kukaa karibu na safu ya ulinzi.

Jukumu la kwanza la goalkeeper kuzuia mshambuliaji asifunge . Sweeper goalkeeper anapokuwa karibu na safu yake ya ulinzi anakuwa na nafasi kubwa ya kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma.

Dunia ya sasa inahitaji wachezaji wa kisasa kuendana na mifumo ya kisasa. “Sweeper goalkeeper” ni  mlinda mlango wa kisasa anayeendana na mahitaji ya mpira wa kisasa. Kwa hiyo Farouk Shikalo ni aina ya magolikipa wa kisasa kuzidi Metacha Mnata.

SAVES

Moja ya tatizo kubwa ambalo Metacha Mnata huwa linamsumbua ni uwezo wa kufanya “saves”. Tatizo hili siyo kubwa sana kwa Farouk Shikalo ukilinganisha na Metacha Mnata. Farouk Shikalo anajua kufanya “saves” kuzidi Metacha Mnata.

KUCHEZA KROSI

Moja ya madhaifu ya Metacha Mnata ni kupanga safu yake ya ulinzi kwenye mipira ya krosi au kona. Pamoja na kwamba hajui kuipanga safu yake ya ulinzi lakini pia siyo mzuri kuicheza hiyo mipira hasa ya kona. Hii ni tofauti na Farouk Shikalo ambaye ni mzuri kwenye mipira ya krosi na anajua kuipanga vyema safu yake ya ulinzi.

UTULIVU WA MPIRA MIGUUNI.

Kwenye mechi ya juzi dhidi ya Namungo FC, miguu ya Farouk Shikalo ilikuwa na utulivu mzuri kila ilipopata mipira. Hii ni tofauti kabisa na Metacha Mnata ambaye siyo mtulivu akiwa na mpira miguuni.

KUSAMBAZA MIPIRA

Farouk Shikalo anasambaza vyema mipira. Anajua kupiga pasi ndefu na fupi kwa uhakika tofauti na Metacha Mnata. Metacha Mnata huwa anapoteza mipira mingi anavyosambaza mipira.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

68 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Sergio Ramos

Je, klabu zinaweza kuvunja utaratibu kwa mchezaji pendwa?

SIMBA VS PLATNUM

Thamani ya miguu ya mastaa wa kigeni wa Simba