PAMEKUWAPO na dhahania nyingi za ‘ikiwa’ na ‘lakini’ kuhusishwa na uwezekano wa Arsenal kutwaa ubingwa wa England lakini wikiendi iliyopita, kwa mara ya kwanza, ilionekana kana kwamba wapo tayari kufanya hilo.
Hakuna timu imekuwa mbele namna hii wakati mwaka ukimalizika halafu ikashindwa kutwaa ubingwa katika historia ya ligi hii kubwa zaidi England. Uongozi wao utaweka pengo la alama 10 ikiwa watawapiga Newcastle kwenye mechi yao nyumbani leo na ubingwa utakuwa tayari kwao, washindwe wenyewe.
Kocha Mikel Arteta amejaribu kuepuka au kupuuza simulizi za jinsi hii, labda akijua kwamba shinikizo lilikuwa upande wao wakati wakipambania kumaliza katika nafasi nne za juu msimu uliopita. Hata hivyo, kuna sababu zinazoonesha kwamba Arsenal wana uwezo wa kutwaa ubingwa safari hii, mara ya kwanza tangu msimu wa 2003-04.
Arsenal sasa wanaonekana kuwa vizuri kisaikolojia na kila wakiingia mchezoni wanakuwa na mawazo ya kushinda. Katika kila mechi wanaonesha viwango vipya vizuri, wakiwa wamebadilika sana na kujiamini, baadhi ya visababishi ni kuingia kikosini kwa Gabriel Jesus na Oleksandr Zinchenko kutoka Manchester City.
Uthabiti uliokuwa unakosekana safari hii upo dhahiri, kama walivyoonesha walipocheza na Aston Villa na Liverpool. Jesus, ambaye sasa ni majeruhi amekuwa kama kiongozi, akitoa ushauri kwa wenzake na amemsaidia aliyechukua nafasi yake, Eddie Nketiah.
“Bado anatupa nguvu sana kwa kila kitu anachofanya kwenye uwanja wa mazozi,” nahodha Martin Odegaard anasema.
Tangu msimu huu uanze, Odegaard amekuwa katika hali nzuri, akichangia usaidizi wa mabao matatu na kufunga moja katika michezo miwili. Amehusika katika mabao 12 msimu huu – mengi kuliko aliyohusika nayo kwenye mechi 36 msimu uliopita.
Anavyokokota mpira kwenda mbele na kurudi nyuma, na jicho lake la pasi kwa Gabriel Martinelli kwenye nusu ya kwanza ya mechi dhidi ya Brighton & Hove Albion Jumamosi pamoja na fagia fagia yake na kusababisha mwenzake kufungia timu yao bao la nne vilionesha kiwango chake.
Ni mchezaji aliyepewa maelekezo na Arteta wakati wa mapumziko na hakika amekuwa akiongoza kwa vitendo badala ya kupayuka tu.
“Huwa ninazungumza pale ninapojisikia kufanya hivyo na husema kile ninachoona chafaa kusema; nafanya kile kinachotakiwa kwa wakati muafaka,” anasema.
Mikimbio ya Odegaard inapewa uwiano na kazi nzuri ya Thomas Partey, ambaye ameonesha utofauti na uzuri tangu kusajiliwa kwake 2020. Kiungo huyo amekuwa mtamu sana uwanjani na itakumbukwa jinsi alivyofanikiwa kumpokonya mpira Declan Rice — akianzisha muvu iliyopelekea bao la kusawazisha la Bukayo Saka dhidi ya West Ham United — dakika chache baada ya kufanikiwa kumkaba Michail Antonio, aliyekuwa tayari kufunga bao, akitaka kufanya 2 – 0.
Jumamosi alimnyang’anya mpira Tariq Lamptey, akipelekea bao la kwanza la Saka, akikaa kwenye nafasi mujarab wakati Brighton wakikimbilia kufunga bao. Takwimu zote muhimu chanya kwa Partey zimeboreka msimu huu, ikiwa ni pamoja na anavyoshinda kumiliki mpira, tachi zake, pasi na uchache wa faulo anazofanya.
Arteta, kwa madirisha mawili ya usajili yaliyopita, ameshindwa kuingiza kikosini aina ya kiungo alichotaka na anajua kwamba kikosi chake si kipana vile. Amefanya mabadiliko machache sana kwenye first eleven zake anzia kuliko makocha wengine wa timu kubwa msimu huu na amekuwa akibadilisha wachezaji baadaye sana.
Alijaribu kupumzisha wachezaji wakati Arsenal wakiongoza 3 -0 baada ya dakika 60 dhidi ya Brighton, kasha wakiwa 4-1, lakini walioingia walikuwa kutu. Hata hivyo, walifanikiwa kumaliza wakiwa na matokeo mazuri.
Arteta amehakikishiwa kwamba zipo fedha kwa ajili ya usajili katika safari yake ya karibuni kuzungumza na wamiliki wa klabu nchini Marekani. Anasema anataka mchezaji sahihi na si wajaza kikosi tu, na habari zilizopo ni juu ya Mykhailo Mudryk, aliyeandika kwenye mitandao ya jamii juu ya kiu yake ya kutua London Kaskazini.
Hata hivyo, hadi majuzi Shakhtar Donetsk walikuwa bado wakimng’ang’ania, wakikataa ofa ya Arsenal, wenyewe wakitaka wapewe pauni milioni 85 kwa winga huyo.
Ilionekana awali kwamba kuumia kwa Jesus kwenye Fainali za Kombe la Dunia kungekuwa balaa kubwa kwa Arsenal na matumaini yao ya ubingwa. Mshambuliaji huyo aliyeumia goti atakuwa nje hadi mwezi ujao, lakini mambo bado yanakwenda vyema kwa Arsenal uwanjani, wakiwa na Nketiah.
Tofauti na wapinzani wao, Arsenal hawakabiliani na matakwa na Ligi ya Mabingwa na hivyo wanatakiwa wawe na uwezo wa kufanya mabadiliko zaidi wanapoanza Ligi ya Europa, wakati Liverpool na City wanajua kwamba lazima waweke kikosi cha kwanza mara nyingi.
Arsenal ni timu ya tano tu katika historia ya Ligi Kuu ya England kutwaa alama 43 au zaidi katika mechi 16 za awali za msimu. Katika misimu miwili iliyopita, City walichukua kombe wakiwa na alama 86 na 93 mtawalia. Pengijne Arsenal watatakiwa kutwaa alama nyingine 47 katika mechi 66. Arsenal wameifanya Emirates kuwa ngome imara, wakishinda kwa asilimia 100.
Mechi kumi zijazo za Arsenal:
Jioni ya Leo: Newcastle (h)
Jan 15 Tottenham (A)
Jan 22 Manchester United (h)
Feb 4 Everton (a)
Feb 11 Brentford (h)
Feb 15 Man City (h)
Feb 18 Aston Villa (a)
Feb 25 Leicester (a)
March 4 Bournemouth (h)
March 11 Fulham (a)
Comments
Loading…