in , , ,

KUELEKEA KWENYE MECHI YA CHELSEA NA ARSENAL

Kitu kinachomuumiza Wenger kwa kipindi hiki ni namna gani atakavyoweza
kuziba pengo la kiungo kwa sababu ya majeraha yanayomkumba katika
eneo lile.

Kuna hatihati ya Ramsey kutocheza, Carzola ni majeruhi wa muda mrefu,
Xhaka anatumikia adhabu ya kutocheza mechi 4 na Elney yupo Gabon na
timu yake ya Misri kwenye michuano ya Afcon.

Hii inamfanya awe na maswali mengi ya nani atakayeweza kucheza na
Francis kwenye eneo hilo la kiungo.

Kwa kiasi kikubwa Chamberlain ataingia moja kwa moja kwenye cha leo.
Kuanza kwa Chamberlain kutakuwa na faida na hasara zifuatazo.

Faida: Uwepo wa Chamberlain utasaidia kuongeza kasi ya mashambulizi
yanaoanzia katikati ya uwanja hii ni kutokana na kasi yake aliyonayo.

Pia kwa hivi karibuni Chamberlain amekuwa akihusika vizuri kwenye
magoli yani kufunga na kutoa msada ya magoli, akiwa na mwendelezo wa
hii tabia atakuwa na msaada mkubwa sana kwenye timu.

Hasara: Ili uwazibe Chelsea kwa kiasi kikubwa unatakiwa uwakamate
Kante na Matic ili wasiweze kusambaza mipira maeneo ya pembeni yani
kwa kina Alonso na Moses ambao huleta uhai wa mashambulizi ya Chelsea.

Hivo kiungo anayehitajika ni mwenye uwezo wa kukaba na kushaanzisha
mashambulizi kwa wakati mmoja.

Kuwepo kwa Francis kunaipa nafasi kubwa Arsenal ya kuwa na mtu mwenye
uwezo wa kukaba lakini asipopata msaidizi katika eneo la ukabaji
inaweza kuwagharimu sana Arsenal kwa kiasi kikubwa.

Eneo jingine ambalo linahitaji busara kubwa kwa Arsenal kwenye mechi
hii ni eneo la ushambuliaji.

Mabeki wa Chelsea wamekuwa imara sana kwa kiasi kikubwa, hivo ili
uwaghasi unahitaji mshambuliaji ambaye hatulii kwenye eneo lake, na
siyo mshambuliaji ambaye anakaa muda mwingi kwenye eneo lake kwa
sababu ni rahisi kumkaba hasa hasa kwa njia ya man to man.

Kwa hiyo Arsenal watakuwa na nafasi nzuri ya kushinda kama mbele
wataanzisha watu wenye mbio.

Wakiwaanzisha Sanchez Welbeck Iwobi itakuwa na faida kubwa sana kwao
kwa sababu, kumwanzisha Welbeck kama mshambuliaji wa kati unapata
faida mbili, moja Welbeck ana uwezo Mzuri wa kumalizia, pili Welbeck
anatabia ya kuhama hama eneo lake, hii itakuwa na msaada mkubwa kwa
kina Sanchez na Iwobi kuwa na uwezo wa kuingia moja kwa moja kwenye
eneo la kumi na nane kwa Kubadilishana kipindi ambacho Welbeck anahama
eneo lile.

Ubora wa Chelsea unaanzia kwa kina Kante na Matic, hawa ndiyo wenye
Ufunguo sahihi wa mashambulizi, ndiyo wanaoamua mashambulizi ya
Chelsea yaanzie upande upi mwa uwanja.

Hivo ukiwabana Kante na Matic unakuwa umenyima huduma za mipira kwa
kina Moses na Alonso ambao wamekuwa mhimili mkubwa kwenye mashambulizi
ya Chelsea.

Kuna kitu ambacho Alonso na Moses wanatakiwa wawe makini nacho kwenye
mchezo wa leo.

Arsenal wanawashambuliaji wa pembeni wenye kasi, hivo wasijisahau
sana kurudi nyuma haraka pindi wanapoenda kushambulia.

Martin Kiyumbi

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Serengeti boys

SERENGETI BOYS YAFUZU FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA

Tanzania Sports

CAMEROON MABINGWA WAPYA AFRIKA