in , ,

Kepa katuonesha SARRI hana SAUTI NZITO !

Ulikuwa unatazama fainali ya Carabao Cup?, bila shaka jicho lako ulilipa muda mwingi kwa ajili ya fainali hii.

Fainali ambayo ilikuwa inakutanisha timu kubwa kwa sasa pale England (Manchester City na Chelsea).

Timu ambazo zinasifika kuwa na makocha ambao kwa kiasi kikubwa wanaamini katika mpira mzuri wa kuburudisha.

Ndivyo ambavyo timu zao zinacheza, huchoki kuziangalia kwa kiasi kikubwa. Chelsea akikamata mpira utafurahia jinsi anavyoupamba mpira rangi.

Hata mpira ukitua miguuni mwa wachezaji wa Manchester City basi nafsi yako lazima iburudike sana kwa sababu mpira hutua kwa wakuu wa washereheshaji wa mpira duniani.

Kwa sababu tu wanaongozwa na mkuu wa ushereheshaji duniani (Pep Guardiola). Huyu ni Genius wa mpira.

Ana heshimika sana. Mashabiki wengi wa mpira wanamweheshimu sana, na mashabiki ambao ni wapinzani wake wanamuogopa sana.

Kwa sababu tu ya alama ambayo ashawahi kuiweka kwenye mpira wa miguu duniani. Alama ambayo humfanya aonekane ni kocha bora sana.

Kocha wa kutisha sana, ndiyo maana kuna wakati watu huwa hawatamani kukutana naye kwenye mechi kwa sababu tu huwa na asilimia kubwa ya kukudhalilisha.

Heshima hii imemfanya mpaka aheshimike kwa wachezaji wengi anaowafundisha kila anapopita kufundisha duniani.

Na wachezaji wengi hutamani sana kufundishwa naye kwa kukuamini kuwa kuna kitu kikubwa sana anachoweza kuwapa wachezaji kupitua kuwafundisha.

Hii huwa inafaida kubwa sana kwa Pep Guardiola, kwa sababu kupitia heshima anayoipata kupata kwa wachezaji humuonesha kuwa ana nguvu sana.

Siyo nguvu ya mwili, hapana nguvu ya sauti. Nguvu ya sauti ya kwenye vyumba vya kubadilishia nguo mpaka kwenye uwanja.

Huwa naamini ushindi siku zote huanzia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Hapa ndipo ushindi unapoanzia.

Hapa ndipo ile hali ya hewa ya kutengeneza ushindi huwa inaanzia hapa. Kwa sababu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo huwa kunatengenezwa mahusiano.

Mahusiano ambayo huwa yanakuwa na muunganiko kuanzia kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa ujumla.

Yani wachezaji wanakuwa pamoja au wamoja kwanza wao wenyewe. Pia wachezaji wanakuwa wamoja au pamoja na benchi la ufundi.

Wote huwa kitu kimoja, wote huwa na wazo moja. Na wote kwa pamoja huaminiana. Yani kocha anawaamini wachezaji wote, na wachezaji wanamwamini kocha.

Yani kile ambacho mchezaji anakifanya kocha anatakiwa kukiamini, na kile ambacho kocha anakifanya lazima wachezaji waamini kupitia yeye.

Kwa sababu yeye ndiye husimama na kuwatazama na kuona mapungufu ndani ya uwanja. Yani umoja huu ndiyo huwa mwanzo wa ushindi ndani ya timu.

Hiki kitu kikikosekana tu, huwa kinaharibu sana hali ya hewa ya timu hata kama timu ina wachezaji bora kiasi gani, lakini haiwezi kufanya vizuri kwa sababu haiyokuwa na muunganiko mzuri wa kimahusiano.

Mahusiano mazuri huwa ni mbinu kubwa sana ya kupata ushindi kwa makocha wengi. Kwa sababu huwa wanaamini wachezaji wanaweza kuwapigania wao kwa nguvu.

Hiki kitu jana kilikosekana kwenye timu ya Chelsea. Kuna kitu cha tofauti kabisa tulikiona. Golikipa wa Chelsea alipokataa kutolewa.

Umesoma huko juu ?, kuna sehemu nimekuambia kuwa kocha na wachezaji lazima waaminiane , na hii ni kwa sababu ya mahusiano bora ambayo wameyajenga .

Wachezaji lazima waamini maamuzi ya kocha kwa sababu wamemuamini yeye ndiye kiongozi mkuu. Yeye anaona vizuri kuliko wao.

Chochote anachokifanya lazima kiwe kwa manufaa ya timu. Imani hii haiji hivi hivi tu, inakuja kwa kujengwa kwa mahusiano imara ndani ya timu.

Kuna timu kinaonekana hakipo sawa kwenye timu ya Maurizio Sarri. Kuna sehemu amelegeza. Hakuna mahusiano imara ndani ya kikosi na baadhi ya wachezaji.

Ndiyo maana inafikia mchezaji kugoma kutoka. Kungekuwa na mahusiano imara ndani ya timu basi kungekuwepo na ile heshima ya wachezaji kwa kocha.

Kepa alikosa heshima kwa kocha wake. Na heshima hii aliyoikosa, inawezekana sana Maurizio Sarri hakuitengeneza awali ndiyo maana hakuipata Jana.

Hapa ndipo mzizi wa ushindi unapoanzia. Kwenye mahusiano imara. Yani bila mahusiano imara hakuna kitu kinachoitwa ushindi kinaweza kukutembelea.

Maurizio Sarri anatakiwa kujifunza kuwa na sauti, sauti ambayo anatakiwa kuitengeneza kwa kuweka mahusiano imara kabisa ndani ya kikosi chake cha Chelsea.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Paul Godfrey katusahaulisha Juma Abdul

Tanzania Sports

Manchester United haina njia MBADALA!