in

Juma Abdul, Yondani Hawakunusa Harufu

Katika maisha ya kawaida ya mpira wa mgiuu inatakiwa unuse harufu ya mafanikio haraka iwezekanavyo vinginevyo utakwama mazima na hujui utatokea wapi baada ya mambo kubadilika.

Yanga na Simba moja ya vilabu ambavyo havishikiki unapotaka kuvizungunza wengi wanataka useme yaliyo mazuri tu. Vivyo hivyo kwa wachezaji pia wanapenda waongelewe vizuri sio upande wa pili wa mabaya.

Yanga waliwaacha nyota wake wawili Juma Abdul pamoja na Kelvin Yondani baada ya kushindana maslahi binafsi.

Yondani yeye kajikalia kimya anakula pensheni zake wala hatusikii kutaka kwenda wapi wala wapi, kuna dili moja ilikuja dhidi ya JKT Tanzania wakashindana.

Lakini upande wa Juma Abdul kila kukicha tunasikia habari mpya juu yake. Mara anasema atapata timu mara anataka kwenda wapi, hebu tuangalie ripoti yake ya hivi karibuni.

Beki huyo amesema kwa sasa anafikiria zaidi kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na kuna dili analisubiri na kama likitiki tu anasepa.

Miaka yake huenda ikabakia miwili yakucheza soka la nguvu na ushindani  kwa umri wa pasipoti.

Beki huyo mtaalamu kwa krosi amesema kwa sasa hajasaini timu yoyote hapa nchini labda dili lake la kwenda nje likwame ndipo anaweza kufikiria timu nyingine ya kwenda.

Akiwa Yanga msimu wa 2019/20 alitoa jumla ya pasi sita za mabao kwa mguu wake wa kulia aliachwa na Yanga baada ya kushindwana kwenye masuala ya mkataba.

Abdul pamoja na beki mwingine wa kati, Kelvin Yondani walitangazwa kuachwa na Yanga klabu ambayo waliitumikia kwa miaka nane.

Hata hivyo kumeibuka maneno kuwa klabu hiyo imepanga kuwaita tena mezani wachezaji hao wazoefu ili kufanya nao mazungumzo ya kuwemo katika kikosi hicho msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Ukiachana na mazungumzo labda namie nitoe mawazo yangu juu ya watu hawa wawili.

Ni kweli maslahi yalikuwa muhimu zaidi kuliko kitu chochote lakini kama kile tulichokisikia juu ya kupewa hela ya usajili na mshahara kuongezewa ndio sababu ya kuondoka ilikuwa kitu cha kujifikiria.

Upande wa  Yanga ulikuwa tayari kuongeza mshahara ila sio kutoa hela ya usajili.

Sidhani kama watu hawa walipata washauri sahihi juu ya mustakabali wao.

Kwa Yondani sina shida sana kwakuwa yeye mwenyewe amenyuti haongei chochote ila Juma kila siku anatoa habari mpya.

Kuna wakati alisema wazi kuwa atapata timu kubwa miongoni mwa kubwa tunazozifahamu.

Wengi walihusishwa na kusaini Simba kusaidiana na Shomari Kapombe wengine walisema ataenda  Azam FC.

Lakini  kote huko kunaonekana tayari kumeota nyasi, na mishahara ambayo Juma na Yondani hawawezi kufika.

Na hii ndio sababu hata timu ndoto zinashindwa kuomba hudu mazao.

Inawezekana kabisa kupata ya timu ya kuitumikia aila hela wanayoitaka wataiweza hapo ndipo palikuwa pakufikiria kabla ya chochote.

Juma ambaye anatupa stori za kuandika kila kukicha alipaswa apate mshauri mzuri ili aliangalie hili kwa ukubwa wake.

Tatizo sio kuwa na timu je hata wakipata hizo timu ambazo sio Yanga, Simba na Azam wataweza kupata kile wanachokitaka?

Hiki ndicho walipaswa kukiangalia na wangepata jibu wakati wanafanya mashauri na waajiri wao wa zamani.

Hapa sasa ndipo unagundua kuwa ‘Timing’ yao haikuwa nzuri walipaswa kuangalia mbele zaidi.

Juma atawaambia nini watu kama atakosa kabisa dili ambalo analisema na kubakia pale alipo au asipate timu kabisa.

Ukweli ni kwamba Namungo, KMC na Mbeya City sio kwamba hawataki huduma za nyota hawa wanazihitaji sana tatizo chambichambi wanaweza kuwalipa zaidi ya makadirio yao waliyo yapanga?

Ukubwa wa wachezaji hao huenda pia wanatamani wasaini dili katika timu ndogo hata kama mshahara mdogo lakini kwa haya (Aibu)  tulizoumbwa nazo binadamu huenda wakaona si vyema kwenda huko .

Lakini pia huenda wakasimamia msimamo wao juu ya maslahi wanayoyataka wakiangalia tayari washafika maji ya jioni.

Juma Abdul bado nafasi yake iko wazi Yanga, sijafikiria kama Kibwana Shomary na Paul Godfrey wataweza kuziba ufa aliouacha.

Alitakiwa abaki awape ujuzi na hata akistaafu Paul Godfrey na Kibwana  watakuwa wamekamilika.

Juma Abdu
Juma Abdu

Kwa Yondani sehemu yake ya kucheza pale Yanga kunamushkeri kwakuwa tayari kuna watu wamejaa lakini ilikuwa muhimu kubaki ili kuongea chachu na uzoefu wake ungesaidia sana.

Hapakila mmoja anasubiri kumuona Juma akiwa na uzi mpya huku mkongwe Yondani naye akiwa katika majukumu  mapya.

Lakini hii iwe fundisho kwa wengine wote ambao wanasuasua juu yamaamuzi matukio kama haya yanatakiwa wayapatie ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Swali lingine la wazi Yanga watathubutu kuwafuata tena au wataamua kuachna nao kama walivyotoa taarifa.

Ningekuwa mimi ndio kiongozi wa Yanga kama  mfanyakazi wangu alinifanyia kazi nzuri ningewafuata tena.

Najua kutakuwa na maneno mengi sana juu ya kuwafuata tena na kuanza mazungunzo mapya ila ningefanya hivyo kwa ajairi ya uhai wa timu.

Hasa ule upande wa kulia bado nahisi anatakiwa mtu mzoefu zaidi kuweza kuikabili sehemu ile.

Hivyo turufu yangu kubwa kwa beki wa kulia  Juma Abdul angefuatwa tena.

Juu ya Kelvin Yondani ni mchezaji ninaye muheshimu kama watamfuata itakuwa jambo la busara sana kuongeza ukubwa wa kikosi naheshima pia.

Haya tumalize hapo chini vipi Rwandamina, Hans Van Pluijm au Stewart Hall ? ngoja tuone watatuletea kocha gani Yanga.

Toa mawazo yako hapo chini ili tushiriki kwa pamoja mawazo yetu.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply
  1. Kimsingi Yanga na Yondani wangekaa chini wayajenge kwa kila mmoja kukubali kupoteza kwa ajili ya kulindiana heshima.Kisha watengeneze mpango mkakati utakaomfanya Yondani astaafu kwa heshima akiwa Yanga.Jambo hilo litawajenga wachezaji waliopo sasa kiakili na kujua kwamba baada ya muda hawatatupwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
LM

Fedha, makocha na vifaa;

Tanzania Sports

Kocha wa YANGA kaja kuifunga Simba