in ,

Jude Bellingham kufuata nyayo za Waingereza Real Madrid

.

Nyota huyu anakuwa wa sita mzawa wa England kujiunga na Real Madrid. Jude amesaini mkataba wa miaka 6 na tayari ametangazwa na miamba hiyo ya Hispania…

ENGLAND ni nchi ambayo wachezaji wake wengi wanacheza Ligi ya nyumbani. Mara chache sana kuona wachezaji wazawa wa England wakitoka kwenda Ligi za nchi zingine kama vile Italia, Hispania,Ufaransa,Ujerumani na nyinginezo. Wengi wa wachezaji wao wanapenda kubaki EPL ambako kumewavutia wachezaji wa kigeni pia. 

Baadhi ya wachezaji waliowahi kwenda Ligi zingine wamefanikiwa kuonesha vipaji vyao na kudhihirisha kuwa inawezekana kwa wachezaji wa England kwenda kwingineko. Jude Belllingham ameingia katika orodha ya wachezaji ambao wamekwenda kucheza Ligi za nje. Nyota huyu alikuwa mchezaji wa Birmingham  City kabla ya kujiunga na Borussia Dortmund kwa dau la pauni milioni 25 tu. 

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 hajachukua uamuzi kama wa Owen Hargreaves ambaye aliamua kuondoka Bayern Munich kurudi nyumbani EPL alipojiunga na Manchester United. Vilabu vingi vilionesha nia ya kumsajili Jude Bellingham, lakini mwenyewe amechagua kwenda Real Madrid. Uamuzi wa Belllingham unaonesha namna alivyojifunza maisha nje ya EPL na kuamini kuwa inawezekana kufanya vizuri bila kusakata kabumbu EPL. 

Tanzania Sports

Nyota huyu anakuwa wa sita mzawa wa England kujiunga na Real Madrid. Jude amesaini mkataba wa miaka 6 na tayari ametangazwa na miamba hiyo ya Hispania. Wapo wazawa wengine sita wa England ambao wamecheza soka Real Madrid hivyo Jude Bellingham anakuwa mchezaji was aba kutoka nchi hiyo. Baadhi ya wachezaji hao walisajiliwa moja kwa moja kutoka EPL, lakini kwa Jude Bellingham hali imekuwa tofauti kwani amejiunga akitokea Ligi Kuu Ujerumani maarufu kama Bundesliga.  Je ni nyota gani wengine wa England waliowahi kucheza Real Madrid?

LAURIE CUNNIGHAM

Alisajiliwa kutoka West Bromwich Albion mwaka 1979. Huyu alikuwa winga na mchezaji wa kwanza wa England kujiunga Real Madrid. Alifunga mabao 20 katika mechi 66 za mashindano yote aliyoshiriki, mengi yakiwa katika msimu wake wa kwanza na nusu katika klabu hiyo ambako ilifanikiwa kutwaa taji la La Liga. Nyota huyo alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Real Betis mnamo Desemba 1980, na baada ya hapo akawa mchezaji wa kuuguzwa zaidi kuliko kucheza soka. Majeraha yalimlazimu kukosa mchi nyingi na hata alipopona Real Madrid iliamua kumtoa kwa mkopo kwa kipindi cha miaka miwili. Cunningham alifariki dunia katika ajali ya gari jijini Madrid Julai 1989 katika kipindi ambacho alikuwa akicheza klabu ya Rayo Vallecano. Kifo chake kilimkuta akiwa na umri wa miaka 33 tu. 

STEVE McMANAMAN

Nyota huyo aliwika zaidi alipokuwa Liverpool. Alikuwa winga machachari aliyetetemesha timu nyingi za EPL akicheza nafasi ya winga. Uwezo wake wa kukokota mpira,kupiga chenga na kasi vilimpa sifa kubwa ya kuwindwa na Real Madrid. Mwaka 1999 aliamua kujiunga na Real Madrid ambako mara nyingi alicheza kama kiungo wa kati na mara chache nafasi ya winga kama alivyokuwa Liverpool. 

Sababu ya Steve kupangwa kiungo wa kati ni kutokana na matumizi yake ya nguvu na stamina aliyokuwa nayo. Kwa kipindi cha misimu minne akiwa Santiago Bernabeu alitwaa mataji mawili ya La Liga na mawili ya Ligi ya Mabingwa. Katka mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2000 dhidi ya Valencia alichaguliwa kuwa mchezaji bora mechi. McManaman hadi sasa amekuwa katika orodha ya wachezaji wakongwe wa Real Madrid tangu alipostaafu kucheza soka. Huyu anatajwa kuwa mchezaji wa England aliyekuwa na uwezo wa kupiga chenga na kasi kubwa kuliko wengine.

DAVID BECKHAM

Baada ya Luis Figo, Zinedine Zidane na Ronaldo De Lima, Beckham ni kijana mwingine aliyeibukia katika kikosi cha mastaa wa real Madrid ambacho kilikuwa maarufu kwa jina la Galactico. Usajili wake ulikuwa ni mtindo uleule wa Florentino Perez ambaye alikuwa anasajili mastaa katika kikosi chake na liweza kumwaga fedha ya kumpata nyota yeyote. 

David Beckham alijiunga na Real Madrid wiki chache kabla ya Steve McManaman kuuzwa Manchester City mwaka 2003. Nahodha huyo wa England alikuwa kiungo asiyeshindika katika kipindi cha miaka mitatu. Alicheza vema, akalifanya eneo la kiungo la Real Madrid kuwa imara zaidi lakini bahati mbaya alikosa ubingwa kipindi hicho. 

Beckham hakuwa na mahusiano mazuri na kocha Fabio Capello katika msimu wake wa mwisho. Msuguano wa Capello ulisababisha Beckham kuondolewa kikosini na kuwekwa kando kabla ya  kurudishwa na akaonesha kiwango kikubwa cha kusakata kabumbu na kufanikiwa kutwaa taji la La Liga 2006/2007. Baadaye aliondoka Real Madrid na kwenda kujiunga na klabu ya LA Galaxy ya Marekani.

MICHAEL OWEN

Akiwa katika umri mdogo na kiwango kikubwa Michael Owen hakusita kuchukua fursa ya kujiunga na Real Madrid. Ingawaje baadhi ya wataalamu wa soka wanasema uamuzi wa kujiunga Real Madrid mwaka 2004 ulichochea kuporomoka kiwango na uwezo wa nyota huyo katika kandanda. Kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 24 tu. Mshambuliaji huyo alikuwa mahiri kupachika mabao na anakumbukwa kwa kuwafunga Barcelona katika mchezo wa El Clasico, lakini asilimia kubwa za mechi alizocheza alikuwa akitokea benchi kuchukua nafasi ya Raul Gonzalez au Ronaldo De Lima katika safu ya ushambuliaji. Baada ya kudumu kwa msimu mmoja 2004-2005 aliondoka Real Madrid kwenda kujiunga na Newcastle United. Uamuzi huo ulikuja baada ya Real Madrid kuwasajili nyota wawili wa Kibrazil Robinho na Julio Baptista.

JONATHAN WOODGATE

Maajabu ya beki huyu aliyesajiliwa kutoka Tottenham Hotspurs katika msimu wake wa kwanza tangu alipojiunga na Real Madrid hakucheza mechi hata mota kati ya 38 za La Liga. Woodgate alikuwa anakabiliwa na majeraha, lakini tukio la kukumbukwa pia ni pale alipojifunga katika mchezo wake wa kwanza akiwa Real Madrid dhidi ya Athletic Club. Woodgate alicheza mechi hiyo baada ya kuwa majeruhi kwa miezi 13 tangu aliposajiliwa. 

Wakati akihusishwa na kusajili Real Madrid bado alikuwa akitibu majeraha yake. Hatua aliyofanya ni kuanza kujifunza lugha ya Kihispania na kusoma habari nyingi zilizoripotiwa kuhusu masuala ya soka ukiwemo usajili wake. Beki huyo alikuwa Madrid kwa msimu 2005-2006 kabla ya kutemwa na miamba hiyo ya Hispania na kupelekwa kwa mkopo katika klabu ya Middlesbrough ambayo ilimsajili jumla mwaka 2007. Woodgate na Oowen ni wachezaji wa England ambao hawakufanikiwa kutwaa taji lolote wakiwa Real Madrid. 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Ligi Kuu Tanzania kama Umoja wa Mataifa

Tanzania Sports

Presha kubwa Kocha mpya wa Yanga