in , , ,

Eric Ten Hag amekosea..

Sancho hamwelewi Aaron Wan-Bissaka

MECHI tano Manchester United wana pointi 6. Wameshinda mechi mbili, wamefungwa tatu. Katika mazingira hayo bado mashabiki wameshindwa kuvumilia baada ya kumzomea kocha wao Eric Ten Hag kwenye mchezo wao dhidi ya Brighton. Ulikuwa ujumbe kuwa hali ya Manchester United si nzuri na wachezaji pamoja na benchi la ufundi wanatakiwa kuamka na kuleta furaha kikosini. 

Katikati ya jinamizi la kusaka pointi kuna msuguano mwingine kati ya kocha mkuu Eric Ten Hag na winga wake Jadon Sancho. Wawili hawa hawaelewani kabisa. Alianza kocha Eric Ten Hag ‘kuropoka’ mbele ya kamera za Televisheni alipoulizwa swali ili kutoa sababu kwanini hakumjumuisha winga Jadon Sancho kwenye kikosi cha kwanza au benchi. 

Ten Hag hakuelewa mtego uliokuwepo mbele yake, akategeka na kuingia mazima, akasema Jadon Sancho hakufanya vizuri kwenye mazoezi ya timu hiyo. Hivyo Ten Hag alisistiza kiwango duni mazoezini kilimfanya ashindwe kumjumuisha. Kauli hiyo inaonekana kumkera zaidi Jadon Sancho ambaye bila uvumilivu na heshima akaandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akipinga kile kilichosemwa na kocha wake.  

Tanzania Sports

Sancho alisisitiza anataka kucheza mpira na si vinginevyo. Kana kwamba haitoshi, Eric Ten Hag amesema uongozi wa klabu ya Manchester United ulimwambia kuwa arudishe utamaduni wa nidhamu wa timu hiyo, kwani makocha waliopita baada ya kustaafu Sir Alex Ferguson hawakuwa wakichukua hatua kali dhidi ya mastaa wa timu hiyo. 

Wakati kidonda hakijapoa, Sancho amekataa kuomba radhi kwa kocha wake na hivyo ameondolewa katika kikosi cha kwanza na haruhusiwi kufanya mazoezi na timu hiyo. Hili ni balaa lingine.

Wikiendi hii Manchester United wamepokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa kikosi cha Brighton cha Roberto De Zebri. Kilikuwa kipigo kwenye dimba lao la nyumbani la Old Traford. Yaani siku hizi Old Traford watu wanajipigia tu kama hawana akili nzuri. Ule umwamba wa Old Trafird umeyumba kwa kiasi kikubwa. 

SANCHO HAKUMWELEWA WAN BISSAKA

Tanzania Sports

Inawezekana Eric Ten Hag angeweza kukwepa mtego wa swali alililoulizwa, lakini alikosea na kisha Jadon Sancho akaharibu zaidi. Kama kuna mchezaji wa Manchester United ambaye alipitia wakati mgumu na kutishiwa kuporwa namba basin i Wan Bissaka. Beki huyo alikuwa na dalili zote za kuondoka, na hakuwa na uhakika kucheza kikosi cha kwanza.

Maneno yote aliyasikia, alijua nini kitakachoendelea lakini Wan Bissaka hakuwahi kuzungumza kokote, hakuwa tayari kuwa sehemu ya zogo ndani ya Old Traford. Lakini katika mazingira ya kibinadamu mchezaji huyo alifahamu hatima yake iko mikononi mwake. Shukrani kwa washauri wake hawakumfanya aropokwe wala kujaribu kuanzisha ‘bifu’ na kocha wake Eric Ten Hag. Kwa Wan Bissaka aliacha muda uzungumze. 

Akatoa nafasi kwa kazi yake kuzungumza. Taratibu Wan Bissaka ameanza vizuri msimu huu na ameonesha hali nzuri kimchezo kuliko msimu uliopita. Wan Bissak anaweza kuwa somo zuri kwa Jadon Sancho. Ni somo pia kwa wachezaji ambao wanatafuta ugomvi na benchi la ufundi. Kimsingi Wan Bissaka alijielewa, alielewa na kumwelewa Eric Ten Hag. Jambo zuri akaonesha utulivu, amekuwa mtiifu na anacheza kwa ari na kujituma katika mfumo unaoagizwa na kocha wake. Wan Bissaka ameonesha busara kubwa na ustahimilivu kuliko Sancho. Tena tofauti ni kubwa sana. ni kocha gani hapendi kuwa na mchezaji mtulivu na asiyehitaji zogo nje ya uwanja zaidi ya kuimarisha uwezo wake kiuchezaji? Bila shaka Wan Bissaka anawatamanisha makocha wengi ili wamsajili.

LAITI ANGEKUWEPO FERGUSON

Kama kuna kitu ambacho wachezaji wa Manchester United wana bahati nacho ni kukosekana kwa Sir Alex Ferguson katika benchi la Ufundi la klabu hiyo. Ule umwamba wa Old Traford umedorora. Ule ukali wa timu umeshuka.

Uamuzi mgumu kuchukuliwa na kocha Old Traford umeporomoka sana, angalau Eric Ten Hag anajaribu kudhibiti nidhamu ya timu hiyo. Alikuwepo Cristiano Ronaldo, akatibuana na Ten Hag. Naye kaambiwa aondoke. Ulikuwa uamuzi mkali na msimamo wa aina yake, lakini uongozi wa Manchester United ulitakiwa kukubaliana nao.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Simba,Yanga zatuma ujumbe mzito CAF

Tanzania Sports

Waarabu wameshtuka nini kwa soka la Ulaya?