in , ,

Dakika za lala salama kuwapasua vigogo EPL


PRESHA imepanda. Hivi ndivyo unaweza kusema kuhusu Ligi Kuu ya England katika dakika za
lala salama ambako timu zinacheza mechi zao za 37 wikiendi hii. Vigogo mbalimbali vya EPL
wanahaha,wachezaji wanahangaika na makocha wanataka ka msimu vizuri wakiwatika nafasi
ambazo wanaweza kuziita za mafanikio.


Jasho linawatoka mashabiki wenye hofu na imani kuhusu timu zao. Akilini mwa kila shabiki
kumejaa matumaini na hofu pia. Hakuna mwenye uhakika kati ya timu tatu nani ataingia kwenye
Top Four’. Kinyang’anyrio cha kuingia Top Four kimekuwa kigumu, huku timu mbili pekee
zimejihakikishia nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao.


Timu zenye uhakika katika nafasi mbili za juu ni Manchester City vinara wa EPL ambao
wikiendi hii wanawakaribisha Chelsea kwenye dimba lao la Etihad, pamoja na wapinzani wao
wa karibu Arsenal ambao waliambulia kichapo bao 1-0 kutoka kwa Nottingham Forest. Kwahiyo
Pep Guardiola na Mikel Arteta hawana wasiwasi kuhusu nafasi zao za juu.
Vita ya makocha


Kocha Erik Ten Hag wa Manchester United hana uhakika kama atamaliza katika nafasi nne za
Ligi Kuu. Jurgen Klopp wa Liverpool naye anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha
haikosi Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Lakini je, makocha hawa wawili wataweza kupenya
katikati ya changamoto zinazowakabili? Eddie Howe anatishia nafasi ya Klopp na Ten Hag.


Howe anaongoza kikosi cha Newcastle United kuwinda nafasi ya nne za juu ambazo
zinamhakikishia kucheza hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa, ambapo wikiendi hii anamenyana
na Leicester City waliojihakikishia nafasi ya kushuka daraja. Makocha hawa hawalali usingizi
mzuri. Kiimani wanaomba wenzao wafungwe na wao washinde mechi zao.
Kimaandalizi wanahaha kutafuta kila njia na mbinu kuhakikisha timu zao zinashinda na kutinga
Top Four. Lakini hakuna kocha mwenye uhakika kati ya watatu hao. Ni vita ambayo imekoleza.


kwenye mbio za EPL.


Namna hazidanganyi; Timu tatu, nafasi mbili
Liverpool wamejikusanyia pointi 66 kutokana na michezo 37 baada ya kutoshana nguvu na
Aston Villa kwa matokeo ya 1-1 wikiendi hii. Newcaster United wamejikusanyia pointi 69
katika mechi 36. Wenzao Manchester United wamejikusanyia pointi 69 kutokana na mechi 36.
Kwa maana hiyo Newcastle United wamebakiza mechi mbili za kumaliza msimu, ambazo
wakishinda zote wanaweza kufikisha pointi 75. Vijana wa Liverpool wamebakiza mechi moja,
ambapo wakishinda zote watakuwa na pointi 69. Baada ya ushindi wa Manchester United dhidi
ya Bournemouth wamebakiza tatu. Ikiwa Manchester United watashinda mechi zote tatu

watakuwa wamepata pointi 75 sawa na Newcastle United. Kimahesabu ya ushindi kwa Man
United na Newcastle maana yake watakuwa wametinga nafasi tatu nan ne kwa pointi 75 ambazo
haziwezi kufikiwa na Liverpool.


Uwezo wa Liverpool ni pointi 69 tu ambazo zitakuwa nne pungufu hivyo wanaweza kuishia
nafasi ya tano. Kitu pekee ambacho Jurgen Klopp na Liverpool yake watakifanya ni kusali sala
zao zote ili wapinzani wake wawili hao wapoteze pointi. Hii ina maana namba hazidanganyi.
hapa, kila mmoja ashinde mechi zake.
Usiku wa Ligi ya Mabingwa

Tanzania Sports


Tayari Arsenal imerudi kwenye usiku wa Ligi ya Mabingwa ambako walipoteana kwa miaka
kadhaa. Man United nao wanajaribu kurudisha zama zao za ukali katika usiku wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya. Eric Ten Hag anataka kuvutia wachezaji zaidi na kuondokana na jinamizi la
kutupwa kwenye mashindano ya Europa. Lakini ili afuzu Ligi ya Mabingwa lazima ashinde
mechi zake zote zilizobaki. Faida waliyonayo Man United ni kwamba wana mechi moja
mkononi kwahiyo wanatakiwa kupambana kwa nguvu na maarifa.


Newcastle United ndiyo mpya katika kinyang’anyiro hiki. Newcastle United hadi sasa wana
mafanikio makubwa kwa nafasi wanayoshikilia sana, huku wakiwa wamepata wamiliki wapya
toka Uarabuni. Pesa ya waarabu bila shaka itakwenda kuboresha kikosi chao, na kumwezesha
kocha wao Eddie Howe kujivunia mafanikio yake.


Ikiwa Newcastle watafanikiwa kufuzu Ligi ya Mabingwa yatakuwa mafanikio makubwa kwa
kocha Eddie Howe raia wa Uingereza. Kwanza atakuwa na uhakika wa kuboresha kikosi chake
kwa vile waarabu watamwaga fedha nyingi pamoja na kujihakikishia marupurupu mengi kwa
malengo ya kufanya vizuri katika usiku wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Njia pekee anayoweza
kushangilia mafanikio ni kuhakikisha anakiongoza kikosi chake kushinda mechi zote zilizosalia.
Duru za kimichezo nazo zinaibua swali juu ya mustakabali wa Eddie Howe kama pesa hizo
zitaendelea kumzunguka yeye ama atatimuliwa. Wachambuzi wanaamini ikiwa atafanikiwa
kufuzu Ligi ya Mabingwa maana yake kipimo kitakuwa mafanikio atakayoleta, kinyume chake
wamiliki wataanza ksuaka makocha wa daraja la juu kumzidi Eddie Howe. Sababu ni rahisi,
uwekezaji mkubwa unawahitaji watendaji wakubwa, na hilo ndilo tishio likalozunguka kibarua
chake hadi siku ya mwisho.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

70 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Kikosi Cha Timu ya Simba Sports Club

Maadui watano wa Simba 2022-23

Tanzania Sports

Mikel Arteta, na Arsenal watembee kifua mbele