in , , , ,

Chelsea watupwa nje Ulaya

Piga nikupige kwenye mechi ngumu na kali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) katika dimba la Stamford Bridge imeisha kwa Chelsea kutupwa nje.
Ilikuwa mechi iliyovuta ushabiki mwingi, huku Chelsea na wapinzani wao, Paris Saint-Germain (PSG) wakikamiana kiasi cha mshambuliaji wa kati wa PSG, Zlatan Ibrahimovic akatolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 30.

Walikuwa ni wenyeji waliotangulia kupata bao kupitia kwa Gary Cahil dakika ya 81, lakini bao likasawazishwa dakika ya 86 na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, David Luiz.
Wakiwa na bahati ya kuwa na mchezaji mmoja wa ziada, mechi iliingia muda wa ziada, na Chelsea walipewa nafasi kubwa ya kushinda, hasa pale walipopata penati dakika ya 96 iliyotumbukizwa wavuni na Eden Hazard.

Jose Mourinho, haamini anachokiona uwanjani..
Jose Mourinho, haamini anachokiona uwanjani..

Hata hivyo, PSG hawakukata tamaa, wakapambana hadi mwisho na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 114 kupitia kwa Nahodha Thiago Silva.
Kwa kuwa kwenye mechi ya kwanza timu hizo zilitoka 1-1 nchini Ufaransa, matokeo ya 2-2 nchini England yaliwapa faida PSG kwa sababu ya bao la ugenini, hivyo Chelsea wakatupwa nje.

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alisema kwamba vijana wake hawakuweza kukabiliana na hali halisi kisaikolojia uwanjani licha ya kuwazidi PSG mchezaji, kwani shinikizo lilikuwa kwao.
Chelsea wameumizwa na mchango wa mchezaji wao wa zamani, Luiz, ambaye Mourinho alimuuza kwa pauni milioni 40, licha ya kuwa ndiye aliyewasaidia The Blues kutwaa ubingwa wa UCL na pia wa Ligi ya Europa.

Wakati Luiz mara kadhaa alionekana akitunishiana misuli na Diego Costa kiasi cha wote kulambwa kadi za njano, Ibrahimovic alitolewa nje kwa mchezo mbaya dhidi ya Oscar.
Penati ya Chelsea ilipatikana kutokana na Silva kushika mpira wa juu wakati akiokoa, lakini kwa kurekebisha makosa yake na kufunga, aliibuka shujaa. Huyu ni nahodha wa Timu ya Taifa ya Brazil pia.

Costa, alikuwa na bahati ya kuendelea kuwa uwanjani....
Costa, alikuwa na bahati ya kuendelea kuwa uwanjani….

Kocha wa PSG, Laurent Blanc alikuwa mtulivu muda wote wa mchezo tofauti na Jose Mourinho aliyeonekana kuhamaki muda mwingi na wakati mwingine kulalamikia uamuzi.
Katika mechi nyingine, Bayern Munich waliwafunga Shaktar Donetsk mabao 7-0 wakati mechi za awali Porto waliwafunga Basel 4-0 wakati Real Madrid licha ya kufuzu walifungwa 4-3 na Schalke.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Falcao hali ngumu

KAMATI YA BUNGE YA UKIMWI NA MADAWA YA KULEVYA YATEMBELEA MAKAO PSPF, WAFURAHISHWA NA MAFANIKIO YALIYOFIKIWA