in , , ,

Chelsea wapewa Falcao

*Sterling atakiwa Bayern, Stamford Bridge, Man City

*Mourinho ataka kuwatupia virago Quadrado, Oscar

Baada ya mshambuliaji wa kati wa Colombia, Radamel Falcao kushindwa kutamba na Manchester United sasa Monaco wamewaambia mabingwa wa England, Chelsea wanaweza kumchukua mchezaji huyo.

Falcao anakamilisha mkopo wake wa mwaka mmoja Old Trafford, lakini hajawasaidia chochote zaidi ya kuchuma kitita cha fedha. Alipotolewa kwenye mechi dhidi ya Arsenal majuzi, alipungia washabiki katika namna inayoonesha ataondoka.

Jumanne hii, Falcao aliweka katika mtandao wa Twitter picha yake akiwa Old Trafford akiwashukuru washabiki wa United, akisema msimu huu alipata uzoefu ambao hatakaa ausahau.

Chelsea wanatafakari la kufanya kwenye ushambuliaji, ikiwa kuna haja ya kusajili mchezaji mwingine, kwa sababu pia hawajaamua iwapo Didier Drogba atabaki kama mchezaji, ataondoka au atabaki kwenye benchi la ufundi.

Drogba ni chaguo la pili kwenye ushambuliaji wa kati baada ya Diego Costa ambaye amekuwa akisumbuliwa na misuli ya paja na ana tabia ya hasira, vitu vinavyoweza kumkoshesha mechi kadhaa. Bodi ya Wakurugenzi ya Chelsea itakutana hivi karibuni kutoa uamuzi.

Licha ya Falcao kufunga mabao manne tu msimu mzima, Chelsea wanamfikiria, na wanaona kwamba kocha Jose Mourinho anaweza kumtengeneza akafaa na kufunga mabao mengi. Monaco wanamkwepa ili kuepuka gharama kubwa za mishahara.

Wakala wa Falcao ni Mreno Jorge Mendes — mwenye uraia sawa na wa Mourinho na ambaye pia ni wakala wa kocha huyo. United walikuwa na mazungumzo na Monaco Aprili juu ya kuhuisha mkataba wake lakini mazungumzo hayo yanadaiwa kuvunjika.

Japokuwa Monaco ndio walioanzisha mazungumzo kwa ajili ya Falcao kuingia kwenye kikosi cha Louis Van Gaal mwaka jana na kuwafurahisha Man U, haielekei kwamba Old Trafford watamnunua, kwani ni bei ghali na hachezi vyema.

Monaco wakiwa wanatafuta klabu ya kumchukua ili wamlipe mshahara wake wa pauni 200,000 kwa wiki, wanawaangalia Chelsea – matajiri wa London wachukue nafasi hiyo. Chelsea hawana mchezaji wa kikosi cha kwanza anayelipwa kiasi hicho kwa wiki, hivyo labda itabidi Falcao akubali mshahara kupunguzwa.

Itakuwa ngumu kwake kukubali, kwani kwao Monaco bado anao mkataba ambao unawataka Monaco au timu anakopelekwa kwa mkopo wamlipe kiasi hicho cha fedha. Eden Hazard aliyesaini mkataba mpya wa miaka mitano hafikii pauni 200,000 kwa wiki.

Klabu za Manchester City na Bayern Munich zimeonesha nia ya kumchukua mshambuliaji wa Liverpool, Raheem Sterling, 20, aliyekataa mkataba mpya na kusema anataka kuondoka Anfield.

Man City wapo tayari kutoa pauni milioni 40 kumnasa mchezaji huyo wa England, na pia wanapanga kumpa ofa ya mshahara wa hadi pauni200,000 kwa mwezi, wakati Liverpool walimpa wa pauni 90,000 kwa wiki asaini mkataba mpua akakataa.

Bayern hawajatoa ofa, ila wanasema watamfikiria iwapo atatoa uamuzi wa kuachana na Liverpool. Anatarajiwa kukutana na kocha Brendan Rodgers na Ofisa Mtendaji Mkuu, Ian Iyre Ijumaa hii.

Chelsea nao wamejiingiza kwenye vita hiyo, wakisema wapo tayari kumuuza winga waliyemnunua msimu huu, Juan Cuadrado, 26, na kiungo mshambuliaji,Oscar, 23, ili wapate fedha za kushindana kutoa ofa kumnasa Sterling.

Kipa wa Chelsea, Petr Cech, 32, anaweza kuwa mbadala wa David De Gea iwapo Mhispania huyo ataamua kuondoka kwenda Real Madrid anakotakiwa kuchukua nafasi ya Iker Casillas.

Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Marcel Desailly anasema Cech anatakiwa kuondoka kwenye klabu hiyo ya London kwa sababu amebakisha miaka miwili tu ya kucheza soka.

Wakala wa Cech anasema kwamba mteja wake angependa kujiunga na ama Arsenal, Manchester United au Paris St-Germain. United are wanafikiria kumsajili kipa wa Ajax na Uholanzi, Jesper Cillessen, 26, kuziba pengo tarajiwa la De Gea.

Aston Villa wanaandaa pauni milioni 15 kumsajili mshambuliaji wa Queens Park Rangers, Charlie Austin, 25, anayetakiwa pia na Liverpool na Chelsea.

Kiungo mkabaji wa Leicester, Esteban Cambiasso, 34, anafikiria kuongeza mkataba wake hapo baada ya kutajwa kuwa mchezaji bora wa klabu hiyo kwa mwaka huu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

HAMILTON NA MKATABA

Taifa Stars fedheha