in , ,

HAMILTON NA MKATABA

WA PAUNI MILIONI 100

Dereva wa magari ya mbio za langalanga ya Formular One, Lewis Hamilton ameingia katika hatua ya kipekee, baada ya kusaini mkataba mpya na timu ya Mercedes AMG ukiwa na thamani ya pauni milioni 100.

Hamilton (30) ambaye mkataba wake ulikuwa ukimalizika mwisho wa msimu huu ameanguka wino kubaki na klabu hiyo kwa miaka mitatu ijayo na kwa malipo hayo, ndiye mwanamichezo anayelipwa zaidi ya wote Uingereza.

Hamilton anaishi Monaco, ambako kuna unafuu mkubwa wa kodi na pia watu wengi wa ng’ambo hupenda kuhifadhi humo fedha zao kwani hakuna kufuatwafuatwa ili mamlaka zijue alikozipata mwekaji wala kudaiwa kodi nyingi.

Kwa mujibu wa mkataba mpya, Hamilton atakuwa akipata pauni 91,575 kwa siku, ambapo kwa wiki ni £641,026 na kwa mwaka £33,333,333. Kadhalika katika kila mashindano atalipwa £1,571,429.

Hamilton alizaliwa Januari 7, 1985 Stevenage, Hertfordshire, England na akiwa na umri wa miaka 10 tu alimfuata kiongozi wa timu ya McLaren, Ron Dennis wakati wa Tuzo za Autosport na kumwambia angependa kushiriki mbio za magari.

Miaka mitatu tu baada ya hapo, Hamilton alisajiliwa na McLaren na Mercedes-Benz katika ‘Young Driver Support Programme’, akaja kushinda British Formula Renault, Formula Three Euroseries na kisha GP2 akaanza kupanda chati.

Alikuwa dereva wa timu ya McLaren 2007 na miaka 12 tangu alipokutana na Dennis alianza ushiriki wa Formula One, akiwa dereva mdogo zaidi kwenye programu yao aliyepatiwa mkataba rasmi.

Baba yake ana asili ya Afrika wakati mamaye ni Mzungu, hivyo hurejewa kama dereva wa kwanza mweusi wa Formula One. Wazazi wa baba yake walihamia Uingereza kutoka Grenada miaka ya ’50. Wazazi wa Hamilton walitengana akiwa na umri wa miaka miwili tu, hivyo akalelewa na mama yake na dada wa kufikia.

Hamilton alinukuliwa akisema kwamba angependa kuishi Uswisi au nchi nyingine isiyo na usumbufu wa waandishi, ambapo akiwa nchini Uingereza wabunge wamepata kuhoji juu ya kodi anazolipa, ikielezwa kwamba anakwepa na kuikosesha serikali mamilioni ya pauni.

Kuhusu maisha binafsi, amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii Nicole Scherzinger, mwimbaji kiongozi wa bendi ya Kimarekani ya Pussycat Dolls tangu 2007, lakini 2010 ilitangazwa walitengana ili kila mmoja ajikite kwenye kazi yake.

Hata hivyo, walionekana wakiwa pamoja 2010 kwenye Turkish Grand Prix na Canadian Grand Prix jijini Montreal Juni mwaka huo huo. Kati ya 2011 na 2014 wamerudiana na kutengana mara kadhaa, kabla ya kuonekana tena pamoja Novemba 2013. Walitengana tena Februari mwaka huu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

England U-21 hawa hapa

Chelsea wapewa Falcao