in , , ,

Chelsea wajivurugia ndoto

Jose Mourinho hajaamini jinsi vijana wake walivyocheza na kushindwa kuwafunga Norwich ambao wanaelekea kushuka daraja wakiwa katika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi.

Tena wakicheza nyumbani, Chelsea walishindwa kabisa kupenya ukuta wa Norwich, timu ambayo imekuwa na kawaida ya kufungwa mabao mengi msimu huu, na Mourinho analaani jinsi walivyoshindwa kumaliza kazi kipindi cha kwanza.

Suluhu hiyo ina maana kwamba Chelsea sasa watategemea Manchester City na Liverpool wanaoongoza ligi wapoteze mechi zao. Liverpool wakishinda mechi ya Jumatatu hii tu tayari watakuwa wamewapotezea Chelsea, kwa sababu baada ya mechi ya Jumapili Chelsea wamefikisha pointi 79 huku Man City na Liver wakiwa na pointi 80. City wana faida ya mabao tisa ya kufunga zaidi ya Liverpool.

Katika mechi ya awali Jumapili hii, Arsenal walijihakikishia tena kwa msimu wa 17 mfululizo kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwafunga West Bromwich Albion kwa bao 1-0 kupitia kwa Mfaransa Olivier Giroud anayeongoza kwa kucheza mechi nyingi Arsenal msimu huu.

Arsene Wenger amekatisha matumaini ya wapinzani wake wakubwa, Everton na Tottenham Hotspur waliokuwa wakiwania nafasi ya nne na sasa watapigania kucheza Ligi ya Europa.

Kwenye eneo la kushuka daraja, baada ya Cardiff na Fulham kuangushwa Jumamosi, timu moja zaidi inatakiwa, nazo ni katyi ya West Brom wanaohitaji pointi moja katika mechi zao mbili dhidi ya Sunderland na Stoke.

Timu nyingine iliyo kwenye mkondo wa kushuka daraja ni Sunderland ambao watakiepuka kikombe hicho iwapo watapata pointi tatu kwenye mechi zao mbili dhidi ya West Brom na Swansea. Norwich wapo hatarini zaidi na watabaki ligi kuu iwapo watawafunga Arsenal kwenye mechi ya mwisho wikiendi hii lakini pia waombe Sunderland apoteze mechi zake mbili zilizobaki.

Manchester United msimu huu ni wazee wa hapa hapa England, kwa sababu hawawezi kufuzu hata kucheza Ligi ya Europa na sasa wanasubiri wapate kocha mpya wajipange upya kwa msimu ujao.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Man City washindwe wenyewe

Liverpool wavurunda