in , ,

BALEKE KUMNG’OA DUBE?

Moja ya habari ambayo imekuwa ikizungumzwa sana na vyombo vingi vya habari pamoja na mashabiki wa klabu ya Yanga ni kiwango cha mshambuliaji wa Yanga, Prince Dube.

Prince Dube kwa mechi za hivi karibuni amekuwa akikosa nafasi nyingi za kufunga ambazo zinaonekana za wazi kwenye michezo mbalimbali ambayo amekuwa akianza.

Kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba , Prince Dube alikosa nafasi zaidi ya nne kwenye mchezo huo.

Pia kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CBE ya Ethiopia uliochezwa Ethiopia, Prince Dube licha ya kufunga goli lililowapa ushindi Yanga, lakini alikosa nafasi nyingi za wazi kwenye mchezo huo.

Hali hii ya kukosa nafasi nyingi zimeongeza presha kubwa nje ya uwanja kwa sababu watu wengi walitazamia Prince Dube kuwa ni tiba kwenye klabu ya Yanga baada ya kuondokewa na mshambuliaji wao bora Fiston Mayele.

Presha hii inaonekana kuwaingia pia benchi la ufundi la klabu Yanga ambapo kwenye mazoezi ya klabu ya Yanga yaliyofanyika usiku wa Alhamisi, ilionekana Jean Baleke akiwa anafanya mazoezi maalumu ya jinsi ya kufunga.

Jean Baleke ambaye alikuwa na mwalimu maalumu ambaye alikuwa anamfanyisha mazoezi peke yake namna ya kufunga huku wachezaji wengine wakiwa wanafanya mazoezi pamoja.

Mazoezi haya maalumu yanaweza kuwa ni dalili kwa Yanga kuanza kumtengeneza Jean Baleke kama mtu ambaye atamweka benchi Prince Dube kwenye mechi mbalimbali zijazo.

Ikumbukwe Prince Dube msimu huu kacheza mechi sita za mashindano na katika mechi hizo sita amefunga magoli manne na kutoa pasi moja ya mwisho ya goli.

Pamoja na kiwango hicho bora bado mashabiki wa klabu ya Yanga wanaonesha kutoridhishwa naye hasa anapokosa nafasi nyingi za wazi za magoli.

Baada ya mazoezi maalumu ya Baleke, swali linabaki, je Jean Baleke anaenda kumng’oa Prince Dube kwenye eneo la ushambuliaji ya Yanga ?

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

“Simba lazima ishinde”-Ahmed Ally