in , , ,

ARSENAL UBINGWA WAO UPO KWENYE MECHI ZA KIUME

DAKIKA 83 wakati nahodha wa Arsenal Martin Odegaard alipokuwa anatolewa dimbani, kamera za Televisheni zilionesha mchezaji anayeingia ni kinda Ethan Nwaneri, hapo hapo akili ya haraka inakuambia kuna goli lake linakuja katika muda mfupi. Kwenye mchezo huo Arsenal walikuwa washindi wa karibu Kila kitu na kumaliza mchezo kwa kucheza kiume ingawa ubingwa wao upo mbali. Hata hivyo yapo mambo ayanayowaangusha Manchester City kwa kiasi kikubwa na kuifanya timu yao kuwa nyepesi mbele ya vijana wa Mikel Arteta. TANZANIA SPORTS inakuletea masuala muhimu yaliyojitokeza katika mchezo huo ambao Manchester City wamekumbana na kipigo kikali cha mabao 5-1. 

VIJANA WA PEP GUARDIOLA WANA MAKOSA MENGI

Manchester City wana makosa mengi dimbani. Timu yao inayumba eneo la kiungo ushambuliaji na ulinzi hivyo safi ya ulinzi kukumbana na mzigo mzito. Bao la kwanza lilipatikana sababu ya makosa hayo. Bao la pili lilionesha Ukubwa wa makosa ya Man City kwa sababu viungo walipoteza mpira katika mazingira mepesi mno. Badala ya kutoa pasi mchezaji anajikuta anapoteza nafasi ya kulinda mpira. Kosa hili lilikuwa na maana Man City walipoteana katika kiungo wa ushambuliaji ambao walikuwa na jukumu la kutengeneza mashambulizi. Hata hivyo makosa yao yaliwapa nafasi Arsenal kujipanga vyema. Kombinenga matata ya Thomas Partey, Skelly, na Rice iliwafanya viungo wa Man City wawe wanarudishwa nyuma mara kwa mara. 

MAN CITY WAMEISHIWA GRISI

Katikati ya dimba Man City walizoeleka kutawala mchezo, wangefanya chochote wanachojisikia kwa pasi za rula za kuwafikia walengwa. Lakini katika mchezo wao dhidi ya Arsenal eneo la Ubunifu umedorora na wamepoteza kiunganishi toka eneo la ulinzi kwenda ushambuliaji. Kwa mechi kadhaa sasa Erlin Haaland amekuwa alicheza kama mshambuliaji pekee hali ambayo inawapa nafasi wapinzani wao kuwashambulia. Si Bernando Silva wala Phil Foden ambao wangeweza kulainisha majukumu ya Man City kupata ushindi. Grisi ya kulainisha na kuibuka na ushindi. Timu ikikosa ubora katika kiungo inakuwa dhaifu. Declan Rice alitumia muda mwingi katikati kushoto, kisha Skelly katikati-mbele kushoto. Hivyo viungo wawili wa Arsenal walikuwa wanaliandamana eneo la beki wa kulia, Kisha Thomas Partey akawa anacheza katikati-mbele akielekea upande wa kulia ambako nyuma ya mstari wa 18 walikuwa Martin Odegaard na Havertz . Kimahesabu eneo la winga wa kushoto lilikuwa na wachezaji watatu wa Arsenal; Rice, Skelly na Trossand. Ni sababu hii Martinelli alionekana mara nyingi eneo la ushambuliaji kuliko winga. 

WASHTUKIZE, HAWANA KASI 

Mojawapo ya mabadiliko yaliyofanyika kipindi cha pili kwa Arsenal ni kuongeza vitu viwili; Kasi na mashambulizi ya kushtukiza. Kama wangecheza shambulizi la kushtukiza basi upande wao wa kulia ulikuwa na Kasi zaidi ambako Havertz alikuwa anazurura huko. Wakati Havertz alikuwa anazurura huko, Maertinelli aliingia eneo la namba 9 kwa urahisi, huku wachezaji wenzake watatu wakifuata nyuma. Ile Kasi ya kushambuliwa iliwaathiri Man City kwani hawakuwa na mpango mbadala pale walipotakiwa kukabiliana na timu hiyo. 

Tanzania Sports

PEP GUARDIOLA HANA SILAHA YA MWISHO

Katika falsafa yake ya ufundishaji amekuwa akijinyima mtu wa mwisho kumaliza mchezo. Akiwa Barcelona kazi yake ilorahisishwa na wachezaji watatu; Andres Iniesta, Xavu Hernandez, na Lionel Messi. Lakini alipoenda Bayern Munich akaifanya falsafa yake ifanye kazi kuliko wachezaji binafsi. Timu zake zinakosa wachezaji wa kuamua matokeo au wale tegemeo la mwisho. Kwa mfano, baadhi ya wachezaji wanatumika kama silaha ya mwisho. Hii silaha ya mwisho ni mchezaji ambaye anabeba majukumu na kuamua matokeo. Timu inapoingia kwenye hatari na kuhitaji matokeo au kupindua meza wanajikuta hawana mchezaji wa aina hiyo. Ni sababu hii timu ya Pep Guardiola inapozidiwa inakosa mbinu mbadala za uchezaji binafsi. Hana watu wa kumaliza mechi, alishikwa falsafa yake unakuwa mwisho wa mchezo. 

ARSENAL WANATAKA UBINGWA BILA JASHO?

Nwaneri, Martinelli, Skelly, Rice, Saliba ni aina ya wachezaji wenye vipaji na wanaohitaji msaada Kila wakati. Arsenal wameifunga Man City wakiwa wanautaka mchezo, waliutafuta mpira, walitafuta matokeo na zaidi walitaka kulipiza kisasi cha kunyanyaswa katika misimu kadhaa sasa. Lakini timu hii inaweza kucheza vizuri mchezo huu kisha inakwenda kuboronga dhidi ya ndogo au kufungwa katika michezo isiyotarajiwa. Ukitazama mabao matamu ya Ethan Nwaneri, Partey na Havertz lazima utajiuliza yalikuwa wapi hayo tangu mwanzo wa msimu? Yalikuwa wapi magoli mazuri kama hayo tangu mwanzo? Ni kama vile Arsenal wanautaka ubingwa bila jasho. 

MAN CITY WANAKATIKA MNO

Tanzania Sports

Jinsi wanavyojipanga unaweza kudhani watacheza kiufundi kama walivyozoeleka. Lakini wakinyang’angwa mpira unaona wazi Man City wanayumba mno katika kuzuia mtu na mtu au nafasi. Wanapoteza mipira katika mazingira ya ajabu kidogo. Umakini umeshuka mno na ari yao katika mapambano inaonekana kuwa ya kiwango cha chini. Kama Arsenal wangekuwa kiwanjani na mshambuliaji kamili Kariba ya Thierry Henry basi wangeweza kuibuka na ushindi mno zaidi ya hayo mabao matano. Udhaifu wa timu kupoteza muunganiko ambao ilisababisha vipande vingi vya Man City, ilihitajika kuwa na mshambuliaji mwenye uwezo wa kupachika hata mabao matatu ndani ya mchezo mmoja. Hilo ndilo alilokosa Mikel Arteta. 

WALINZI WAFUNGAJI

Beki wa kushoto wa Man City anapangwa kuingia eneo la hatari kuliko kawaida. Ni sababu hiyo Gvadiol amekuwa akifunga mabao mengi katika siku za hivi karibuni. Hasara yake ni kwamba endapo upande wake ikipingwa ‘Counter attacks” hawezi kurudi haraka, hivyo mzigo unaenda Kwa mabeki wa kati ambao nao wanajikuta wanaachia nafasi eneo lao na hivyo viungo wanaporudi kuja kuziba nafasi wanakuwa wamechelewa. Ushahidi wa kuyumba eneo la ulinzi sababu ya walinzi kwenda kushambulia zaidi ni pale ambapo Thomas Partey alipata mwanya wa kuachia shuti kali lililombabatiza John Stones kabla ya kutinga wavuni. Katika mazingira yale John Stones alibaki peke yake huku Akanji akiwa na jukumu la kuzuia upande kati-kushoto. Hivyo viungo wa City hawakurudi kuziba eneo hilo na kujikuta wakizabwa bao la pili. 

MAWINGA WATAMU 

Savinho ni winga mzuri wa Man City sawa na Martinelli Kwa upande wa Arsenal. Katika uchezaji wake Savinho alipika bao la kusawazisha baada ya kuachia krosi maridadi iliyotua kwenye kichwa cha Erlin Haaland ambaye aakapachika bao hilo. Savinho anaweza kuwa silaha nzuri ya Man City pale ambapo Pep Guardiola atapunguza kumbana katika mfumo. Ni winga ambao akipewa uhuru wa kuonesha zaidi kipaji chake anaweza kuleta matunda mazuri Etihad Stadium.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

55 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

WYDAD CASABLANCA NA HESHIMA LIGI KUU TANZANIA

Tanzania Sports

Wingu zito kwa Real Madrid