in , , , ,

Wingu zito kwa Real Madrid

LIGI ya mabingwa Ulaya inarejea katika hatua ya mtoano ambapo bingwa mtetezi Real Madrid atakuwa mgeni wa Manchester City kwenye dimba la Etihad jijini Manchester. Wakati washabiki wakisubiri mechi hiyo kuna matukio ambayo yanaifanya kutawaliwa na wingu zito.  Kuanzia benchi la ufundi, wachezaji na amshabiki wanakabiliwa na kibarua kigumu cha kubashiri nani ataibuka mbabe katika mchezo huo. Timu hizi zinakutana baada ya kushindw akufuzu hatua ya 16 hivyo zitapaswa kuchuana ili kupata nafasi ya kuungana na zingine zilizofuzu. TANZANIASPORTS kwa kuzingatia uzito wa mchezo huo inakuletea masuala muhimu ambayo yanasababisha kuwa gumzo.

Vichapo vikali wikiendi

Manchester City walikumbana na kipigo kikali kutoka kwa Arsenal. Kufungwa mabao 5-1 kumeibua mjadala ikiwa timu hiyo inaweza kukabiliana na bingwa mtetezi Real Madrid. Kikosi cha Pep Guardiola kilionekana dhahiri shihiri kuyumba baada ya kuruhusu mabao matano kutinga katika lango lake. Wakati Manchester City wakilazwa idadi hiyo, wapinzani wake Real Madrid nao wlaikutambana na kipigo cha 1-0 kutoka kwa Espanyol katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Hispania. Kipigo hicho pia kilipunguza pengo la pointi kati ya Real Madrid na washindani wake wa karibu Atletico Madrid wakiwa nyuma kwa pointi moja. Kwahiyo timu zote mbili zitakutana wiki ijayo zikiwa zinatoka kwenye maumivu makali ya kufungwa.

Vichwa vinauma kwa Makocha

Timu inapofungwa wanaolaumiwa ni wachezaji na makocha wao. Mara nyingi makocha ndiyo wanabeba jukumu la kushindwa kwa timu na baadhi yao wanakwenda mbali zaidi kwa kusema lawama za kufungwa wabebeshwe wao kwani ndiyo wanaamua nani aanze kikosi cha kwanza. Pep Guardiola atakuwa na kibarua za kuwarudishia kujiamini wachezaji wake pamoja na kuwakumbusha namna bora ya kucheza dhidi ya Real Madrid. Kwa upande wake Carlo Ancelotti atakuwa na kazi ya kuhakikisha safu yake ya ushambuliaji inafanya kazi nzito na kuendeleza maumivu makali kwa Man City. Suala la mbinu gani zitakazotumika kuokoa msimu wao ndilo mjadala mkubwa. Kila timu inapopangwa wachezaji wanapoteana na kujikuta wakifungwa kama ilivyotokea wikiendi iliyopita kwa kuwaruhusu Arsenal kupata mabao matano ndani ya dakika tisini. Nao Real Madrid watakuwa wanatafuta jawabu kwanini hawakuweza kupachika bao lolote katika mchezo wao dhidi ya Espanyol.

Wingu la majeruhi

Carlo Ancelotti ataingia kwenye mchezo dhidi ya Manchester City akiwa amewakosa wachezaji wake muhimu katika safu ya ulinzi. Antoni Rudiger, Eder Militao na David Alaba watakosekana katika mchezo dhidi ya Man City. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Real Madrid imesema beki wa kati Antonio Rudiger atakaa nje kwa siku 20 ikiwa na maana ataukosa mchezo wa kwanza dhidi ya Man City kwenye dimba la Etihad. Eder Militao na David Alaba hawatarajiwi kurudi haraka kwahiyo hawatakuwa kwenye mechi zote mbili. 

Matumaini ya Carlo Ancelotti yatakuwa kwa kiungo mkabaji, Aurelien Tchouameni na kinda Raul Asensio kucheza kama mabeki wa kati. Jukumu la mabeki hao litakuwa kumdhibiti Erlin Haaland na wenzake ili wasilete madhara katika lango la Real Madrid. Kibarua hiki ni kigumu kwa wachezaji hao wawili kwani Tchouameni anafahamika kama mchezaji wa nafasi ya kiungo lakini mara kadhaa ametumikia nafasi ya beki namba nne akimsaidia Antonio Rudiger. 

Vilevile Raul Asensio ni kinda ambaye amepandishwa kutoka Castilla hivyo uzoefu wake kwenye mashindano hayo ni hafifu. Kabla ya kuwavaa Man City, kikosi cha Carlo Ancelotti kitakuwa na kibarua kigumu katika mchezo dhidi ya Atletico Madrid wiki hii ambao utaamua nani kinara wa La Liga. Matatizo ya Real Madrid huenda yakatumiwa vyema na wapinzani wao kuanzia Atletico Madrid hadi Man City kwani watakuwa hawako imara katika safu ya ulinzi. 

‘Kikosi ungaunga’ kuwapa ushindi?

Sio siri Man City wanautaka ushindi kwenye mchezo huo kama kulipiza kisasi cha kutolew amsimu uliopita. Hali kadhalika Real Madrid watataka ushindi kudhihirisha kuwa wao ni miamba ya soka barani Ulaya kisha kufuzu hatua nyingine. Hata hivyo kutokana na timu hizo kufungwa katika mechi zao za mwishoni mwa wiki iliyopita ni dhahiri zitataka kurekebisha makosa yao. Real Madrid wataingia dimbani Etihad wakiwa na kikosi kidogo mno kwani sehemu tatu kiwanjani watakuwa wameunga unga kwa lugha ya vijana wa mjini. 

Beki wa kulia amekuwa akipangwa Lucas Vazquez ambaye kwa asili ni winga. Kwahiyo atakuwa na kibarua kigumu kukabiliana na mawinga wawili Savinho na Marmoushi wa Man City. Katika safu ya ulinzi namba tano na nne wachezaji wawili watakaopangwa itakuwa sawa na kuunga unga tu kwani Tchouameni na Asensio ni wachezaji abao wanahitaji kulindwa ili waoneshe viwango vyao. Katika mazingira hayo Real Madrid wataingiza kikosi kilichounga ungwa tu bila kukamilika, huku Man City nao watakabiliana na hofu dhidi ya matokeo mabaya wanayopata katika michezo mbalimbali. Je nani atafuzu kati ya Real Madrid na Manchester City? Jawabu litapatikana Etihad na Santiago Bernabeu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

50 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

ARSENAL UBINGWA WAO UPO KWENYE MECHI ZA KIUME

Tanzania Sports

Marco Asensio na vita ya kuokoa kipaji chake