in , , , ,

Arsenal moto mkali

*Welbeck apiga 3 Galatasaray wakilala 4-1
*Liverpool wafungwa Uswisi, Madrid safi

Arsenal wamempa zawadi kubwa kocha wao Arsene Wenger alipotimiza miaka 18 klabuni hapo kwa kuwanyuka Galatasaray mabao 4-1.

Katika mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) iliyopigwa nyumbani kwa Arsenal – Emirates, mchezaji mpya Danny Welbeck alipachika mabao matatu, ikiwa ni mara ya kwanza kupiga hat trick tangu aingie soka ya wakubwa.

Mwingereza huyo alikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu, akicheza kwa ushirikiano mkubwa na Alexis Sanchez aliyefunga bao moja, Mesut Ozil na Alex Oxlade-Chamberlain, ambapo Welbeck alicheza kama mshambuliaji wa kati, nafasi anayoipenda.

Hata hivyo Arsenal walipata pigo kwa kipa wao namba moja, Wojciech Szczesny kupewa kadi nyekundu ikiwa imebaki zaidi ya nusu saa, alipomwangusha chini mshambuliaji Burak Yilmaz, hivyo Arsenal wakacheza wakiwa pungufu kwa muda huo.

Yilmaz ndiye alifunga bao la kufutia machozi kwa penati yake, huku kipa mpya wa Colombia, David Ospina akichukua mahali pa Szczesny. Huu ni ushindi wa kwanza kwa Arsenal kwenye mashindano ya UCL mwaka huu, kwani walipoteza mechi ya kwanza kwa 0-2 dhidi ya Borussia Dortmund katika mechi ya Kundi D.

Galatasaray wanafundishwa na kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Italia, Cesare Prandelli, wakaanza na mabeki watatu lakini mambo yalipokuwa mazito wakaongeza wa nne kutoka mbele lakini haikusaidia.

Katika mechi nyingine ya kundi hilo, Dortmund waliwakandika Anderlecht mabao 3-0 na kujiimarisha kileleni kwa kufikisha pointi sita, Arsenal ni wa pili kwa pointi tatu, wakifuatiwa na Anderlecht na Galatasaray.
 
LIVERPOOL HOI NCHINI USWISI
sg

Liverpool wameendelea na soka mbovu waliyoanza nayo msimu huu, pale walipofungwa na Basel ya Uswisi bao 1-0 katika mechi iliyomwacha kocha Brendan Rodgers akijiuliza afanye nini, kwani maisha bila Luis Suarez yanaonekana kuwa magumu.

Liverpool wameshinda mechi nne tu kati ya tisa walizocheza msimu huu kwenye mashindano yote na usiku wa Jumatano hii hawakuonekana tishio mbele ya Basel, washambuliaji wakishindwa kuelewana huku ukuta wao ukionekana kuvuja.

Mlinzi Martin Skrtel alicheza hovyo kwa kupiga mpira wa kichwa kuelekea kwenye lango lake, ukamgonga Dejan Lovren ukawa unaelekea wavuni, kipa Simon Mignolet akauzuia kwa mikono  ukamwendeaMarco Streller aliyeukwamisha wavuni.

 Katika mechi yao ya kwanza, Basel walifungwa 5-1 na Real Madrid na kuonekana wachovu lakini sasa wamewashangaza Liverpool. Kazi kubwa ipo kwenye mechi ijayo, ambapo Liver watacheza na Real.

MATOKEO MENGINE YA UCL

Katika mechi nyingine, Atletico Madrid waliwapiga Juventus 1-0, Malmo FF wakawatandika Olympiakos 2-0, Ludo Razgd wakalala 1-2 kwa Real Madrid na kuwaacha vijana wa Carlo Ancelotti wakitamba kileleni mwa kundi lao kwa pointi sita kutoka mechi mbili.

Kwingineko Zenit St Petersburg walikwenda suluhu na Monaco huku Bayer Leverkusen wakiwasulubu Benfica 3-1.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Chelsea safi, Man City wabanwa

England yataja kikosi