in , ,

Arsenal, Chelsea roho kwatu

“Arsenal pull off their ‘greatest escape’ and leave Arsène Wenger feeling lucky”

Arsenal na Chelsea wamefanikiwa kuvuka mtihani wa kucheza hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).
Arsenal walioanza vibaya michuano hiyo kwa kufungwa mara mbili kabla ya kupata ushindi mmoja kisha wakapigwa mabao matano na Bayern Munich wanajiamini.

Wakicheza ugenini, Arsenal walifanikiwa kuwafunga Olympiakos 3-0 kupitia kwa mshambuliaji wake wa kati, Olivier Giroud na kujihakikishia kuvuka.

Walikuwa wakihitaji ushindi wa tofauti ya mabao walau mawili, na Mfaransa huyo akawapa matatu, akimfanya kocha Arsene Wenger, wachezaji wengine na washabiki kuwa roho kwatu.

Hii ni mara ya kwanza kwa Giroud kufunga hat-trick kwa klabu yake na sasa wamemaliza nafasi ya pili nyuma ya Bayern Munich.
Giroud alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 29 kutokana na kazi nzuri ya Aaron Ramsey, kisha akafunga la pili dakika nne tu baada ya mapumziko akimalizia kazi ya Joel Campbell aliyewavuka mabeki watatu, kisha akawazunguka wawili. La tatu alifunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 67 baada ya beki wa Olympiakos kuunawa mpira.

Huu ni msimu wa 16 mfululizo Arsenal wanafika hatua ya 16 bora Ulaya na ulikuwa usiku wa kukumbukwa jijini Athens, Arsenal wakionesha uzoefu wao.

Katika mechi ya mtoano, Arsenal wanaweza kupangwa na Real Madrid, Atletico Madrid, Barcelona, Wolfsburg au Zenit St Petersburg walioshika nafasi za kwanza kwenye makundi yao.

Willian, akiifungia Chelsea bao la pili.
Willian, akiifungia Chelsea bao la pili.

Katika mechi nyingine, Chelsea walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Porto nchini Ureno.
Chelsea walipata bao la kwanza baada ya mkwaju wa Diego Costa kutemwa na kipa Iker Casillas kisha kumgonga mchezaji wa Porto, Ivan Marcano na kuzama wavuni.

Porto walikuwa wakihitaji kushinda ili kufuzu, lakini kwa bao hilo na lile la Willian, ilimaanisha Wareno hao wametupwa nje.
Chelsea wameshika nafasi ya kwanza kwenye kundi lao na sasa kwenye mtoano wanaweza kupangwa na ama Paris St-Germain, Juventus, PSV Eindhoven, Benfica, Roma au KAA Gent. Arsenal na Chelsea wanaungana na Manchester City waliofuzu, huku Manchester United wakitolewa.

Katika matokeo mengine Jumatano hii Bayer Leverkusen walienda sare ya 1-1 na Barcelona, Valencia wakilala 0-2 kwa Lyon na Roma wakienda suluhu na BATE Bor.
Dinamo Zagreb walilala 0-2 kwa Bayern Munich, Dynamo Kiev wakawafunga Macabi Tel Aviv 1-0 na KAA Gent wakawashinda Zenit St Petersburg kwa 2-1.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Man United nje Ulaya

Tanzania Sports

Arsenal vinara Ligi Kuu