in , , ,

Man United nje Ulaya

*City vinara wa kundi, Ronaldo apiga nne

Kocha Louis van Gaal ameonja chungu ya kushindwa, baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).
United walilala kwa mabao 3-2, wakikikubali kichapo cha Wolfsburg nchini Ujerumani. Man U walianza vyema na kupata bao la mapema kupitia kwa Anthony Martial alipokea vyema mpira wa Juan Mata.Hata hivyo, Wolfsburg walijibu ndani ya dakika tatu tu, kupitia kwa Aparecido Rodrigues na dakika 16 baadaye Wajerumani wakatia bao la pili pale Naldo alipompatia mpira Vieirinha na kumalizia vyema.

United walidhani kwamba wamesonga mbele baada ya Josuha Guilavogui kujifunga akiwapa bao la pili na la kusawazisha, lakini dakika za lala salama zikashuhudia Naldo akifunga kwa kichwa safi na kukatisha ndoto za kufika hatua ya makundi.

United wangevuka iwapo wangewafunga Wolfsburg au kwenda sambamba na matokeo baina ya PSV Eindhoven dhidi ya CSKA Moscow. Hata hivyo, PSV waliwashinda CSKA Moscow 2-1 na kufuzu, huku United wakigharimika kwa kupoteza mechi yao.

Tofauti na United, Man City walianza taratibu mechi yao dhidi ya Borussia Monchengladbach, kwenye mechi ambayo mabao matano yalifungwa ndani ya dakika sita tu, ambapo City walitoka nyuma hadi kushinda 4-2.

Ushindi huo unamaanisha kwamba City wameshika usukani kwenye kundi lao baada ya kumalizika hatua ya makundi wakifuatiwa na Juventus. Kwa maana hiyo, vijana wa Manuel Pellegrini wataziepuka timu za Barcelona na Real Madrid kwenye hatua ya 16 bora huku United wakitarajia kutupwa kwenye Ligi ya Europa.

Mabao ya City yalifungwa na David Silva, Raheem Sterling mawili na Wilfried Bony. Pellegrini amejitapa kwamba vijana wake wakiwa wanacheza kama walivyofanya kwenye kipindi cha pili, basi wanaweza kuimudu timu yoyote.

Katika hatua nyingine, nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunga mabao manne wakati timu yake walipowakong’ota Malmo 8-0 na kuweka historia ya ushindi mnono zaidi katika hatua ya makundi UCL.

Mreno huyo alifunga mabao matatu ndani ya dakika 11, ambapo sasa amefikisha jumla ya mabao 88 UCL. Mfaransa aliyepatwa na kashfa ya kujihusisha na mikanda feki ya ngono ya Mfaransa mwenzake, Mathieu Valbuena, alifunga mabao matatu huku jingine likitiwa kimiani na Mateo Kovacic.

Matokeo haya yanakumbushia mengine kama hayo ambayo Liverpool waliwafunga Besiktas 2007, enzi hizo Rafa Benitez anayewafundisha Madrid sasa, akiwa kocha wa Liver, hivyo amejiwekea rekodi nzuri ya mafanikio.

Sijui kama anajua anachokifanya kwa United?
Sijui kama anajua anachokifanya kwa United?

Ronaldo, anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika historia ya UCL, anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao zaidi ya 10 katika hatua za makundi, ambapo amefunga mabao 11 katika mechi sita.

Katika mechi nyingine za UCL, Paris Saint-Germain (PSG) waliwapiga Shaktar Donets 2-0, Benfica wakalala 1-2 kwa Atletico Madrid, Galatasaray wakaenda sare ya 1-1 na FC Astan wakati Sevilla waliwafunga Juventus 1-0.

Leo Arsenal wanacheza na Olympiakos kwenye mechi ambayo ili wafuzu lazima washinde wka tofauti kubwa ya mabao. Bayern Leverkusen wanacheza na Barcelona, Chelsea wanawakabili Porto na Valencia wanawakaribisha Lyon.

Matokeo mengine ya CL
Matokeo mengine ya CL

Kadhalika, Roma ni wenyeji wa BATE Bor, Dinamo Zagreb wanacheza na Bayern Munich, Macabi Tel Aviv wakisafiri kukabiliana na Dynamo Kiev huku Zenit St Petersburg wakienda kucheza na KAA Gent.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

PSPF yatoa msaada wa vitanda Temeke Hosp

Tanzania Sports

Arsenal, Chelsea roho kwatu