in , , ,

Aguero awaua Bayern Munich


*Chelsea wawasasambua Schalke

Mabao matatu yaliyofungwa na Sergio Aguero yametosha kuwapa Manchester City ushindi dhidi ya mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich.
Katika mechi hiyo ngumu ya Kundi E ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) Man City walishinda 3-2, na walicheza wakiwa wamewazidi Bayern mtu mmoja kwa dakika 70, kwani Mehdi Benatia alipewa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Aguero.

Ushindani wa kufuzu kwenye kundi hilo sasa unakuwa wa aina yake kwa timu tatu zinazofungana kwa pointi tano zote, ambapo licha ya City, CSKA Moscow na Roma zote zina pointi hizo huku Bayern wakiwa na pointi 12.
Aguero alifunga mabao yake katika dakika ya 21 kwa penati, ya 85 na ya 90. CSKA Moscow walikwenda sare ya 1-1 na Roma na sasa City wamebakisha mechi dhidi ya Roma, wanayotakiwa kwa vyovyote kushinda, pia Bayern wawafunge CSKA Moscow. City wana uwiano dhaifu wa mabao kuliko wenzao.
Bayern walizinduka katika dakika ya 40 kwa Xabi Alonso kufunga kwa mpira wa adhabu ndogo kisha Robert Lewandowski kufunga kwa kicha dakika tano tu baadaye. Ilikuwa kama ndoto kwa City kushinda bila Yaya Toure anayetumikia adhabu, Fernandinho, David Silva wala Edin Dzeko.

CHELSEA WAWACHANIA MBALI SCHALKE

Chelsea waliendeleza wimbi la ushindi kwa kuwakandika Schalke mabao 5-0 nyumbani kwao, huku Jose Mourinho akikutana na kocha wa Wajerumani hao, Roberto Di Matteo aliyewapa Chelsea ubingwa wa Ulaya 2012.
Kitabu cha mabao kilifunguliwa na John Terry katika dakika ya pili tu ya mchezo na kuwavurugia siku wadau wa Wajerumani. Willian alifunga dakika ya 29 kabla ya Kiirchhoff kujifunga dakika moja kabla ya mapumziko.
Waliporudi kutoka mapumziko iliachukua muda mrefu, lakini dakika ya 76 Didier Drogba alifunga bao na dakika mbili baadaye Ramires akafunga kitabu hicho. Chelsea wamefuzu kwa hatua ya 16 bora
Di Matteo alichezea Chelsea mechi 175 kati ya 1996 na 2002, akatwaa nao Kombe la FA mara mbili kabla ya kuja kuwa kocha hapo kwa muda mfupi miaka miwili iliyopita. Kama makocha wengine wengi wa Chelsea, alifukuzwa kazi baada ya kutopata matokeo mazuri.

MESSI AWEKA REKODI MPYA

Katika mechi nyingine, Apoel Nicosia ya Cyprus walifungwa mabao 4-0 na Barcelona, ambapo Lionel Messi aliweka rekodi kwa kuwa mfungaji bora wa wakati wote katika UCL, baada ya kutupia hat-trick. Messi aliingia kwenye mechi hiyo akiwa na mabao 71, sawa na Raul huku Cristiano Ronaldo akiwa na mabao 70.
Luis Suarez ndiye alifunga bao la kwanza, likiwa ni lake la kwanza kwa klabu yake hiyo mpya. Kadi nyekundu zilitembea, mchezaji wa Barcelona, Alcántara do Nascimento akitolewa nje kwa kadi ya njano ya pili sawa na Leme Amorim kwa mchezo mbaya.
Matokeo mengine ni Paris Saint-Germain kuwafunga Ajax 3-1, Sporting Lisbon wakawapiga NK Maribor 3-1, BATE Bor wakalala nyumbani 3-0 kwa Porto huku Shakhtar Donetsk wakikubali kichapo cha 1-0 kutoka kwa Athletic Bilbao.
Timu zilizovuka tayari kwa hatua ya mtoano ni Real Madrid, Borussia Dortmund, Bayern Munich, Paris Saint-Germain, Barcelona, Chelsea, Porto na Shakhtar Donetsk.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Hamilton: Ushindi ni mwanzo mpya

Arsenal wawafyatua Dortmund