in

Yanga wanatakiwa kuionea wivu Simba!

Yanga na Simba Uwanjani

Hesabu zangu zinaniambia kuwa Simba imechukua kombe la ligi kuu kwa mara ya tatu mfululizo. Msimu huu Simba wanatafuta kikombe chao cha nne mfululizo kwenye ligi kuu Tanzania bara.

Katika misimu hiyo mitatu iliyopita Simba imefanikiwa kufika katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika. Mara ya kwanza walifika robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika na msimu huu ndiyo wameingia kwenye makundi.

Katika misimu mitatu iliyopita ndiyo timu pekee ambayo imechukua ngao ya hisani mara tatu mfululizo kuzidi timu yoyote. Ndiyo timu pekee iliyochukua kombe la shirikisho kuzidi timu zote ndani ya misimu mitatu iliyopita.

Ndani ya misimu mitatu iliyopita Simba ndiyo timu pekee ambayo ilikuwa inaingiza watazamaji wengi kwenye mechi zao za ligi kuu Tanzania (mechi zote za nyumbani na ugenini).

Msimu wa mwaka 2018/2019, msimu ambao Simba walifanikiwa kuingia kwenye hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika ndiyo ilikuwa timu ambayo ilikuwa inaingiza  mashabiki wengi kwenye uwanja wake wa nyumbani kuzidi timu zote.

Hamasa ilikuwa kubwa, na ndani ya misimu mitatu iliyopita Simba imekuwa na hamasa kubwa sana ndani na nje ya uwanja. Ndani ya uwanja wachezaji walikuwa na hamasa kubwa sana kutokana na posho, mishahara mizuri na mazingira mazuri ya kambi.

Ndani ya misimu mitatu iliyopita Simba imekuwa timu ambayo nje ya uwanja mashabiki wake wana hamasa kubwa. Hamasa ambayo iliwafanya Simba kuingiza watu wengi ndani ya uwanja.

Hamasa ambayo iliifanya Simba kuwa ndiyo timu yenye wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamiii. Wiki iliyopita Simba imefanikiwa kuwa na jumla ya wafuasi milioni mbili katika mtandao wa Instagram pekee wakati Yanga wakiwa na wafuasi laki tisa kwenye mtandao wa Instagram.

Simba kwenye mtandao wa kijamiii wa YouTube ina wafuasi laki moja na elfu sabini wakati Yanga kwenye mtandao huo wa kijamiii wa Instagram una wafuasi elfu sabini.

Simba kwa kiasi kikubwa imewazidi Yanga kwenye sehemu nyingi ndani ya miaka mitatu iliyopita. Yanga wanatakiwa kuwaonea wivu Simba na siyo kukalia kuanzisha mada ya uchawi wa kutumia paka nyeusi. Wafikirie namna ambavyo wanaweza kuyafikia mafanikio ya Simba. Simba kwa sasa iko nafasi ya 13 katika orodha ya vilabu bora Afrika wakati Yanga haipo hata 30 bora.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Waamuzi wa Tanzania

Marefa wa Tanzania ni mizigo?

michael sarpong

Yanga wampe muda Michael Sarpong