Dirisha la usajili ligi kuu Tanzania Bara limefungwa Yanga, Simba na Azam FC zimesajili wachezaji wenye ubora mkubwa wa kushindania taji la ligi hiyo itakayoanza Septemba sita.
Wakati huo huo nyota Juma Abdul na Kelvin Yondani wamekosa timu kipindi hiki cha dirishala usajili kufungwa.
Bado wanayonafasi endapo timu inawahitaji kwani FIFA inaruhusu mchezaji kusajiliwa hata kama usajili umefungwa, lakini asiwe na mkataba na timu nyingine, vigezo hivi nyota hawa wanavyo.
Timu za Simba, Yanga na Azam FC wamesajili wachezaji nyota ambao watatoa ushindani wa hali ya juu msimu huu ukitaka kuamini hayo angalia usajili wao.
Simba SC
Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Simba SC walifanya usajili wa nyota kadhaa kwa ajiri ya kuongeza nguvu kikosi chao ambacho kitashiriki ligi ya mabingwa barani Afrika.
Walimsajili Larry Bwalya kutoka Zambia, Joash Onyango kutoka Gor Mahia ya Kenya, Duchu, Ame Ibrahim na Benard Morrison.
Usajili wao umelenga kuziba zile nafasi ambazo zilionekana haziko vizuri huku wakiwaacha baadhi ya nyota wake kama vile Shiboub, Deo Kanda na Tairone Da Silva.
Je watatetea ubingwa wao msimu huu ambao una timu kali ambazo zimejipanga pia, tusubiri tuone hadi mwisho.
YANGA
Yanga ambayo imeacha nyota 16 katika kikosi kilichoshiriki msimu uliopita nayo imefanya usajili wa kisayansi ili kuweza kurudi katika hali yao ya kawaida.
Hadi dirisha la usajili linafungwa Yanga wamesajili wachezaji 26 huku ikiwa na wachezaji 8 wa kimataifa na nafasi mbili katika dirisha dogo.
Wakati huo Yanga wamewanyakua nyota wafuatao Carlinhos, Farid Mussa, Yacouba Sogne, Michael Sarpong, Bakari Nondo, Abdallah Shaibu, Tuisila Kisinda, Mukoko Tunombe, Yassin Mustapha, Kibwana Shomary, Wazir Junior pamoja na Zawadi Mauya.
Hao wataungana na wengine ambao walibaki katika kikosi hicho, Yanga ni timu ambazo zimeonekana zinaweza kusumbua msimu ujao.
Azam FC
Wakati Azam FC wao wamefanya usajili wa kisayansi pia wamewachukua nyota kadhaa kuja kusaidiana na waliopo, Prince Dube, Ally Niyonzima, Emmanuel Charles, David Kissu, Awesu Awesu, Ismail Aziz na Ayoub Lyanga.
Yote hayo ni matakwa ya kocha Aristica Ciaoba ambaye anahitaji kusuka kikosi cha ushindani msimu ujao na ikiwezekana wachukue ubingwa wa ligu kuu Tanzania Bara.
Katika kuchagua zile tatu bora zangu Yanga, Simba na Azam FC wanabakia kuwa timu shindani msimu ujao.
Kagera Sugar itashika nafasi ya nne katika zile nafasi za juu kama nilivyoweza kuangalia usajili pamoja na utimamu wa timu.
Timu nyingine ambazo zimefanya usajili huku Ndanda FC iliyo daraja la kwanza imesajili nyota wa zamani wa Yanga na Simba.
Timu hiyo imewachukua Mrisho Ngassa usajili huru, Jerson Tegete, Nurdin Chona na Stamili Mbonde.
Wakati yote hayo yakiendelea Namungo FC imewaongeza nyota aliyeachwa na Yanga Jaffary Mohamed na Abdurhalim Humud aliyekuwa Mtibwa Sugar.
Huku Ruvu Shooting ikiwaongeza Juma Nyoso na Mohamed Banka, kocha mkuu akiwa Charles Boniface Mkwasa.
Kujiandaa kwa timu nyingi msimu huu katika dirisha la usajili unaonesha dhahiri kuwa msimu huu unaoanza Septemba 6 utakuwa wa moto sana.
Moja ya timu ambazo zimeonekana kujiimarisha ni pamoja na Kagera Sugar ambayo iliwatoa nyota wake muhimu wawili Zawadi Mauya kwenda Yanga na Aweso Aweso aliyetimkia Azam FC.
Imeachana na Juma Nyoso huku ikimuongezea mkataba mnono Yusuph Mhilu ndani ya timu hiyo.
Hizi hapa timu zitakazoshiriki ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao ambao utakuwa na timu 18.
Azam FC, Biashara United, Ruvu Shooting, Mbeya City, Tanzania Prison, Simba SC, Gwambina FC, Ihefu FC, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, JKT Tanzania, Namungo FC, Coastal Union, Polisi Tanzania, Mwadui FC, KMC, Dodoma Jiji na Young Africans.
Ratiba ya ligi ambayo itaanza Septemba 6 ni kama ifuatavyo, Yanga dhidi ya Tanzania Prisons wakati Simba itaanzia ugenini dhidi ya Ihefu FC ambayo imepanda daraja msimu huu.
Ratiba kamili ni kama ifuatavyo
Biashara United v Gwambina, Dodoma Jiji v Mwadui, Ihefu v Simba, Mtibwa Sugar, Ruvu Shooting v Namungo, Coastal Union, Young Africans v Tanzania Prisons, Azam v Polisi Tanzania, Kagera Sugar v JKT Tanzania, KMC v Mbeya City
Huo ni mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo msimu huu tukumbuke vitu vya kuangalia mfungaji bora, anayetoa pasi za mwisho, pamoja na nani anayepeleka mashambulizi.
Comments
Loading…