Taarifa zinaendelea kusambaa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Tanzania kupata uwakilishi wa timu nne katika michuano ya klabu bingwa Afrika.
Hii imekuja baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kutaja baadhi ya timu zilizo na uwakilishi wa timu nne huku Libya ikitupiliwa mbali licha ya kuwa na sifa za kuwakilisha.
Kuondolewa kwa Libya kunatokana na kufuta ligi yao ndani ya nchi hiyo.
Taarifa za ndani kabisa zimearifiwa kuwa timu ya Yanga na Azam FC zinaweza kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu Bingwa Afrika msimu huu, hii inatokana na baadhi ya nchi kufuta ligi zao kutokana na janga la Korona.
Nchi ambazo zimeanza kufuta ligi zao ni pamoja na Libya ambapo imefuta ligi ya nchi hiyo huku Shirikisho la soka la Africa (CAF) limeifungia nchi hiyo kushiriki michuano yanayoandaliwa na Shirikisho hilo kwa mwa huu.
UshirikiΒ wa Yanga na Azam utakujaje?
Kwanza ijitahidi imalize nafasi ya pili, ikimaliza nafasi hii itashiriki michuano ya klabu bingwa Afrika na huyu watatu ataungana Namungo FC ambayo tayari imekata tiketi ya kucheza michuano ya kombe la Shirikisho barani humo.
Pili Libya ipo nafasi ya 12 kwa viwango vya CAF ikiwa na alama 16.5, ina uwezekana wa kutoa timu nne.
Ila sasa hapa unaweza kuona inayofuatia ni Tanzania iliyo nafasi ya 13 ikiwa na alama 14, hivyo ni rahisi CAF kuifikiria Tanzania kuchukua nafasi ya Libya.
Kama haitoshi kuna nchi nyingine zimejitoa ikiwemo Sudan Kusini, Ethiopia na Jamhuri ya Afrika Ya Kati, hizo zote fursa kwa Tanzania kushiriki timu nyingi katika michuano hiyo.
Hili la Libya lilifahamika tangu wajitoe ila sasa kitendo cha CAF kutoa orodha ya timu zilizo na ushiriki wa timu nne ndio ukawa habari sasa.
Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao alipoongea na Mwanasports alijibu kuwa hata wao wanaona taarifa hizo katika mitandao.
Tuelewane kuwa kwa kawaida timu ambayo haina mashindano haipati nafasi ya kuingiza timu katika michuano ya CAF.
Hii inamaanisha kuwa hata Tanzania tungevunja ligi basi hata ushiriki wetu ungefungiwa na tusinge shiriki.
Comments
Loading…