in

Wachezaji wanaotia fora Euro 2020


MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Ulaya inaendelea katika majiji mbalimbali. Kwa sasa
mashindano hayo yamefikia hatua ya mwisho ya mechi za makundi kabla ya kupata timu 16
zitazopepetana kwenye mtoano kuelekea robo fainali,nusu fainali na kisha fainali. Michuano hii
ilisubiriwa kwa hamu kubwa baada ya kuashirishwa kwa miezi 12 zaidi kutokana na ugonjwa wa
corona uliotanda duniani mwaka 2020 hivyo kuhatarisha afya mashabiki.
Katika makala haya ninaangalia wachezaji waliotia fora kwenye hatua hizi za makundi kabla ya
kupata timu za mwisho za kusonga mbele na kisha bingwa wake. Niwachezaji walioonesha
kiwango kikubwa na kuwakuna mashabiki kote Ulaya.
Giorgio Chiellini (Italia)
Tangu alipoonesha cheche zake mara ya kwanza mwaka 2004 hadi sasa amechezea mechi 100
katika kikosi cha timu ya Taifa ya Italia. Nyota huyu wa Juventus ndiye msingi wa timu hiyo
maarufu kama Azzuri. Akiwa na miaka 36 Chielini anaonekana kuwa mchezaji muhimu ndani na
nje ya kikosi hicho, kwa kutoa uzoefu wake kwa vijana wa kocha Robertto Mancini. Amedumu
katika kikosi cha Italia kwa miaka 10. Italia imefuzu hatua ya 16 baada ya kushinda mechi zake.
Caglar Soyuncu (Uturuki)
Wakati Real Madrid ikiwa imeachana na nahiodha wake Sergio Ramos, tayari jina la mrithi
wake limekuwa likihusisha mastaa kadhaa akiwa Soyuncu. Nyota huyo ndiye chanzo cha
kung’ara Jamie Vardy, James Maddison na Kelechi Iheanacho kwa sababu ndiye mlinzi wao wa
kati mwenye uwezo mkubwa.
Soyuncu ni raia wa Uturuki ambaye amecheza mashindano haya kwa kiwnago kizuri tangu Juni

 1. Akiwa na miaka 25 amekuwa mhimili wa Uturuki. Ufundi,utulivu,maamuzi ya haraka na
  ubora wa kuondoa hatari za juu langoni mwao ndio sifa anazomwagiwa na mashabiki wa soka
  wakati huu wa mashindano.
  Oleksandr Zinchenko (Ukraine)
  Akiwa na umri wa miaka 17 tu, Zinchenko aliondoka Ukraine kukimbia vita na kwenda kucheza
  soka jijini Moscow kabla ya kusajiliwa na timu ya Ufa na baadaye Manchester City. Njia yake
  ya kufanikiwa katika soka ilikuwa ngumu, lakini ni mchezaji anayependwa na kuaminiwa na
  kocha Pep Guardiola katika nafasi ya beki wa kushoto. Amekuwa mchezaji muhimu wa Ukraine
  na anasifika kwa kucheza soka la kushambulia zaidi kama winga wa kushoto. Kipaji na uwezo
  mkubwa wa kusoma mchezo ni sifa zinazompa nafasi ya kung’ara katika mashindano ya Euro
  mwaka huu.
  Tyrone Mings (England)

Nyota huyo kutoka klabu ya Aston Villa anaelekea kumiliki safu ya ulinzi akishirikiana na John
Stones wa Manchester City. Mings akiwa mgeni kwenye mashindano ya kimataifa amefuta
wasiwasi uliotawala kuhusu nafasi hiyo kutokana na majeraha ya nahodha wao Harry Maguire.
Kocha wao Gareth Southgate ameonekana kupata jawabu mbadala katika safui ya ulinzi na nyota
huyo ameonesha kiwango cha juu,utulivu na uwezo wake wa kukabiliana na washambuliaji
hatari umeoneka. Ni kati ya wachezaji wa England ambao wametia fora hadi sasa.
Reece James (England)
Kati ya mabeki wa kulia ambao wametia fora hadi sasa kinda huyo kutoka Chelsea ameonesha
umahiri na utulivu. Kiwango bora alichokinesha kwenye mchezo wa fainali ya Ligi ya
Mbaingwa Ulaya dhidi ya Manchester City ndicho anachokionesha kwenye mashindano ya
kimataifa akiwa na England. Kwa sasa anamiliki nafasi ya beki wa kulia na kuwashaulisha
kabisa mashabiki wao ambao walitegemera Trent Alaxander Arnold huenda angecheza mbele.
pia amepora namba kutoka kwa benki mkongwe wa kulia wa England Kyle Walker wa Man
City mwenyer umri wa miaka 31. Kocha Southgate amempa jukumu Reece, naye analitendea
haki.
Federico Chiesa (Italia)
Hakuna mwneye wasiwasi kuhusu kiwango cha nyota huyo mwenye umri wa miaka 23.
Kuelekea mashindano hayo alikuwa na kiwango maridadi kabiwa ambapo mashabiki wa Italia
wanategemea kuona vitu adimu zaidi kutoka kwake. Katika msimu wa 2020-2021 alipachika
mabao 15 kwaajili ya Juventus, akiwa amezifumania nyavu za vigogo kama AC Milan na Inter
Milan.
Ronaldo (Ureno)
Akiwa na umri wa miaka 36 Ronaldo anaendelea kuonesha cheche zake. Uchu wa ushindi bado
umemtawala, akiwa anaongoza taifa hilo ambalo ni bingwa mtetezi wa Euro. Kwa sasa ndiye
mshambuliaji anayekaribia kuweka rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye wa muda wote wa
mashindano ya Euro tangu yaanzishwe mwaka 1960. Ronaldo amefunga mabao 12 tangu
alipoanza kucheza michuano ya Euro mwaka 2004.
Joshua Kimmich (Ujerumani)
Bingwa wa krosi matata na zenye kuzichachafya timu pinzani ndani ya dimba la Allianz Arena.
Kimmich anacheza nafasi ya kiungo wa pembeni kulia ili kumpisha Toni Kroos ambaye
anamiliki dimba la katikati akiwa na Ilkay Gundogun. Kimmich amekuwa akimimina majalo
makali na amekuwa chachu ya ushindi wa mabao 4-2 wa Ujerumani dhidi ya Ureno. Ushindi
ambao ulifufua matumaini yao ya kufuzu hatua ya 16.
Alexander Isak (Sweden)

Urefu,kasi,kupiga mashuti na uwezo wake wa kumiliki mpira ni miongoni mwa sifa ambazo
Sweden wanajivunia. Isa kana uzoefu wa miaka minne katika soka la kimataifa, nab ado anayo
safari ndefu ya kucheza kwani sasa ana umri wa miaka 21. Ni mshambuliaji ambaye anaonekana
kuchukua nafasi ya Zlatan Ibrahimovic. Isak anachezea klabu ya Real Sociedad.
Diogo Jota (Ureno)
Wengi walitegemea angepata nafasi ya kucheza, lakini hofu ilikuwa mfuo unaotumiwa na kocha
wake wa kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza. pia ushindani kutoka kwa vijana kama vile
Joao Felix na Andre ulitajwa kuwa tishio kwake kupata nafasi. Lakini kocha wake amempa
nafasi kikosi cha kwanza na ametia fora. Kwa sasa ana umri miaka 24, anayo nafasi ya kung;ara
zaidi.
Artem Dzyuba (Urusi)
Ingawaje Urusi wanaonekana kupepeusuka katika mashindano haya lakini mkongwe huyo
ameonesha uongozi na kuwavutia washabiki wengi. Anasifika kwa nguvu za mwili na ndio
silaha ambayo imekuwa ikiipa mafanikio klabu yake ya Zenit. Ni nyota anayesumbuana na
mabeki na ameonesha kuwa bado anayo nafasi ya kuonesha makali yake katika soka la
kimataifa, ingawaje kuna fununu kuwa huenda akastaafu soka la kimataifa.
Youri Tielemans (Ubelgiji)
Hakuna anayefikiria kiwnago cha kibou cha Edern Hazard ambaye amezidiwa hata na mdogo
wake. Kando ya wachezaji hao yupo Youri Tielemans ambaye anawapa kiburi Ubelgiji. Nyota
huyo wa Leicester City haitashangaza kama atawindwa na timu kubwa zaidi kwa sababu ana
kiwango na ufundi ambao unamwezesha kucheza katika vikosi ya sasa vya Man
United,Liverpool,Real Madrid,PSG,Man City au Barcelona. Jambo zuri zaidi bado yeye ni kinda
katika kandanda.
Lorenzo Insigne (Italia)
Huyu ni silaha ya ushindi ya kocha Mancini. Akiwa amevalia jezi yake nambari 10 mgongoni ni
mchezaji ambaye anaipa uhakika wa mabao Italia kutokana na kiwango na ufundi wake. Ni
winga wa kushoto na hupendelea kushambulia kutokea upande huo hata akama atapangwa
kucheza nafasi ya mshambuliaji wa pili. Kama kuna kitu cha kujivunia kwa kocha Italia basin i
kuwepo kwa mchezjai huyo kwenye kikosi chake. Ni mtu ambaye anaweza kuipa furaha wakati
wowote nchi yake.
Lucas Hernandez (Ufaransa)
Ufaransa imewahi kupata beki mahiri wa kushoto wakati wa fainali za kombe la dunia mwaka
1998 na Euro mwaka 2000, Baxcente Lizarazu. Mjadala ulikuwa nani atakuwa mrithi sahihi wa
Lizarazu, licha ya mabeki kadhaa kupita katika nafasi hiyo. Lucas Hernandez anaonekana

kumiliki nafasi hiyo kwa muda mrefu sasa ambaye anakipiga klabu ya Bayern Munich. Akiwa
na miaka 25 Lucas amekuwa mhimili katika kikosi cha Didier Deschamps na amecheza kwa
kiwango bora tangu kuanza mashindano hayo mwaka huu.
Dries Mertens (Ubelgiji)
Akiwa na miaka 34, Mertens anaonekana bado mchezaji muhimu katika kikosi cha Ubelgiji
kwenye mashindano haya. Nyota huyo wa Napoli amecheza kwa mafanikio msimu uliopita na
kupachika mabao 10, hivyo kumfanya kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Ubelgiji.
Kai Havertz (Ujerumani)
Huyu ndiye mfungaji wa bao la ushindi la Chelsea kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Cheche zake amehamishia kwenye mashindano ya Euro ambako alionesha makali hayo kwenye mchezo dhidi ya Ureno alipopachika mabao mawili safi na kuihakikisha Ujerumani Inapata pointi tatu na matumaini ya kufuzu hatua inayofuata.
Kocha Joachim Low amemwamini kinda huyo kuongoza safu ya ushambuliaji badala ya Timo
Werner kwa sababu ana nguvu na ujuzi katika kugombania mipira ya juu kjliko mwenzake.
Jordi Alba (Hispania)
Huyu anaonekana kama mkongwe katika kikosi cha Hispania akiwa anakiongoza kama nahodha
chini ya kocha Luis Enrique. Alba amekuwa mchezaji muhimu wa Barcelona na anaendelea
kuwika katika kikosi cha timu ya taifa licha ya changamoto ya kusaka ushindi kwenye mchezo
wa mwisho kujihakikisha kufuzu hatua ya pili. Kwa sasa ana miaka 32 na huenda ikawa ni
michuano yake ya mwisho kuitumikia Hispania.
Pedri (Hispania)
Kinda huyu ameendeleza cheche alizoonesha Barcelona msimu uliopita. Pedri amekuwa mchezaji
mbunifu na hatari kwa timu pinzani. Ana kasi, nguvu na ubunifu wa hali ya juu. Ni aina ya
wachezaji wanaowafaa Hispania kutokana na mfumo wa uchezaji wa kumiliki mpira kwa muda
mrefu na kupigiana pasi. Mtindo wake wa kucheza unafananishwa na mkongwe Andres Iniesta.
Pedri ameonesha kiwango kizuri kwenye michuano hii.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Faida na hasara za kuondoka Sergio Ramos

Yanga FC

Zoa zoa ya wachezaji itawanyima mafanikio Yanga