in ,

Wachezaji Sita ambao hawatakiwi kucheza Manchester United

Manchester United mpaka sasa hivi inapambana kuchukua nafasi nne za juu ili ipate nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao.

Lakini timu inaonekana kuwa na mwenendo wa kusua sua sana. Kuna baadhi ya wachezaji ambao wanaonekana hawana hadhi ya kuvaa jezi ya Manchester United.

SMALLING

Huyu anaonekana ni beki ambaye amekuwa akipata namba kwa siku za hivi karibuni. Lakini kiwango chake kimekuwa hakiendani na jina la klabu yenyewe. Amekuwa siyo madhubuti sana kwenye eneo la kujilinda.

PHIL JONES

Kuna wakati Manchester United ishawahi kuwa na Vidic pamoja na Ferdinand kwa wakati mmoja. Hawa walikuwa ni mabeki imara kuwahi kutokea katika timu ya Manchester United, hawa walikuwa mabeki ambao ni wa kiwango cha juu kabisa , kiwango ambacho Phil Jones hajawahi kukufikia na hana ndoto ya kuifikia

MARCUS ROJO

Huyu kwa msimu huu amecheza mechi nyingi na timu yake ya Taifa ya Argentina kuliko timu yake ya Manchester United. Amekuwa akisumbuliwa sana na majeruhi, majeruhi ambayo yamekuwa yakiyapa hasara zaidi Manchester United. Hivo wanatakiwa kumalizana naye kuliko kuendelea kuwa naye.

ASHLEY YOUNG

Ameitumikia sana timu yake. Ni jambo jema sana na anastahili heshima yake. Amekuwepo kwenye sehemu ya mafanikio ya Manchester United tangu enzi ya Sir. Alex Ferguson. Lakini kwa sasa ni muda sahihi kwake yeye kupumzika na kuziacha damu changa yeye pamoja na Antonio Valencia.

Eric Baily

Huyu ni beki ambaye wengi walikuwa na mategemeo naye makubwa sana lakini kwa kiasi kikubwa hajawahi kufanya kitu kikubwa kulingana na mategemeo ya wengi kutokana na majeruhi ya mara kwa mara.

Alexis Sanchez

Wakati anakuja Manchester United wengi walikuwa na mategemeo makubwa ya yeye kufanya vizuri lakini ikawa tofauti na mategemeo ya walio wengi. Umri unaenda na kadri ya siku zinavyozidi kwenda anazidi kufanya vibaya, angekuwa na umri mdogo angevumilika lakini kwa miaka 29 ni ngumu kuvumilika ni muda ambao yeye anaelekea kumaliza maisha yake ya mpira wa miguu.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Baada ya tokomeza zero ya JOKATE ifuate tokomeza fedheha ya KARIA

Tanzania Sports

Viongozi wana kiburi, Zahera ana jeuri, Wachezaji hawajui cha kufanya