in , ,

Wachezaji Man U waumia

Wachezaji Man U waumia

*Baadhi walikuwa wakipika

*Kuna aliyeg’atwa na mbwa

Hatua ya Serikali ya Uingereza kulazimisha watu kujifungia ndani, kujitenga na kujilinda dhidi ya virusi vya corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu, vimesababisha matatizo kwa baadhi ya wachezaji wa Manchester United.

Yawezekana kuonekana kama kichekesho au utani, kwani inaelezwa kwamba katika kukaa peke peke na kuingia kwenye harakati za kujihudumia, yupo mmoja aliyeumia wakati akipika chakula nyumbani kwake na mwingine akang’atwa na mbwa.

Baada ya Habari hizo kuvuja, klabu sasa wamesema kwamba wapo tayari kutoa rasilimali zaidi kwa ajili ya wachezaji ili kuwalinda na pia khuhakikisha afya ya akili inabaki kuwa nzuri wakati huu wa lockdown kukwepa Covid-19.

Daktari wa klabu hiyo, Steve McNaily anasema kwamba lazima wawasaidie wachezaji wao, kwa sababu kukaa ndani kwa muda mrefu sana bila kupata ushauri nasaha kunaweza kuwaathiri kisaikolojia.

Akasema kwamba wanafuatilia kwa karibu suala la afya ya wachezaji hao na athari wanayoweza kuwa wanapata kwa kulazimishwa kujifungia ambapo sasa ni kadiri ya mwezi mmoja. Anasema hiyo ni muhimu ili watakaporudi uwanjani wawe timamu kimwili na kiakili.

Wataalamu wa lishe nao wameanza kuwashauri wachezaji juu ya jinsi ya kujipikia wenyewe nyumbani kwa usalama, kwa sababu tayari ‘ajali’ kadhaa zimetokea huko jikoni wakati wakitekeleza jukumu hilo muhimu kwa afya zao, kwa wachezaji kadhaa kuungua na kupata majeraha mengine.

Mchezaji mmoja anaelezwa kwamba ilibidi akatafute ushauri wa mganga, baada ya kung’atwa na mbwa wake mwenyewe.

“Wataalamu wa lishe tayari wameanzisha ukurasa wa masomo ya mapishi kwa ajili ya vijana kupitia mtandao wa Instagram. Wengi wao (wachezaji) wameshaanza kupata stadi mpya za aina mbalimbali juu ya kupika baada ya hao kadhaa kupata majeraha wakiwa kwenye mchakato wa mapishi ya vyakula vyao.

“Kwa bahati nzuri vijana wanaendelea poa sasa. Hatupati tena taarifa za majeraha mapya japokuwa pamekuwapo matukio yasiyokuwa ya kawaida walipojaribu kutia mikono yao kwenye majiko kupka awali. Mwingine aling’atwa na mbwa wake. Aina hiyo ya mambo, ni mielekeo tofauti tu,” anasema McNally.

Juu ya hatua ambazo klabu inachkua kwa ajili ya kuwalinda wachezaji katika afya ya akili, daktarin huyu anasema kwamba ikiwa mambo yatakwenda kama yanavyotarajiwa kwa kurudi kwenye mazoezi mwez ujao, basi litakuwa jambo chanya. Anasema muda wa kukaa ndani ukiongezwa itabidi klabu ifanye zaidi kuwafundisha.

“Ikiwa watalazimika kubaki ndani mwao basi tutachukua hatua na kuwagwia rasilimali wanazohitaji. Hatutaki wajihisi kwamba wanatakiwa kuwa na matatizo ya afya ya akili lakini tutajitahidi kuwa karibu nao. Lazima tuwasiliane na vijana hawa mara kwa mara kuhakikisha wapo vyema, hasa wale ambao tuna shaka nao kwa jinsi tunavyowajua au kuhisi.

“Kufanya mazoezi kila siku ni ushindani sana na kwa hakika watakuwa wanakosa hilo pamoja na ile hali ya kutaniana na kuwa na uchanya kama kundi. Najua wanawasiliana katika makundi yao ya WhatsApp, lakini si sawa na kuwa pamoja. Patakuwapo na hali tofauti, kuna baadhi ya vijana mambo yao yatatenguka lakini wengine watabaki kujiongoza vizuri,” anasema daktarin huyo.

Jopo la makocha wa United limeanza kubuni njia za kuwafanyisha mazoezi kwenye uwanja wa klabu wa Carrington lakini wakiwa pia wanatimiza matakwa ya kukaa mbalimbali na kujikinga na maambukizi. Kwa sasa kila mchezaji anafuata programu ya kufanya mazoezi peke peke, lakini hatimaye walimu wanawapima kila Ijumaa asubuhi kujua walifanya kipi na kwa ufanisi gani

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Ozil agoma kukatwa mshahara

Tanzania Sports

‘Saudia wasiuziwe Newcastle’