in , , ,

Vita ya ufalme wa soka Misri

MASHABIKI wa soka barani Afrika wanafahamu juu ya umahiri wa nchi ya Misri katika mchezo wa soka. Bahati mbaya kama zilivyopoteana Nigeria, Ghana, Togo, Cameroon, Afrika kusini kwa kuzitaja chache ndivyo ambavyo Misri ilikumbana na wakati mgumu tangu kuondoka kwa kocha Hassan Shehata. Chini ya Shehata Misri ilikuwa na wafalme ndani ya uwanja, kama vile Mohammed Mido, Hassan Hossam, Amd Fatih Ahmed Hassan, Mohammed Gedo, na wengineo wengi. Katika soka la Afrika Misri ilikuwa inatawaliwa na mastaa waliocheza kandanda kwenye vilabu vya ndani na baadhi yao walikuwa wakicheza nje. Katika usakataji wa kandanda Misri walikuwa na majembe ya nguvu kwenye mashindano ya Afrika, kabla ya kuporomoka miaka ya karibuni. Licha ya kuwa na mastaa wengi kwenye timu yao hawakufuzu mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia. Baadala yake kizazi cha akina Mohammed Salah ambacho kilikuwa na wachezaji wenye vipaji vya wastani ndicho kilichofanikiw akufuzu fainali za Kombe la Dunia. Kwa muda mrefu Mohammed Salah ndiye mwanamfalme katika soka la Misri. Salah anasifika kupeperusha vyema bendera ya Misri kwenye mchezo wa soka. 

Vilabu vikubwa 

Tanzania Sports

Katika soka la Ulaya ukitaka mchezaji anayetoka Misri jina la Mohammed Salah limekuwa maarufu kwenye viwanja vingi vya soka barani Ulaya. Amecheza Basel, kisha akaenda Chelsea, na baadaye akaelekea Roma kabla ya kusajili na Liverpool. Salah alianza soka lake akiwa winga wa kulia na kushoto, lakini chini ya aliyekuwa kocha wake Jurgen Klopp alianza kumbadilisha kidogo kidogo kutoka winga hadi mshambuliaji. Zipo nyakati katika mfumo wa safu ya washambuliaji watatu, alipangwa kama mshambuliaji wa mwisho huku akizungukwa na mastaa wawili mahiri Sadio Mane na Roberto Firmino. 

Uchezaji wake umempa mataji mengi na kuweka rekodi nyingi za ufangaji kuanzia Liverpool hadi kwenye Ligi ya England kwa ujumla wake. Mohammed Salah ndiye mshambuliaji anayewinda kuandika rekodi ya kupachika mabao mengi katika Ligi Kuu England na kuwazidi mbali akiwa Theiry Henry (Arsenal), Alain Shearer (Newcastle United), Andy Cole na Dwight Yorke (Manchester United) na wengineo. Katika soka la Ulaya, Mohammed Salah ni bidhaa adimu katika kikosi. Licha ya ujio wa kocha mpya Arne Slots bado amekuwa kinara wa safu ya ushambuliaji. Bahati nyingine ni kucheza na wachezaji wakubwa katika klabu kubwa nchini England. Kwa sasa anafukuzuia rekodi ya kuwa mkongwe wa klabu hiyo kama alivyofanya Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.

Mtikisiko wa Mfalme wa Misri

Kama nilivyotangulia kusema Mohammed Salah ndiye mfalme wa soka Misri, ana rekodi ambazo hakuna mchezaji wa nchi hiyo anaweza kuzifikia. Mchezaji pekee ambaye anaweza kutambiana na Salah ni Hossam Hassan ambaye amecheza mechi nyingi za timu ya Taifa na miongoni mwa wanaoshikilia rekodi ya Shirikisho la soka duniani FIFA. Hata hivyo, kwenye Ligi ya England, jina la Mohammed Salah ndilo pekee ambalo lilikuwa limechukua sehemu kubwa ya uwakilishi wa Misri. Kwa washabiki wa soka wa Misri, huwaambii kitu kuhusu Mohamed Salah.

Hata hivyo Mohammed Salah amepokea kijana mwingine kutoka kwao Misri ambaye amekuja kutikisa Ligi Kuu England akiwa na klabu ya Manchester City. Pep Guardiola amemsajili nyota huyo kutoka Buneseliga ambako alikuwa moto wa kuotea mbali. Katika kuimarisha kikosi chakje kwenye usajili wa mwezi Januari, Pep Guardiola amekivuta kipaji cha Omar Marmoush raia wa Misri.

Kana kwmaba haitoshi akiwa na mwezi mmoja na siku akdhaa England amepachika ‘hatrick’ yake kwanza kwenye mchezo dhidi ya Newcastle United ya Eddie Howe. 

Je Marmoush ni mchezaji wa aina gani?

Kwanza yeye ni winga wa maeneo mawili kushoto na kulia. Lakini anaweza kucheza kama mshambuliaji wa kati. Katika uchezaji wake Marmoush ndiye mchezaji ambaye anaelekea kuwa na kasi kama Mohammed Salah. Kwenye kikosi cha Man City kuna mawinga watatu wenye kasi, Savinho, Doku na sasa Marmoush. Ni mchezaji ambaye anao uwezo wa kutumia miguu yote miwili, kulia na kushoto. Anaweza kupiga mashuti makali, anafunga mabao kwa vichwa, krosi na uwezo wa kukokota mpira ni wa hali ya juu. spidi yake anapocheza mpira ndiyo ile ambayo anayo Mohammed Salah.

Je ni mfumo gani unaomfaa zaidi?

Omar Marmoush kama ilivyo kwa Moahmmes Salah anaweza kutumika katika mfumo wa 4-3-3 au 3-4-3 pamoja na 3-4-2-1. Bahati nzuri katika kikosi cha Man City kuna mshambuliaji namba moja Erlin Haaland. Kwa maana hiyo Omar Marmoush anaweza kucheza eneo hilo endapo Haaland atakuwa majeruhi au mabadiliko ya mfumo. Usajili wake ni mbadala wa Julian Alvarez aliyehamia Atletico Madrid. Mfumo wa Pep Guardiola ni ule unaowapa wabunifu nafasi kubwa ya kuamua matokeo ya mchezo. Kwa mgfano Bernado Silva na Phil Phoden wanakuwa msingi wa safu ya ushambuliaji, huku Marmoush na Savinho wakipishana kucheza ama kupangwa pamoja. Kama mshambuliaji huria, Marmoush ana kasi kuliko Haaland. Kama ukokotaji wa mpira na wenye mwelekeo basi Marmoush ndiye mchezaji anayeweza kuiikimbiza Man City muda mwingi.

Je, Marmoush anaweza kumtikisa Salah?

Kila zama na kitabu chake. Kiufundi Marmoush anampa kocha vitu vitatu; kasi, mashuti na maarifa ya kufunga mabao ua kutengeneza mabao. Ni vitu kama hivyo ndivyo vinampa nafasi kubwa Mohamed Salah kutamba katika kikosi cha Liverpool na timu ya taifa ya Misri. Ni sahihi kusema Marmoush ndiye anatakiwa kuchota mengi kutoka kwa Moahmmed Salah. Lakini pia kiubinadamu Marmoush amekuja EPL kuleta changamoto ya ufalme wa Misri katika kandanda. Kwa maana hiyo ushindani wa nani zaidi kati ya wachezaji wa Misri ni miongoni mwa mambo yatakayokuwepo katika Ligi kuu England. Pep Guardiola amewaleta kwenye vita ya ufalme Omar Marmoush na Moahmmed Salah.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

UONGOZI YANGA UACHE PAPARA KAMA MAN UNITED 

Tanzania Sports

Chipukizi Man Utd kwenye rada ya Ruben Amorim