in , , ,

Van Gaal: Mke ataniondoa United

*Aston Villa wamsajili Jordan Ayew
*Drogba ajiunga na Montreal Impact

Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amesema huenda akaondoka klabuni hapo ndani ya miaka miwili kwa sababu ya ahadi aliyompa mkewe Truus.

Van Gaal (63) alisaini mkataba wa miaka mitatu na tayari amemaliza miwili na anasema kwamba huenda 2017 akaondoka.

“Nilimuahidi mke wangu hivyo. Kwamba hatuna tena miaka mingi pamoja na hiyo ndiyo sababu. Nimemaliza kila kitu kama kocha tangu kwingine nilikotoka,” akasema Van Gaal.

Aliongeza kwamba alikuwa amemuahidi kwamba angeachana na masuala ya ukocha akifikisha miaka 55 lakini wiki ijayo anafikisha miaka 64 na bado anafanya kazi.

“Kitu pekee kipya nilichotaka ni kufundisha klabu ya Ligi Kuu ya England (EPL) na sasa niko hapa. Je, nina haja ya kwenda Qatar kutafuta fedha zaidi? Sidhani. Natakiwa kufurahia maisha na mke wangu,” anasema LVG ambaye mkewe wa kwanza, Fernanda, alifariki dunia kwa saratani 1994.

Kocha huyo anasema Man United wanahitaji mchezaji nyota kama Cristiano Ronaldo ili kuwa na ushindani wa kweli dhidi ya timu kubwa.

Anatoa mfano wa wachezaji wengine wazuri ambao wangefaa, japokuwa anaamini Ronaldo anaweza kurejea Old Trafford ni wa Bayern Munich, Franck Ribery na Arjen Robben; wa Chelsea, Eden Hazard na Willian; wa Real Madrid, Gareth Bale; wa Barca, Neymar na Lionel Messi.

VILLA WAMSAJILI JORDAN AYEW
ayew

Aston Villa wamemsajili mshambuliaji wa Ghana, Jordan Ayew kwa mkataba wa miaka mitano.

Ayew, 23, anaingia Villa Park akitoka Lorient ya Ufaransa na pia aliisaidia nchi yake kushika nafasi ya pili kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu.
Villa wamefanya usajili huo baada ya kumuuza mshambuliaji wao wa kati kutoka Ubelgiji, Christian Benteke kwa Liverpool kwa pauni milioni 32.5.
Ayew anakutana na wachezaji wengine aliyekuwa naye Ligi Kuu ya Ufaransa – Ligue 1, Jordan Amavi na Idrissa Gueye.

Villa walimpoteza pia nahodha wao, Fabian Delph aliyejiunga na Manchester City, lakini wameshawasajili Scott Sinclair, Micah Richards na Mark Bunn , hivyo huenda wakawa na msimu mzuri kuanzia Agosti hii.

DIDIER DROGBA AJIUNGA MONTREAL
diid

Mshambuliaji mkongwe wa Ivory Coast aliyeondoka Chelsea, Didier Drogba amejiunga na klabu ya Montreal Impact ya Major League Soccer (MLS), Canada.

Drogba, 37, ameondoka Stamford Bridge kiangazi hiki baada ya kucheza mechi 381na kutwaa ubingwa wa England mara nne na wa Ulaya mara moja akiwa na klabu hiyo.

Mmiliki na Rais wa Montreal, Joey Saputo alisema kusaini kwa Drogba katika klabu yake kumeifanya hiyo kuwa moja ya siku kubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo.

“Ni heshima kubwa kumwalika Didier Drogba hapa. Tangu mazungumzo yangu ya kwanza naye nilihisi kwamba alitaka kuchezea Montreal. Kuwasili kwake kutafaidisha kila eneo,” anasema rais huyo.

Drogba anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi kwa Ivory Coast, ambapo katika mechi 105 amefunga mabao 65.
Drogba ameingia kwenye Ligi ya Amerika Kaskazini kama ilivyo kwa Frank Lampard aliyejiunga na New York City.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

MOBUTU ALIVYOPELEKA MATUMAINI ANFIELD

KERR ANATARAJIA MIUJIZA