in , , ,

Van Gaal aanza kazi Man U

Kocha mpya wa Manchester United, Louis van Gaal ameanza rasmi kazi Old Trafford na kutamka kwamba yeye ni mwanademokrasia.

Katika mkutano wake wa kwanza na wanahabari Alhamisi hii, Mdachi huyo aliyeteuliwa kushika wadhifa huo Mei mwaka huu na kubaki na Timu ya Taifa ya Uholanzi kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia, amesema ni kweli ni mkali, lakini anajali utu.

Watu kadhaa waliofanya naye kazi wamewaonya wachezaji wa Manchester United kutocheka tu kwa kumpata, bali wajue watalazimika kufanya kazi ya ziada kuendana na matakwa yake.

Van Gaal (62) amesema atarejesha hali sawa Old Trafford baada ya mambo kwenda mrama msimu uliopita chini ya David Moyes aliyemrithi Sir Alex Ferguson. Van Gaala ametwaa ubingwa wa Uholanzi na Ajax (1993-94, 1994-95, 1995-96), Barcelona (1997-98, 1998-99), AZ Alkmaar ya Uholanzi  (2008-09) na Bayern Munich (2009-10).

Alitwaa ubingwa wa Ulaya na msimu wa 1994-95 na Kombe la Uefa na klabu hiyo hiyo 1991/92. Amesema tetesi zinazoanza kutolewa juu ya mfumo wake wa ukocha si wa haki na kwamba vyombo vya habari vinataka kuonesha kwamba ni mkali, na bahati mbaya ikirudiwa sana watu watadhani ni mtu asiyejali watu.

Van Gaal alitangaza katika mkutano huo kwamba kingo Michael Carrick ameumia kwenye mazoezi na atakuwa nje kwa ‘muda mrefu’ lakini akaitaja Manchester United kuwa ndiyo klabu kubwa zaidi duniani.

Amesema kwamba atataka kuona kikosi chake cha sasa kinafanyaji kwa zaidi ya wiki tatu au nne kabla ya kuamua iwapo kuna haja ya kuongeza wachezaji wengine. Ijumaa hii United wanakwenda Marekani kuanza ziara ya michezo mbalimbali kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya England mwezi ujao.

Alisema ni yeye aliyetoa idhini ya kusajiliwa kwa wachezaji Ander Herrera wa Mexico na  Luke Shaw wa Uingereza msimu huu kwa sababu anawapenda. Akizungumzia kuhusu nani atakuwa nahodha, Van Gaal alisema wachezaji wote wana nafasi ya kuteuliwa, lakini inabidi kwanza awajue vyema.

Hata hivyo, alikiri ni kazi ngumu kuwanoa United kutokana na wadau kutarajia makubwa mno, lakini akasema ikiwa alifundisha klabu kubwa zaidi Hispania, Uholanzi na Ujerumani, mwelekeo anaoutaka ni huo, kwamba atajitahidi sana kufanya vyema.
 
 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

England yaporomokea nafasi ya 20

Tanzania tayari kwa Madola