in ,

Tanzania tayari kwa Madola

Timu ya Tanzania kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola imewasili katika  uwanja wa ndege wa Kimataifa Glasgow, Scotland jana usiku (Alhamis, 17 Julai 2014) kwa ndege ya Shirika la ndege la Falme za Kiarabu (Emirates).

Jumla ya wanamichezo 42 waliwasili Uwanjani hapo na kupokelewa  na Afisa Ubalozi wa Tanzania London Bw. Amos Msanjila. Pamoja na mapokezi na shamrashamra za wenyeji, baadhi ya Watanzania waishio Glasgow walikuwepo Uwanjani hapo wakipeperusha bendera za Tanzania kuwahamasisha wanamichezo hao.

20140718-085204-31924129.jpg

Pichani, Bw. Msanjila akimkabidhi bendera ya Tanzania Nahodha wa Timu hiyo Selemani Kidunda. Wengine pichani ni Kiongozi wa Msafara Bw. Muharame Mchume na Mkurugenzi wa Michezo Bw. Leonard Thadeo.

Michezo ya Jumuiya ya Madola inayotarajiwa kufunguliwa rasmi Jumatano (23 Julai 2014) na Malkia Elizabeth wa Pili itajumuisha nchi na Himaya 70. Michezo hiyo itafungwa tarehe 3 Agosti 2014.  

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Van Gaal aanza kazi Man U

Nahodha Ujerumani aachia ngazi