*Mpira ni mahesabu, siku zote hesabu ukiipatia umeipatia kweli na
ukiikosea umeikosea kweli*
Conte kaingia kwenye mechi akiwa hana wachezaji wake muhimu, wachezaji
ambao walionekana kuwa nyota msimu uliopita.
Hilo halikuwa tatizo, tatizo lilikuwa anakutana na timu ngumu kipindi
ambacho wachezaji wake muhimu hawapo mikononi mwake.
Ndipo hapo alihitaji kutuliza kichwa ili kuzikokotoa hesabu hizi ili
aibuke na majibu ya ukweli.
Hesabu ambazo zilimtaka ni kwa jinsi gani ataweza kuziba pengo la
Cahil kule nyuma.
Kumweka David Luiz kama kiungo wa chini kulisaidia kwa kiasi kikubwa
kuwalinda mabeki vizuri .
Pia kuliwapa uhuru Bakayoyo na Kante kucheza eneo huru kuanzia
katikati mwa uwanja.
Pia asili ya Kante ni kuzuia , Bakayoyo ana asili ya kuzuia pia.
Ukichanganya na David Luiz basi utagundua kulikuwa na aina tatu ya
viungo ambao uwezo wa kuzuia upo ndani yao.
Pamoja na kwamba Bakayoyo na Kante walionekana huru mpaka wakawa
wanasogea mbele kusaidia kushambulia
Lakini pia walisaidia kujaza watu eneo la kati hali ambao iliwanyima
uhuru mkubwa Spurs kwa sababu kila walipokuwa wanajaribu kupitia
katikati kulikuwa na idadi kubwa ya watu.
Suluhisho pekee kwa Spurs lilikuwa kutumia pembeni ili kuwatanua
Chelsea ili eneo la katikati mwa uwanja waliacha wazi ili wao wamtumia
Ericksen kutengeneza nafasi kwa uhuru.
Au kupitia pembeni walikuwa na nafasi kubwa ya kutengeneza nafasi za
kufunga kupitia krosi.
Lakini hakuwakufanikiwa kwa sababu hawakuwa na watu wenye kasi pembeni.
Timu nzima ilikuwa ina press polepole hali ambayo ilikuwa inawafanya
pia Chelsea watulie muda mwingi mwa mchezo bila presha kubwa sana.
Ndiyo maana hata walipokuwa wanaanzisha mashambulizi ya kushtukiza
walikuwa wanafanikiwa kwa kiasi kikubwa.