in

Ujio wa Chikwende ndiyo mwisho wa Morrison?

Chikwende

Jana kuna vitu viwili vilitokea jana ambavyo ni vya kufikirisha sana. Kitu cha kwanza ni kuhusiana na Bernand Morrison. Jana kulisambaa sauti ya mmoja wa wajumbe wa bodi ya Simba, Kassim Dewji.

Sauti hiyo ilikuwa ikielezea sababu kuu ya kwanini Bernard Morrison hachezi kwenye mechi za hivi karibuni. Bernard Morrison alionekana kwenye wachezaji wa akiba kwenye mechi zote za mashindano ya mapinduzi.

Pamoja na kuonekana kwenye orodha ya wachezaji wa akiba lakini hakuweza kupata hata dakika moja ya kucheza kwenye michuano hiyo kitu ambacho kiliibua maswali mengi sana.

Maswali haya yanajibiwa jana na Kassim Dewji kwa kutuambia kuwa Bernard Morrison hachezi kwa sababu kwa sasa ni mgonjwa wa ngiri.

Ugonjwa ambao utamwihitaji yeye kwenda kufanyiwa upasuaji. Upasuaji ambao utamweka nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi sita (6). Kipindi ambacho ni kirefu sana kwa mchezaji wa mpira wa miguu.

Kipindi ambacho kinaweza kusababisha jina la Bernard Morrison kupotea. Kitu hiki kilinifanya nimkumbuke Bernard Morrison. Bernard Morrison wa kipindi kile ambacho alikuwa mfalme Yanga.

Bernard Morrison
Bernard Morrison

Bernard Morrison ambaye aliibeba Yanga kwa miguu yake ya dhahabu. Miguu ambayo iliwavutia Simba kumsajili. Usajili ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa na migogoro mingi sana lakini mwisho wa siku Bernard Morrison alisajiliwa Simba.

Rasmi akawa mchezaji wa Simba ikawa furaha kubwa sana kwa mashabiki wa Simba. Utaachaje kufurahia kipindi ambacho mchezaji bora anapokuja kwenye timu yako?

Furaha hii ilizidi kipimo, ikawa imemlevya Bernard Morrison, taratibu akaanza kusahau majukumu yake ya uwanjani. Takwimu zake za uwanjani zikawa zinashuka kila siku.

Jana ndiyo imetoka taarifa ya yeye kuumwa  ngiri na anatakiwa kufanyiwa upasuaji ambao utamweka nje kwa kipindi cha miezi sita. Baada ya hii taarifa ilitoka taarifa nyingine ya Simba kumsajili Perfect Chikwende.

Mchezaji wa zamani wa FC Platnumz. Mchezaji ambaye aliwafanya Simba katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya uliofanyika nchini Zimbabwe.

Bonge moja la mchezaji, hili halina ubishi. Ubora wake wa uchezaji unatia maswali mengi kuhusiana na Bernard Morrison. Perfect Chikwende anacheza nafasi ambayo Bernard Morrison anacheza.

Bernard Morrison anaenda kufanyiwa upasuaji na atakuwa nje kwa miezi sita kwenye kikosi cha Simba anakuja Perfect Chikwende. Hofu yangu kipindi ambacho Bernard Morrison hayupo, Perfect Chikwende anakuja kubeba ufalme ambao Bernard Morrison alijiwekea Msimbazi?

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Yanga Vs Simba

Tuanze kumuomba samahani Onyango!

Waamuzi wa Tanzania

Marefa wa Tanzania ni mizigo?