Michezo yote 10 ya wiki ya saba ya EPL imeshachezwa. Kwenye makala hii mwandishi wetu amechagua kikosi cha wachezaji 11 waliofanya vizuri kwenye michezo ya EPL wiki hii.

 

Golikipa: HUGO LLORIS (Tottenham)

Alitoa mchango wa kutosha dhidi ya Man City. Aliokoa michomo ya hatari kutoka kwa Kolarov, Sterling na Jesus Navas kwenye vipindi vyote viwili kwenye mchezo huo ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa mabao manne kwa moja.

 

Mlinzi wa Kulia: DARYL JANMAAT (Newcastle)

Alimdhibiti Eden Hazard kwa kiasi kikubwa na alipandisha vizuri mashambulizi ya Newcastle hapo juzi hasa kwenye kipindi cha kwanza. Kutokana na kujaribu kulinda mabao ya timu yake kipindi cha pili alilazimika kupunguza mashambulizi.

 

Mlinzi wa Kati: BREDE HANGELAND (Crystal Palace)

Aliiwezesha Crystal Palace kumaliza mchezo wa juzi bila kuruhusu bao dhidi ya Watford. Hilo liliwezekana kutokana na mlinzi huyo kuwazima washambuliaji wa Watford wakiongozwa na Ighalo kila walipojaribu kuleta madhara.

 

Mlinzi wa Kati: VIRGIL VAN DIJK (Southampton)

Ingawa Swansea walipiga mashuti 11 kwenye mchezo wa juzi lakini mengi kati ya hayo yalipigwa na viungo nje ya eneo la hatari. Washambuliaji wa Swansea walidhibitiwa vyema na van Dijk na hawakuweza kudhuru ngome.

 

Mlinzi wa Kushoto: MATTEO DARMIAN (Manchester United)

ppp

Kwenye mchezo dhidi ya Sunderland hapo juzi Darmian aliliziba vema pengo la majeruhi Luke Shaw. Kiwango alichoonyesha kwenye mchezo huo kinatosha kabisa kumfanya van Gaal aendelee kumtumia kama mbadala wa Shaw.

 

Kiungo wa Kati: ERIC DIER (Tottenham)

Siri ya mafanikio ya Tottenham kwenye mchezo wa hapo juzi dhidi ya Manchester City ilikuwa namna Dier alivyowazima viungo wa Manchester City dakika zote za mchezo. Ushindi wao wa 4-1 ulichangiwa mno na kiwango cha Dier.

 

Kiungo wa Kati: JAMES MILNER (Liverpool)

Ukiacha bao la kuongoza aliloifungia Liverpool dhidi ya Aston Villa hapo juzi Milner alionyesha kiwango kikubwa kwenye mchezo huo. Alikuwepo kila mahala alipohitajika na akatekeleza vyema majukumu yake uwanjani.

 

Kiungo wa Kulia: ERIK LAMELA (Tottenham)

Winga huyu aliwapa tabu mno walinzi wa Manchester City kwenye mchezo wa juzi. Kiwango alichokionyesha kilitosha kabisa kumfanya ang’are kwenye mchezo huo baada ya kutengeneza bao moja na kufunga lingine zuri.

 

Kiungo wa Kushoto: ALEXIS SANCHEZ (Arsenal)

Huyu hahitaji maelezo mengi. Hat-trick aliyoifungia Arsenal kwenye mchezo wa hapo juzi dhidi ya Leicester City imemfanya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick kwenye ligi zote tatu za Italia, Hispania na England.

 

Mshambuliaji: DANIEL STURRIDGE (Liverpool)

Majeraha yalimuweka nje kwa miezi mitano lakini hapo juzi kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa mshambuliaji huyu alionyesha kuwa hahitaji muda mrefu kurudi kwenye ubora wake. Aliwasumbua walinzi na akaifungia timu yake mabao mawili.

 

Mshambuliaji: ROMELU LUKAKU (Everton)

Lukaku alimalizia vizuri nafasi alizopata kwenye mchezo wa jana dhidi ya West Bromwich na kufunga mabao mawili likiwemo bao la ushindi alilofunga kwenye dakika ya 84. Zaidi ya hapo Lukaku alitoa pasi ya bao la Arouna Kone.

Advertisement
Advertisement

Report

Written by Kassim

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

ZAMBIAN COACHES HAVE THE PREMIER SKILLS

Tanzania Sports

Fifa: Warner afungiwa maisha