Michezo yote 10 ya wiki ya nane ya EPL imeshachezwa. Kwenye makala hii mwandishi wetu amechagua kikosi cha wachezaji 11 waliofanya vizuri kwenye michezo ya EPL wiki hii.

 

Golikipa: HEURELHO GOMES (Watford)

 Heurelho Gomes
Heurelho Gomes

Alikuwa shujaa wa Watford hapo juzi dhidi ya Bournemouth. Gomes aliokoa mashuti kadhaa makali kutoka kwa washambuliaji wa Bournemouth ukiwemo mkwaju wa penati uliopigwa na Glenn Murray na kuiwezesha timu yake kupata sare ya 1-1.

 

Mlinzi wa Kulia: NATHANIEL CLYNE (Liverpool)

Pengine timu yake haikupata matokeo iliyokuwa ikiyahitaji kwenye mchezo wa jana lakini Clyne aliwapa changamoto mno wachezaji wa Everton kwenye upande wa kulia kutokana na mashambulizi aliyopandisha hasa kwenye kipindi cha kwanza.

 

Mlinzi wa Kati: PER MERTESACKER (Arsenal)

Petr Cech alifanya kazi ya zaida hapo jana kuhakikisha timu yake inamaliza mchezo bila kuruhusu bao dhidi ya United. Hata hivyo akili na nguvu za Per Mertesacker zilichangia kumlinda golikipa huyo kwa kipindi kirefu cha mchezo huo.

 

Mlinzi wa Kati: VIRGIL VAN DIJK (Southampton)

Virgil van Dijk
Virgil van Dijk

Mlinzi huyu  ameendelea kuonyesha ubora wake hapo juzi dhidi ya Chelsea. Alichangia kwa kiasi kikubwa mno kuwazuia mabingwa hao watetezi wasitengeneze nafasi za kufunga kwenye mchezo huo ambao Chelsea walilala 3-1 nyumbani.

 

Mlinzi wa Kushoto: JEFFREY SCHLUPP (Leicester City)

Kwenye kipindi cha kwanza Schlupp alihusika na mashambulizi mengi yaliyowaonya Norwich lakini hawakuweza kumzuia mlinzi huyo wa kushoto asiwadhuru dakika za baadae. Alistahili kuifungia timu yake bao alilofunga kwenye ushindi wa 2-1.

 

Kiungo wa Kati: GARETH BARRY (Everton)

Anaweza asiwe mmoja wa walioonekana sana kwenye mchezo wa jana ambapo Everton walitoka sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Liverpool. Lakini Barry alitawala vyema eneo la kiungo hasa katika kipindi cha pili cha mchezo.

 

Kiungo wa Kati: KEVIN DE BRYUYNE (Manchester City)

Mkali wa pasi za mabao. Alitengeneza mabao mawili na kufunga lingine safi kwenye mchezo ambao Manchester City waliibuka na ushindi wa mabao sita kwa moja dhidi ya Newcastle na kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England.

 

Kiungo wa Kulia: MARKO ARNAUTOVIC (Stoke City)

Marko Arnautovic wa Stoke City, akishangilia bao lake.
Marko Arnautovic wa Stoke City, akishangilia bao lake.

Winga huyu alihusika na karibu kila shambulizi la Stoke City kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa hapo juzi. Alitumia nafasi aliyopata kwenye dakika za mwanzo za kipindi cha pili cha mchezo na kuifungia timu yake bao pekee la ushindi.

 

Kiungo wa Kushoto: ALEXIS SANCHEZ (Arsenal)

Baada ya kuzamisha hat-trick wiki iliyopita hapo jana Sanchez aliendeleza makali yake alipowafanya walinzi wa United kuonekana si kitu kutokana na namna alivyowanyanyasa na kuifungia timu yake mabao mawili kwenye ushindi wa 3-0.

 

Kiungo Mshambuliaji; CHRISTIAN ERIKSEN (Tottenham)

Tottenham walitoka nyuma mara mbili kwenye mchezo wa jana na kufanikiwa kuambulia sare ya 2-2 kutokana na maajabu aliyoonyesha Eriksen kwa kusawazisha mabao kupitia mikwaju miwili mikali ya mipira ya adhabu iliyozama wavuni.

 

Mshambuliaji: SERGIO AGUERO (Manchester City)

Huyu ndiye nyota wa wiki hii. Alidumu uwanjani kwa dakika 66 pekee kabla ya kumpisha Wilfried Bony lakini aliingia kwenye orodha ya wachezaji waliowahi kufunga mabao matano kwenye mchezo moja wa Ligi Kuu ya England.

Advertisement
Advertisement

 

Report

Written by Kassim

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

NIPENI NAMBA YA MOURINHO TAFADHALI

Tanzania Sports

AW: ALIBADILI MBINU KUWAANGAMIZA MAN U