*Angel Di Maria aelekea Man United?
*Man City wamfuata Elaquin Mangala
*Rio Ferdinand QPR, Khedira Arsenal

Pilika pilika za usajili zinaendelea, ambapo inaelezwa kuwa Barcelona wanaelekea kukamilisha mkataba wa kumnunua Luis Suarez wa Liverpool kwa pauni milioni 80.

Liverpool wamekataliwa ofa yao ya pauni milioni 20 kwa mlinzi wa Southampton, Dejan Lovren (24) na wamekasirishwa na uamuzi huo, kwani Lovren alishawaambia Saints hataki kubaki hapo kwa msimu ujao.

Real Madrid wamewapa Manchester United fursa ya kumsajili winga wao, Angel Di Maria (26) kwa pauni milioni 40. Arsenal, Paris St-Germain na Juventus wanamtaka mchezaji huyo pia.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini atafanikisha dili la kuwasajili kwa pauni milioni 35 Alexis Sanchez (25) na Mathieu Debuchy (28).

Kadhalika watatoa ofa ya pauni milioni 20 kwa kiungo wa Southampton, Morgan Schneiderlin (24), huku Napoli wakiingia kwenye vita ya kumnasa Mfaransa huyo.

Bayern Munich wanapambana na Manchester United, Liverpool na Arsenal kumnasa winga wa Fiorentina, Juan Cuadrado (26). 

Arsenal wameweka mezani kwa Real Madrid pauni milioni 23.8 ili kumsajili kiungo mshambuliaji wao, Sami Khedira (27) na watamtumia rafiki na Mjerumani mwenzake, Mesut Ozil kumshawishi ahamie Emirates.

Manchester City wanaelekea kufanikisha dili la uhamisho wa mlinzi Mfaransa wa Porto ya Ureno, Elaquim Mangala (23) kwa pauni milioni 32.

Hata hivyo, wanasubiri kuona iwapo Chelsea nao wataweka mezani chochote, kwani kocha Jose Mourinho anamtaka mchezaji huyo.

Juventus wanataka kumsajili beki wa Manchester United, Patrice Evra (33) aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita hapo Old Trafford.

Barcelona wamesema wataajiri mtaalamu bingwa wa saikolojia kwa ajili ya kutuliza ‘mashetani ya kung’ata’ ya Luis Suarez akikamilisha mkataba wa kuhamia Nou Camp. 

Queen Park Rangers (QPR) wanatarajiwa kukamilisha usajili wa beki wa kati aliyeondoka Manchester United, Rio Ferdinand (35) atakayeungana na mwalimu wake wa awali, Harry Redknapp.

Phil Neville anatarajiwa kuondoshwa kwenye nafasi yake ya ukufunzi wa timu ya kwanza Man United, kwani kocha mpya, Louis van Gaal anatarajiwa kuleta mtu mwingine hapo.

Kipa wa Chelsea, Petr Cech (32) anaelezwa kwamba huenda akaondoka Stamford Bridge kiangazi hiki.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Wajerumani wapata homa

Ujerumani wawafurusha Ufaransa